MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,537
- 8,824
Madhara ya Wamachinga/Wachuuzi Mijini na nini kifanyike.
Kwa Miaka ya hivi Karibuni hasa kipindi cha awamu ya 5 kumetokea wimbi kubwa sana la Vijana/Wamachinga/Wanyonge ambao wameamua kujiajiri kwa kuchuuza bidhaa barabarani.
Hii inawasaidia sana kujipatia ridhiki ya kila siku.
İla Wimbi hili la Vijana kuja Mijini hasa Miji mkibwa ni la kasi sana na la hatari sana na linaweza lisiwe na tija kwa Vijana wenyewe na pia kwa Taifa.
Madhara ya Umachinga/Uchuuzi Mijini
İkumbukwe kwamba Uchuuzi au Umachinga uko nchi nyingi sana Duniani. İngawa nchi nyingi wana utaratibu na pia asilimia ya uchuuzi inakuwa sio kubwa sana na Serikali za nchi zao wana Discourage sana uchuuzi tofauti na huku kwetu ambako unapaliliwa na kuungwa mkono kwa nguvu zote.
1. Nguvu kazi kupungua sana Vijijini.
Amini usiamini kwa sasa vijijini wamebakia wazee ambao hao ndo tunao tegemea walime vyakula vije mijini.
Vijana wanakimbilia sana mijini kwa sababu ni rahisi na pia hakuna vikwazo kwa wao kufanya uchuuzi barabarani.
Kwa baadae tunaweza pata changamoto ya nguvu kazi hasa vijijini kwenye kilimo na hii ikaleta Balaa la njaa baadae au upungufu wa Chakula.
2. Kujenga Taifa ambalo ni la watu wasio fikiria au kuwaza sana, Taifa la wanao tegemea kubebwa muda wote, Taifa linalo tegemea ready made tu, Taifa la wachuuzi, Taifa la wasio ongeza thamani bidhaa.
Umachinga una attract hata wanafunzi Mashuleni na vyuoni na wanaona ni kitu rahisi sana kwao kufanya na wapo wanao ota kuwa wamachinga au wachuuzi.
Hii ni hatari sana kwa baadae.
3. Serikali itakuja kushindwa kuwafanyia re alocations huko mbele ya safari,
Hawa wamachinga wamesimika hadi vibanda vyao na wanaamini wako pale kihalali, hii itakuja kuleta upinzani mkubwa sana kwa Serikali kipindi cha kuwahamisha.
4. Kukosa Mapato, Serikali inapaswa sana kuhamasisha Formal sectors na sio İnforma sectors ambazo hazina mchango wa maana kwenye Taifa.
5. Uharibifu wa miundo mbinu, Mandhari ya miji, angalia mfano wa Posta ilivyo sasa hivi, hii ni hatari sana.
6. Kuchangia sana uchumi wa nje kuliko uchumi wa Taifa, make asilimia karibia 99 ya product zinazo uzwa ni Made in China au İndia na kadhalika, hii inachangia sana kukuza uchumi wao kuliko wetu.
7. Kusababisha Majanga kwa baadae, wamama wanapika hadi pembeni mwa Petro stations, hii ni hatari sana kwa usalama wa watu na pia Mali zao.
8. Afya ya watu iko hatarini, mazingira ya vyakula vinako pikiwa ni hatari sana, na İnatia wasiwai usalama wa kinacho pikwa hapo.
Nini Kifanyike Sasa na Serijali na sisi Jamii?
1. Wamachinga/Wanyonge wapewe Grace period ya wao kufanya uchuuzi,
Hapa ni kwamba Serikali iandae maeneo yao na pia kuwe ni kwa muda maalumu baada ya hapo wanatakiwa kutoka sasa wakapambane kutafuta Frame zao wenyewe hapo waingie wengine wapya. Wawe wana graduate.
2. Kipaumbele cha Uchuuzi kitolewe kwa Bidhaa za ndani, hasa za mikono na pia vitu kama Matunda
Bidhaa zinazo zalishwa kwa mikoni zipo Dunia nzima hata kwenye mataifa yenye uchumi mkubwa kabisa kama İndia au Japan, Serikali ije na Conditions za watu watako pewa kipa umbele wawe ni wale wanao uza bidhaa za Made in Tanzania, hii ita pushi sana viwanda vya ndani.
3.Uchuuzi wa kupika hasa vyakula na kuwasha mioto barabarani upigwe marufuku kwa nguvu zote kabisa, na watu waruhusiwe kuuza tu product za kawaida.
4. Baadhi ya maeneo Uchuuzi au Umachinga Upigwe marufuku kabisa na maeneo hayo yabakie kwa biashara kubwa tu au kwa ajili ya watu kupumzika, Uchuuzi uwe ni maeneo yebye masoko au Standa kubwa na baadhi ya maeneo yabakie tu kwa Biashara kubwa kubwa.
5. Uharibifu wa Mazingira, Wamachinga wabanwe kabisa kwenye swala la uhalibifu wa mazingira na wawajibike kabisa kutunza yale maeneo wanayo fanyia Uchuuzi wao. Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake inapo kuja swala la mazingira.
6. Kuwe na siku na masaa maalumu ya kufanya uchuuzi au Umachina.
Masaa baada ya kazi ni mazuri sana na siku za weekend na siku za sikukuu pia ni siku nzuri sana.
Hapa watu wengi wanakuwa wameisha move kutoka mijini na wako majumbani mwao ao kuna kuwa hakuba movement kubwa ya watu.
7. Serikali ihamasishe kwa nguvu zote formal sector au sekita rasimi, Uchuuzi usi paliliwe kabisa.
8. Sekita kama za Kilimo zipewe kipa umbele kikubwa hasa vijijini ambako ndo vijana wanakimbia kutoka huko, Kilimo kikipewa kipaumbele na vijana wakaona tija kwenye kilimo hakika hawatakimbilia sana mijini kufanya umachinga.
9. Serikali ihamasishe uwekezaji vijijini, wawekezaji wanao wekeza Vijijini wapewe kipaumbele na upendeleo wa kutosha ili basi hawa watoe ajira kwa vijana na vijana wapunguze kwenda mijini kufanya uchuuzi.
10. Tujenge kizazi cha İnovations, tuhamasishe vijana kuwa inovative sana na kuacha kutegemea kufanya uchuuzi, hii itawezekana kupitia mifumo ya elimu kubadilishwa na pia kuwa na Sera nzuri za ubunifu.
11.Siasa isiwe inapewa kipauumbele kwenywe maswala ambayo inaonekana kabisa hayana tija sana kwa Taifa. Ukiangalia swala la Wamachinga hawa kuna kutumika kisiasa sana na kuliko kutumika kiuchumi.
12. Sheria za Miji ziwe kali kidogo kuvunja watu moyo kukimbilia mijini,
Hata jamii yenyewe, Wazazi, ndugu jamaa na marafiki tunapaswa kusaidia hili ili tujenge kizazi cha inovation na sio kizazi cha kuwa jalala la bidhaa za mataifa ya nje. Tuwaelimishe watoto wetu wachukia sana Uchuuzi na wawe wabunifu.
Mwisho.

Upvote
1