Madhara ya zinaa

kwinyo

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2017
Posts
281
Reaction score
230
MADHARA YA ZINAA KISAYANSI

Wengi katika wanadamu
wanajaribu kuhoji kwa nini
Mwenyezi Mungu anakataza zinaa
wakati kuingiliana baina ya mke na
mume na kuingiliana baina ya
hawara na hawara mambo ni yale
yale, sasa kwa nini akataze???
Kwanza ifahamike kwamba
Mwenyezi Mungu akikataza jambo
basi ujue lina hasara kwetu kwa
kulifuata na lina faida kubwa kama
tukiliacha. Tofauti na wanadamu,
kwa mfano; Serikali inakataza
pombe ya Gongo kwa madai kuwa
ni haramu wakati Bia pia ni pombe
lakini ni halali! Hiyo ni kwa mujibu
wa serikali za ulimwengu. Lakini
katika UISLAMU Mwenyezi Mungu
akisema pombe ni haramu basi
iwe Gongo,Bia,n.k zote ni HARAMU.
Ndivyo pia ilivyo ZINAA, leo
ulimwenguni kuna zinaa ya halali
wenyewe wanaita “zinaa salama
ya kutumia Condom” lakini uislamu
umeharamisha kabisa zinaa,

Mwenyezi Mungu anasema katika
Qur’an, sura ya 17 Bani Israil aya ya
32;
“Na wala msiikaribie ZINAA, hakika
ya hiyo zinaa ni uchafu na njia
mbaya”
Hapo Mwenyezi Mungu amekataza
Zinaa, tena amesema hiyo zinaa ni
uchafu. Haya ni maneno aliyosema
Mwenyezi katika karne ya saba (7).
Je? Watu wa kanuni za maumbile
wanakubaliana kwamba ndani ya
zinaa kuna uchafu? Na kama upo
ni upi? Hatuwezi kuujua uchafu wa
zinaa mpaka tutazame katika
mafundisho ya wanasayansi wa
sasa yaani MODERN SCIENTISTS ili
tujue wamekubaliana vipi na
Qur’an bila wenyewe kujua. Wakati
tunatafuta kujua uchafu wa zinaa
na madhara yake kisayansi lazima
kwanza tujue vitu vikuu vine:
(1) Uchafu ni nini?
(2) Manii yanatoka wapi kwa
mwanaume.
(3) Manii yanatoka wapi kwa
mwanamke.
(4) Na ndani ya manii mna nini.
Tunapozungumzia uchafu kwa
tafsiri ya jumla ni kitu
kilichowekwa mahala pasipostahili.
Mfano; kuchukua kiatu chenye
thamani ya laki moja ukakanyaga
matope kisha kiatu kile ukakiweka
juu ya kitanda cha kawaida na
godoro la sufi ambacho thamani
yake kwa ujumla havifiki elfu
arobaini; lakini pamoja na thamani
ya kiatu kuwa kubwa kuliko
kitanda na godoro mtu akija
atauliza huu uchafu aliyeweka
hapa juu ya kitanda ni nani? Kwa
nini aite kiatu cha gharama
uchafu? Ni kwamba kimekaa
pahala pasipostahili. Hivyo kitendo
cha mwanaume au mwanamke
kupokea au kupeleka manii yake
pahala pasipokuwa halali yake huo
ni uchafu.
Kwa upande wa mwanaume
tunapozungumzia utoaji wake wa
manii ni mfinyo wa glands(tezi) za
aina tano; ambao mfinyo huu
unapatikana baada ya mwanaume
kupata stimulation(msisimko) na
hapo ndipo tezi hizi hujibinya na
kutoa maji ya aina tano tofauti
yanayokutana katika makende na
kuchukua mbegu kisha yanatoka
katika hali na rangi ambayo wengi
tunaifahamu. Glands hizi za
mwanaume zimefungwa baina ya
kifua na mgogo.
Kwa mwanamke manii yake
yanatoka katika Glands za aina
mbili tu ambazo hizi zimefungwa
katika kifua chake. Hivyo maji haya
yanayotoka katika glands hizi mbili
yakichanganyika na ya mwanaume
jumla yanakuwa maji ya aina saba
(7) yakikaa katika pahala
panapokusudiwa kwa mwanamke
na kwa muda maalum hapo ndipo
inapopatikana mimba na kizazi cha
binadamu kinaendelea.
Baada ya kujua hatua ya mwanzo
yanapotokea manii sasa tuingie
katika hatua ya pili ya kujua je?
Ndani ya manii mna kitu gani
kitaalamu. Ndani ya manii mna vitu
vikuu vine:
• PROTEIN
• ACID
• SPERM/CHROMOSOME
• VIRUS
PROTEIN: Ni aina mojawapo ya
“Food Substance” inayorutubisha
mwili. Substance hii inapatikana
ndani ya manii na pia watu wa
mambo ya reproduction system
(mfumo wa uzazi) wanakubali
kwamba manii yanatokana na aina
hii ya chakula na ndiyo maana
kama una njaa shughuli ya Jimai
inashindikana, au kama
utajilazimisha utapata madhara.
ACID: Ni mfano wa tindikali, yaani
kitu chenye ladha ya ukali mfano
ndimu. Na kitu chenye tindikali
kina kawaida ya kuunguza na pia
kulegeza kwa itakayompata au
kumuingia, ndiyo sababu kitaalam
ukimlinganisha mwanamke
aliyeolewa na asiyeolewa kisha
akawa hafanyi zinaa maumbile yao
yanatofautiana. Yule aliyeolewa
mwili wake unakuwa laini zaidi
sababu ya acid inayopatikana
ndani ya manii. Nitakupa mifano
mingi iliyo hai ili akili yako ikubali
kwamba vyote vinavyotajwa
vinapatikana ndani ya manii.
Ukitaka kuthibitisha zaidi acid ya
katika manii ambayo inaunguza
nakulegeza hata ukiwa na kidonda
kibichi ukitia manii kitauma mara
mbili zaidi sababu ya acid. Mfano
mwingine tazama kwa wale
watoto wa kiume ambao
wanaingiliwa kinyume na
maumbile (mashoga) hata kama
zamani alikuwa strong (imara)
kiasi gani akiingiliwa tu, basi
analegea kuanzia kutembea,
kuzungumza na kila kitu sababu ni
Acid inayopatikana ndani ya manii.
Pia ndio maana inakatazwa
kumuingilia mwanamke
anayenyonyesha sababu
ukimuingilia ukamuingizia manii
ambayo yana acid, acid ile itapanda
katika maziwa na kuyaharibu
maziwa na hapo mtoto akinyonya
atanyonya maziwa yenye acid.
Itasababisha mtoto kulegea au
kwa watu wa pwani wanaita
kubemendwa, hivyo mtakua
mmemharibu mtoto. Lakini kama
atakula acid ya baba yake
hatadhurika sana, sababu atakula
acid ambayo kwa asili ndiyo
iliyomtengeneza. Ila mkeo
akiziniwa na mtu mwingine mtoto
ataathirika sana na pengine
itakuwa ni sababu ya kifo chake
kwa kuwa amekula acid ambayo si
ya asili kutoka kwa wazazi wake
hivyo itakuwa ni POISON (sumu)
kwake. Kazi kubwa ya acid kwenye
manii ni kuua bacteria zisizohusika
zinazopatikana wakati zikitoka
kuelekea katika virginal wall.
SPERM: Ni mbegu za kiume
zinazopatikana ndani ya manii na
hizi mbegu haziishi ndani ya mwili
kwa sababu ya hali ya joto la mwili,
kwani mtu wa kawaida ambaye
haumwi anakuwa na nyuzi joto 37
hivyo mbegu zitakufa kutokana na
joto la ziada. Wataalamu wa
mambo ya reproduction na
gynecology wanatueleza kwamba
mshindo mmoja una wastani wa
watoto milioni 200 hadi 300.
Lakini yanayofanikiwa kulifikia yai
ni mia moja tu. Na yanayofanikiwa
kuingia kwa kawaida ni moja au
mawili yakizidi sana manne tu, na
si zaidi ya hapo, lau kama yakizidi
basi ni kwa miujiza yake Mwenyezi
Mungu.
VIRUS: Hivi ni vijidudu ambavyo kila
mtu anavyo vya kwake na pia
haviingiliani baina ya mtu na mtu
na hapa ndipo tutaeleza kwa kina
madhara ya zinaa kisayansi. Lazima
pia tujue kuwa Virus wanafanya
kazi gani na pia wanakwenda
wapi. Katika virginal wall kuna
vijistomata (vitundu) maalum kwa
ajili ya kupokea virus; sababu
mwanaume anapotoa manii yake
yenye protein,acid,sperm/
chromosomes na virus kila kimoja
huchukua nafasi yake kwenda
kunapohusika. Nafasi ya virus ni
kuingia katika vitundu vilivyo
katika virginal wall ili vipate kuishi
humo kwa kuwa ndipo
alipowapangia Mwenyezi Mungu.
Hivyo basi ukiwa unamuingilia
mkeo na ukitoa manii basi moja
kwa moja virus wako watakwenda
kuingia katika vijitundu vilivyo
kwenye virginal wall ili kuishi
humo. Ina maana virus
watakaoingia kuishi kwa mkeo ni
wale ambao wamezoeana. Sasa
ikija kutokea mkeo akazini na
mwanaume mwingine ataingiziwa
virus wasiokuwa wako. Hivyo
hawa wapya wakiingia nao pia
watataka kuingia katika yale
matundu ili nao wakaishi. Kwa
kuwa ndivyo alivyowapangia
Mwenyezi Mungu, hawa wapya
wakiingia tu wale wa zamani
ambao ni wa mume,
watawashangaa, watajiuliza hawa
nao wametokea wapi? Mbona si
katika wale tuliozoeana? Kwa
kushangaa huku wale virus
wenyeji watawashambulia virus
wageni kama antibody bacteria
(kitu kinachotoka nje ya mwili). Na
katika mapigano haya watapelekea
kundi moja kufa na kundi moja
likifa lazima wale waliokufa
watoke, watatoka vipi? Au
watatokea wapi? Jibu ni pale pale
walipoingilia. Hapo sasa ndipo mtu
anapoanza kutokwa uchafu. Na pia
virus wapya waliosalimika
wakiona wanazidi kushambuliwa
na virus wa zamani itabidi
watoboe sehemu nyingine
zisizohusika ili wakimbie na
kujificha katika nyama laini.
Hapo ndipo mtu anapoanza kupata
maumivu makali wakati wa
kukojoa na pia ndio chanzo cha
magonjwa mbalimbali ya zinaa, na
wakati huo mume akimuingilia
mkewe naye pia atapata ugonjwa
wa zinaa sababu atakutana na
virus wageni waliojificha kujihami
katika sehemu laini zisizohusika
watamuingia mume kupitia mrija
wa urinary truck (mrija wa mkojo).
Ndio sababu Mwenyezi Mungu
akasema zinaa ni uchafu. Na
uchafu unaokusudiwa ni
kuchanganya mifumo tofauti ya
mwili yaani mwanamke kuingiliwa
na mwanaume zaidi ya mumewe
pekee. Na hapa ndipo tunapoona
hekima ya Mwenyezi Mungu
kwamba kwa nini ameamrisha
mwanamke kuolewa na
mwanaume mmoja na mwanaume
kuoa mwanamke zaidi ya mmoja.
Hii ni kwa sababu mwanamke
anapokea manii yenye kubeba
VIRUS wa asili kutoka kwa
mumewe. Hapa ndipo
inapopatikana hekima ya ya
mwanamke aliyefiwa na mumewe
au aleyeachwa kwa talaka lazima
akae eda. Eda si tu kuangalia kama
mwanamke ana mimba, bali pia
katika kipindi cha miezi mine na
siku kumi ambacho mwanamke
anakaa eda kwa kuwa katika
kipindi hicho haingiliwi ina maana
wale virus watakosa protein
inayopatikana katika manii
ambayo ndio chakula chao, hivyo
kwa kukosa chakula watakufa.
Kwa hiyo katika kipindi hicho
mwanamke anaandaliwa ili kama
ataolewa tena na mume mwingine
huyu mume mpya ajitengenezee
mifumo yake mipya ambayo
haitapingana na ile ya mwanzo.
Hivyo Mwenyezi Mungu alipokataza
ZINAA anajua kwa kina madhara
yake.
Ndio sababu twasema kwamba
sera bora za kupambana na
magonjwa mbalimbali ya zinaa
kama UKIMWI n.k dunia nzima ni
kufuata UISLAM tu hakuna la zaidi.
Hivyo tunapenda watu walifahamu
hilo na kulifanyia kazi kwa kuwa
UISLAM siyo ugaidi wala si dini ya
vurugu bali ni dini ya AMANI
ambayo inaweza kumfaa mtu
kimwili na kiroho. Tunatoa wito
kwa watu ulimwenguni kote
kumuamini Mwenyezi Mungu wa
kweli na Mtume wake wa karne ya
sayansi na technologia Nabii
Muhammad (Amani ya Allah iwe juu yake Yeye ahli zake na Maswahaba zake) ili kupata nusra
ya mitihani mizito na majanga
yanayotukumba wanadamu hivi
sasa.
 
uzi umekaa kidini huu, peleka jukwaa la imani
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Aiseee naona hawa madokta wamenifundisha madesaa walahi
Ati acid kazi ake nn ktk tendo la jimai?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…