Madhara ya nyama iliyosindikwa

damian marijani

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2010
Posts
695
Reaction score
466
Wana JF, Imekuwa ni "fashion" kuna watu wengi wakila nyama iliyosindikwa siku hizi. Mara nyingi hii inajitokeza zaidi kwa wale ambao hali zao kiuchumi ni nzuri.
Nyama iliyosindikwa (processed meat) ni nyama ambayo imeongezwa kemikali ili iweze kukaa muda mrefu kwenye shelf ikisubiri mlaji.
Baadhi ya kemikali zinazotumika kusindikia nyama hizi ni kama zifuatazo
*Phosphates - inaongezwa kusaidia unyenyevu wa nyama,
*Nitrates - inaongeza rangi ya nyama na kuifanya kuonekana fresh,
*Texturizers - inafanya nyama kuwa laini kutafunika,
*Stabilizers - inaongeza ubora wa nyama kuweza kukaa muda mrefu bila ya kubadilika ladha, Mono *Sodium Glutamate - inaongeza ladha ya nyama.
Nyama zilizosindikwa ambazo tunaziona kwenye soko ni kama sausage (soseji), bacon, ham, pastrami, Bologna, salami, pepperoni, nyama za burgers na nyingine nyingi.
Nyama ambayo haijasindikwa ni ile ambayo haijaongezwa chochote kile kama nyama tunayoinunua buchani.
MADHARA

1. Nyama zilizosindikwa zimeonekana kuaongeza hatari ya kuwa na ugonjwa wa kisukari kutokana na kuwa na kemikali za nitrates. Kemikali ya nitrate imeonekana kudhoofisha utoaji wa hormone ya insulin amba husaidia katika matumizi ya sukari katika damu.
2. Magonjwa ya moyo: Nyama zilizosindikwa haswa nyekundu (red meat) e.g. beef, nyama mbuzi zinachochea mchomo (inflammation) ndani ya mwili kutokana na kuongeza kwa kiasi kikubwa mafuta aina ya Omega 6. Kutokana na hali hii ya mchomo (inflammation) mishipa mikubwa ya damu inaathirika na kuweka utando wa cholesterol na kusababisha hypertension na ugonjwa wa moyo.
3. Cancer: Hali ya mchomo wa muda mrefu unaweka mwili kwenye hatari kubwa ya uwezekano wa kupata cancer ya kongosho (pancreas) kutokana na sumu mbali mbali zilizoko kwenye nyama zilizosindikwa. Sumu mojawapo ni mycotoxin mbayo vile vile inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo, ini na figo. Kutokana na madhara yaliyotajwa hapo juu, mlaji anatahadharishwa kulinda familia yake na yeye mwenyewe kuepuka nyama zilizosindikwa na kujaribu zaidi kula nyama ya samaki, vyakula vitokanavyo na njugu, jamii ya maharage (legumes) na nyama isiyo na mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…