Madhumuni na Dhumuni.

Madhumuni na Dhumuni.

MRIMI MWESO

Member
Joined
May 5, 2012
Posts
5
Reaction score
1
Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitumia neno dhumuni badala ya neno madhumuni. Je, ni sahihi?
 
kiswahili fasaha ni "madhumuni" na siyo dhumuni hayo ni makosa ya mazoea tu
 
kiswahili fasaha ni "madhumuni" na siyo dhumuni hayo ni makosa ya mazoea tu

Ndugu Mrimi Mweso, alichokisema rununu ni kweli; tena kweli tupu! Mazoea ya kutumia dhumuni kumaanisha umoja wa madhumuni unatokana na jinsi inavyojulikana kwamba nomino zote za Kiswahili zimegawanywa katika ngeli zake. Katika ngeli ya O - MA ndimo tunapata nomino zenye tabia hii. Mfano wa nomino hizi ni kama tunda-matunda, tusi-matusi, neno-maneno, embe-maembe, ****-******, jambazi-majambazi n.k. n.k. Kwa hiyo watumiaji wa lugha wanajikuta 'kutekwa' na kanuni hiyo na wanaingiza maneno kama dhumuni-madhumuni, kamasi-makamasi, elezo-maelezo n.k n.k. Nachojaribu kueleza hapa ni kwamba si kila nomino huwa na umoja na wingi. Hivyo kusema dhumuni, msemaji anakuwa amekiuka kanuni za kisarufi.

Ninawasilisha!
 
Sijui kwa nini pamoja na kujua kanuni hii ulimi unakuwa mzito. Mimi siyo mtaalamu wa kiswahili ni mtumiaji tu- juzi juzi nikiwa nawasilisha mada fulani mahali nikataka kusema kwa kiswahili - Please think of targets for each objective. Pamoja na kujua kanuni hii nilishindwa ulimi ulikuwa mzito.... niltakiwa nisemje ili wanielewe vizuri kama nilivyoiweka kwa kidhungu?

naomba mnikwamue hapo
 
Wewe ulikuwa unaongea na waandaaji wa bajeti nini, maana ni kama vile ulikuwa unaanza na 'national objectives' ndipo unashuka kwenye 'target type' kwa kila objective? Anyway ulikuwa unazungumzia malengo yenye uzito tofauti.
 
Back
Top Bottom