Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. BAHATI NDINGO AIWEZESHA VIFAA VYA TEHAMA NA SARUJI MADIBIRA SEKONDARI
Mbunge wa Viti Maalum CCM (UWT) Mkoa wa Mbeya Mhe. Bahati Keneth Ndingo na Mwazilishi wa Bahati Ndingo Foundation & Jamii na Maadili Kampeni mnamo tarehe 22 Aprili, 2023 alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Madibira.
Pamoja na changamoto nyingi walizomueleza mgeni rasmi, Mhe. Ndingo aliweza kuwaunga mkono kwa kuwapatia vifaa kadhaa vya TEHAMA (Photocopy Machine - heavy duty) kwa ajili ya kusaidia kazi mbalimbali Madibira Sekondari
Mhe. Bahati Ndingo aliwapatia wanafunzi wa Madibira Sekondari Ng’ombe mmoja ili vijana wapate kitoweo wakati wanafanya mitihani yao wa mwisho.
Lakini pia alifanikiwa kuchangia mifuko 40 ya saruji (cement) ili kuwaunga mkono Wananchi na Serikali kuwezesha ujenzi wa jiko katika Kituo cha Afya Madibira wilayani Mbarali.
#KaziInaendelea
#MaadiliMemaKwaUstawiWaTaifaLetu
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-04-26 at 18.19.05.jpeg30.2 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-04-26 at 18.19.05(1).jpeg31.7 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-04-26 at 18.19.03.jpeg21 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2023-04-26 at 18.19.03(1).jpeg43.3 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2023-04-26 at 18.19.04.jpeg38.4 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2023-04-26 at 18.19.04(1).jpeg24.7 KB · Views: 5