Maji ya chupa ni maji ya kawaida. Tofouati yake ni katika processing. Yapo yanoyoongezwa madini na yapo yanayopunguzwa kutokana na asili yake.
Tatizo linaweza kujitokeza katika kuandaa na hapo yakawa contaminated kama inavyoweza kutokea kwa kitu kingine.
Yapo madai yanayochunguzwa kuhusiana na plastic zinazotumika. Wapo wana sayansi wanadai kuna plastic nyingine huchanganywa na vitu ambavyo huwa na madhara. Hata hivyo imebaki kuwa ni mjadala usio na hitimisho hadi sasa.
Tukumbuke kuwa vitu vyote vinavyoingia katika 'processing' za viwanda mara nyingi hupoteza uasili, achilia mbali madhara yatokanayo na uandaaji ikiwa ni pamoja na hifadhi.