Viwango vya matumizi ya pombe huhusiana na ongezeko la hatari ya kuendelea ulevi (addiction), ugonjwa wa moyo, kutofyonza vyakula, ugonjwa sugu wa kongosho , ugonjwa wa ini kutokana na pombe, na kansa. Uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni unaweza kusababishwa matumizi kila mara ya pombe. Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa muda mrefu yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili.Ubongo unaokua wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe. Shituka acha kunywa pombe tu
Kwa mujibu wa utafiti ninaoufahamu mimi, pombe husababisha kifo na takribai watu milioni mbili hufa kila mwaka kutokana na matumizi ya pombe...
Kwa hapa kwetu Tanzania utafiti uliofanyika nchini kati ya Februari na Oktoba 2012 kuhusu viashiri vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ulibaini kuwa asilimia 26.8 hadi 31.9 ya wananchi wanatumia pombe na kati ya hao asilimia 27.4 ya wanaume ni walevi wa kupindukia na wanawake ni asilimia 13.4.