damian marijani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2010
- 695
- 466
Wana JF, heshima kwenu wote,
Imekuwa 'fashion' siku hizi kuona watu wengi kupenda kula nyama iliyosindikwa haswa kwa wale ambao wana kipato kinono au hali yao kiuchumi haijayumba.
Nyama iliyosindikwa (processed meat) ni nyama ambayo imeongezwa kemikali ili iweze kukaa muda mrefu kwenye shelf za maduka ikisubiri walaji.
Baadhi ya kemikali zinazotumika ni kama ifuatavyo:-
. phosphates - inaongezwa kusaidia unyevunyevu wa nyama
. nitrates - inaongeza rangi ya nyama na kuifanya kuonekana fresh
. texturisers - inafanya nyama iwe laini kutafunika
. stabilizers - inaongeza ubora wa nyama kuweza kukaa muda mrefu bila ladha kubadilika.
.monosodium glutamate - inaongeza ladha ya nyama.
Nyama zilizosindikwa tuzionazo kwenye soko ni kama sausage (soseji), bacon, ham, pastrami, bologna, salami, pepperoni, nyama za baga na nyinginezo.
Nyama isiyosindikwa ni ile ambayo haijaongezwa kemikali yeyote ile kama nyama inunuliwayo buchani.
MADHARA:
1.Kisukari - Nyama zilizosindikwa zimeonekana kuongeza hatari ya kuwa na ugonjwa wa kisukari kutokana na kemikali za nitrates. Kemikali ya nitrate imeonakana kudhoofisha utoaji wa hormone ya insulin mwilini ambayo ndiyo inayosaidia na kuratibisha matumizi ya sukari katika damu.
2. Magonjwa ya moyo - Nyama zilizosindikwa haswa nyekundu (beef, nyama ya mbuzi) zinachochea mchomo (inflammation) ndani ya mwili kutokana na mafuta ya aina ya omega 6. Kutokana na hali ya mchomo huu, mishipa mikubwa ya damu inaathirika na kuweka utando wa cholesterol ukutani wa mishipa kusababisha hypertension na ugonjwa wa moyo.
3. Cancer - Hali ya mchomo (inflammation) wa muda mrefu inaweka mwili hatarini ya uwezekano wa kupata cancer ya kongosho (pancrease) kutokana na sumu mbali mbali zilizo kweye nyama iliyosindikwa. Sumu mojawapo iliyopo kwenye hizi nyama ni mycotoxin ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo, ini na figo.
4. Mlipuko wa magonjwa - Baadhi ya nyama hizi hazipikwi sawa sawa hivyo kutouwa vimelea vya magonjwa mbali mbali ya wanyama wafugwao kama listeriosis,liver flukes n.k
Kutokana na madhara yaliyotajwa hapo juu, mlaji anatahadharishwa kulinda familia na yeye mwenyewe kuepuka nyama zilizosindikwa na kujaribu kutumia zaidi samaki, vyakula vya njugu, jamii ya maharage (legumes) na nyama isiyo na mafuta.