Madhara ya matumizi mabaya ya dawa ya kushusha presha (viagra)

miyanga

Member
Joined
Dec 24, 2015
Posts
38
Reaction score
55
Salam wanajamvi;

Leo napenda kwa ufupi tuangalie juu ya matumizi haya mabaya ya dawa ya kushusha presha almaarufu kama viagra kama kichwa cha nyuzi yetu kinavyojieleza.

Viagra ni dawa inayopatikana madukani hasa maduka yanayouza dawa za binadamu(pharmacy). Dawa hii ni ya vidonge na hutumika kumudu presha iliyopanda na kupelekea kufanya presha ishuke.

Watumiaji wa dawa hii wengi wao walikuwa wazee tena wale wenye matatizo ya kupanda kwa presha(hypertension) ili kuwasaidia kushusha presha.

Dawa hii ina kiambatanisho kinachoitwa sidenafil ambacho huwa kinafanya mishipa ya damu kutanuka na kupelekea kushuka kwa presha(hypo tension)

Matumizi mabaya
Kwa muda mrefu ilileta utata baada ya kuwa wazee yani watu wazima wanaoenda kuchukua dawa hospitalini kurudi kutaka tena dawa ikiwa muda wa dozi haujaisha na kupelekea kufahamika kuwa kuna matumizi tofauti na ambayo sio ya kawaida kama alivyoelekezwa na mtaalam wa dawa yani mfamasia.

Hiyo inatokana na madhara(side effects) yatokanayo na kiambatanishi(sidenafil) kinachopatikana katika dawa hiyo maarufu( viagra). Matokeo au madhara makubwa yanayoletwa na dawa hii ni kusababisha uume kusimama(erection) kwa uwezo usio wa kawaida na kufanya mtu kuwa na uwezo mkubwa katika tendo la ndoa.

Vijana & wazee wengi kutokana na wimbi lililopo sasa la kupungukiwa nguvu za kiume na kushindwa kuwa na uwezo(performance) wakati wa kufanya tendo la mdoa na kupelekea kushindwa kudumu katika tendo hilo hatimaye kutomridhisha mwenzie wengi wao hupelekea kutumia dawa hii ili kuwasaidia katika shughuli hiyo adhimu ya tendo la ndoa.

Wengine hufika mbali kimawazo yani kutaka apate sifa kwa mwenzie kuwa yeye ni bingwa katika sekta hiyo. Hatima yake hupelekea addiction kwa wale wanaotumia vibaya bila kufata maelezo ya mfamasia na mbaya zaidi hupelekea vifo vya ghafla kipindi mtu akiwa anafanya tendo la ndoa.

Ikumbukwe dawa hii hupelekea kushuka kwa presha kwahiyo unapoitumia bila maelekezo kutoka kwa mtaalam wa dawa inaleta matatizo ambayo kwa sasa hupelekea vifo vingi vya ghafla kwa watu kipindi wakiwa wanafanya tendo la ndoa kwani hushusha presha nakupelekea kifo cha ghafla.

Ombi langu kwa wanajamvi usitumie dawa bila kufata ushauri wa mtaalam wa dawa yani mfamasia.

Viagra haitibu upungufu wa nguvu za kiume matokeo ya kusimamisha mara baada ya kuitumia dawa hiyo ni madhara yatokanayo na dawa hiyo(side effect) hivyo basi tujikite kuimarisha afya zetu tupendelee kula matunda na mbogamboga na tujiepushe kula vyakula ambavyo tunashauriwa si vizuri kwa afya zetu.

Tunapoteza watu na nguvu kazi ya taifa kwa vifo vya ghafla vinavyoshtuwa watu wengi kutokana na matumizi haya ili kupata nguvu ya ziada kutekeleza tendo la ndoa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…