JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Surua ni nini?Surua au kwa Kiingereza “measles” ni ugonjwa unaosababishwa na virusi. Ugonjwa wa surua unaweza kumpata mtu wa rika lolote ila huathiri zaidi watoto. Dalili za awali za surua ni koo kuuma, kikohozi , homa na madoa ya rangi ya kijivu au nyeupe kwenye sehemu ya ndani ya mashavu. Baada ya siku chache, upele mwekundu hutokea.
Dalili za Surua
Surua huweza kuambatana na dalili kama za mafua, kwa mfano kupiga chafya, macho kuwa mekundu na homa. Dalili nyingine ni kuonekana kwa madoa ya rangi ya kijivu au nyeupe kwenye sehemu ya ndani ya mashavu. Baada ya siku chache upele unatokea kwenye ngozi, mara nyingi unaanzia kichwani na shingoni.
Ugonjwa wa Surua kama hautadhibitiwa mapema unaweza kusababisha madhara kadhaa wa Mgonjwa:
Matatizo katika masikio
Homa ya mapafu ‘pneumonia’
Upofu wa macho
Homa ya uti wa mgongo
Kupoteza maisha