Madhara ya Serikali ya Mseto

Akifanyà hivyo atapata upinzani mkubwa roka chama chake kule Zanzibar inawezekana sababu ni takwa la kikatiba na nguvu za kisiasa hazipishani
 
Mkuu kuna tofauti kati ya serikali ya mseto na maamuzi ya Rais kushirikisha/kuteua upinzani kwenye utendaji. Lakini pamoja na utofauti huo bado ni turufu nzuri zaidi kwa upinzani kama mtu atakuwa mzalendo yaani kufanya kazi kwa maslahi mapana ya taifa, ila tatizo la nchi zetu viongozi wetu wote wapo kimaslahi yao binafsi. Na hapo ndio mama atakapo rubuni wapinzani kwa njia za busara, utapewa nafasi ili uonje kwanza halafu ndio linakuja sharti la kwamba kama una taka kubaki kwenye hiyo nafasi toka huko jiunge upande huu ama baki kwenye chama chako na hiyo nafasi tumpe mwingine mwenye shida nayo.
 
Wacha kupiga kelele, wacha muda uongee. Mama aambiwe ukweli, tiba ya kweli kwa Taifa letu ni katiba mpya iliyoandaliwa na Warioba
Nu kweli. Hivi vinafasi ni peremende tu
 
Uwepo wa vyama vingi una umuhimu zaidi kwa taifa kuliko kushirikishwa moja kwa moja kwenye serikali.
Intelijensia ya kimataifa inaonesha kwamba vyama mbadala husaidia taifa kuuma na kupuliza mataifa mengine.
Kwa mfano serikali ya CCM iliwahi kuingia mikataba ya hovyo ambayo siyo rahisi kuivunja.
Kinaingia chama kingine kinavunja na baadaye CCM ikirudi inawabembeleza walalamikaji kwa makubaliano mapya yenye unafuu.
 
Chief nimekuelewa. Ila kunakijimkwamo Fulani hivi kinacholitesa taifa. Kinatokana na uchaguzi uliopita. Hivi unadhani kwanini Ndugai anawang'ang'ania covid 19. Ngoja tusubiri tuone
 
Hahahaa.... yaaniii....

Mimi siku zote nina mashaka na hawa wanaoitwa wapinzani. Hawaelewi nini wanachotaka.

Hakuna Mtanzania mwenye “monopoly” ya upinzani. Bila shaka unaongelea CHADEMA hapa. Basi ni bora uwataje wao kabisa na uijue misimamo yao rasmi wala isiwe kusoma kauli za manazi hapa JF.

In any case, “upinzani” na “wapinzani” is too general. Sidhani kama bandiko lako linawahusu vyama kama UDP, NCCR, ACT, n.k.
 
we umeelewaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…