Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
SHAMBA LA KOROSHO JIMBO LA KERALA INDIA: KOROSHO TAMU LAKINIII MM,…..MADHARA YAKE NI MAKUBWA!
Jimboni Kerala kuna shamba la kampuni ya Kasaragond Cashew Plantation.Hili ndilo lililokuwa shamba kubwa la Korosho nchini India miaka île ya 1940s – 1970s. Shamba hili lilianzishwa na bepari McKenzie enzi ya ukoloni wa Waingereza.
Kwa miaka kadhaa lilikuwa likinyunyiza sumu (viatilifu au pembejeo) aina ya Organophosphate. Siku si nyingi wakulima kule Mtwara walidai sumu aina ya Sulfur iliingizwa ikiwa tayari ime expire. Wizara ikadai itamshughulikia muingizaji.
Ukweli ni kwamba hata ikiwa haija ecpire matokeo ndiyo haya tunayo-ona kwenye picha hizi.
Kuanzia mwaka 2003 -2007,nilikuwa Mratibu wa mradi uitwao Global Pesticides Project uliokuwa unafadhiliwa na SIDA (Sweden), nikizunguka dunia nzima kufundisha madhara ya sumu za Kilimo kwa afya ya binadamu na mazingira. Pia nikikagua utekelezaji wa mkataba wa ILO number 170 wa mwaka 1990 (ILO Convention on Chemical Safety in Work Places),Nikifundisha Afrika, Ulaya, Asia, America kusini.
Safari moja nikafika Kerala India. Nikakutana na hili shamba la korosho la Bwana Mackenzie. Kwa miaka mingi katika shamba hili walikuwa wana-nyunyiza sumu kwa kutumia helikopta kutokana na ukubwa wa shamba. Helikopta ikimwaga sumu mpaka mashuleni, majumbani, visima vya maji, mtoni, n.k.,dhumumi kubwa likiwa kudhibiti ugonjwa wa ukungu kwenye mikorosho.
Hali hii ni sawa na Mtwara, tofauti ni kwamba, Mtwara hawatumii Helikopta,bali mabomba ya mgongoni(Knapsack Sprayers). Mara nyingi mabomba hayayanavuja mgongoni mwa mbebaji,analowana chapachapa.
Mara nyingi pia wanaonyunyiza hawana mavazi ya kinga au wanakula au kuvuta sugars huku wananyunyiza. Mara nyingine pia wanachanganya sulfur kwa kutumia mikono. Mbaya zaidi,wanatumia makopo yaliyo-hifadhi sulfur,kwa kuhifadhia maji, maziwa, unga au hata nafaka.
Utasikia wizara na wanaharakati wakidai “Mwaka huu tutapeleka sulfur ya kutosha Mtwara kabla ya msimu kuanza!” Au “Serikali ipeleka haraka Sulfur kuepuka hasara kwa wakulima!" Kamwe hutasikia “serikali itatoa haraka elimu kwa wakulima kuhusu madhara ya sulfur!" Masikini wakulima! Wanashukuru kwa kuletewa sulfur ya kutosha! Wangelijua madhara yake huenda wangeandamana kudai vifaa ya kinga, elimu, matibabu n.k..
Namsikilizaga Zitto Kabwe “akitetea” wakulima wa korosho kwamba "wapelekewe Sulfur haraka!" Najua dhahiri hajui chochote kuhusu ubaya(toxicity) ya sulfur! Angedai kwanza elimu au sumu mmbadala. Zipo ambazo ni salama zaidi ukilinganisha na sulfur.
Huyu Binti mrembo ukimuangalia haraka utadhani kaota titi. La hasha! Ni uvimbe wa Kansa ya Titi,Kiingereza ikiitwa Breast Cancer. Kansa hii kaipata utotoni. Hawa watoto waliosimama ukutani hawana akili hata chembe.
Ni "makolo" ya kihindi! Hawaelewi chochote darasani. 1+1 ni ngapiii? wanajibu chochote. Miaaa, thelathini nk.Walimu wamefundisha weee...wamefundisha tuisheni weee....lakini wapi. Ukimtuma dukani lazima umuandikie karatasi,bila hivyo utashangaa karudi kuuliza “mama ulinituma ninunue nini vileee?" Hâta mara 5. Ataenda anarudi kuuliza.
Hawa wenye ulemavu waliupata tumboni mwa mama zao. Organophosphate inaweza kuingilia ukuaji wa mtoto tumboni mwa mama. Ina sifa 2 "Kipare" tunaita “Endocrine Disruption” na “Cholinesterase Inhibition”. Endocrine ni tezi inayosimamia ukuaji “growth & development” mtoto Akiwa tumboni kwa mama. Cholinesterase ni “Enzyme” ambayo inasimamia mawasiliano baina ya mama na kichanga tumboni.
Inachofanya sulfur au Organophosphate yeyote,ni kuingilia mawasiliano hayo. Mfano inageuza meseji ya “ota vidole vitano kila mkono” n’a kuifanya mtoto aisome hivi “ota vidole viwili kila mkono”. Mwili wa kichanga utadaka hii meseji feki. Atazaliwa mlemavu kadri ujumbe ulivyochezewa.
Nilibahatika kuwatembelea hawa watoto. Wengine tuliwasaidia. Kama huyu wa mguu. Tuligharamia operesheni ya kukata mguu wa kulia na kumpa mguu bandia. Hii ilimwezesha kutembea kwenda shule.
Ushauri: wizara isijikite tu kupeleka sumu kwa wakulima.Ijikite pia kutoa elimu na mavazi la kinga kwa wakulima na walaji.
Angalizo: Mtu anapo-bugia Bibi,korosho au ulaka akumbuke kwamba ilinyunyiziwa Sulfur!!Watu wanaweza kuadhurika shule ikagoma wakakimbilia umachinga.Wakati mwingine sio kosa lao,wamebugia Sulfur! Najua Ntwara korosho ni viagra! Shauri yenu mtakwisha.