MADINI: Dotto Biteko uso kwa uso na Mzee Kinana, atamani thamani ya dhahabu ionekane Geita

Vugu-Vugu

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2017
Posts
1,381
Reaction score
1,600
IMG-20220904-WA0158.jpg

KINANA "GEITA IENDANE NA THAMANI YA DHAHABU YA MKOA HUO"

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali mstaafu Abdulrhaman kinana amemshauri mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigella kuangalia namna nzuri ya kuupanga mji wa Geita uwe na Muonekano mzuri na wa kisasa na si ulivyo kwa Sasa.

Kinana amebainisha hayo leo September 4,2022 Mjini Geita wakati wa ziara yake ya Siku moja inayolenga kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuangalia Uhai wa Chama hicho.

Kinana amesema Geita ni mkoa mpya ambao una maeneo mengi, hivyo ni muhimu kwa viongozi kuanzia ngazi ya maafisa mipango kuangalia namna nzuri na bora ya kuupangilia ili uwe miongoni mwa miji mizuri na inayovutia hapa nchini.

"Geita inayo Miradi Mingi ya Ki-maendeleo ambayo inatekelezwa ikiwemo Ofisi za Serikali na Idara zake, Makazi ya Watumishi wa Umma pamoja na Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo hivyo ni muhimu kwa Mamlaka za mkoa huo kuweka mikakati ya kuhakikisha Suala la Mipango miji linazingatiwa ili kuupa hadhi na muonekano mzuri" amesema Kinana.

Akiwa Geita Komredi Kinana amekagua Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo ambao unagharimu Bilioni 20.1, Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita ambapo Ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 7.75 pamoja na Uwanja wa Mpira wa Miguu unaomilikiwa na Halmashauri ya mji wa Geita.
 
Sukuma Gaung mlisema Rais Samia hawapendi, Fanyeni kazi kwa bidii Rais hana ukanda wala ukabila
 
Habari ya sukuma gang imetokea wapi tena kwenye issue ya mipango miji? Sielewi ni kwa nini watu wazima mnapenda sana kushadadia ukabila pasipo sababu.
Issue ya msingi ni kwamba miji yetu mingi haikupangwa vizuri toka mwanzo, haijalishi uko usukumani, umakondeni, ufipani, uchagani, au wapi! Designers wetu wanapaswa kufanya kazi bora zaidi ya wanavyofanya sasa.
 
View attachment 2345765

Naona Mzee anavaa Kijamaa hivi
 
Biteko kafanya kazi kubwa sana tangu alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya bunge iliyochunguza ishu za biashara ya Madini ya Tanzanite. Tangu amekuwa naibu Waziri Hadi Leo tumeshuhudia CSR za kueleweka zikitolewa na makampuni makubwa kama GGM. Kwa ambao hawajafika kwenye miji ya Geita, Katoro ndani ya miaka mitano iliyopita basi waende Sasa halafu wataona nini Biteko anafanya ktk tasnia ya Madini. Ikumbukwe stadi iliyofanywa na UNESCO juu ya uwiano wa ukuaji wa miji iliyo karibu na migodini hasa ya wachimbaji wadogo kumekuwa na uhusishwaji wa Moja Kwa Moja na uwepo wa shughuli za uchimbaji wa Madini. Mfano miaka ya 1890 mji wa Johannesburg ilikuwa ni camp ya wachimbaji wadogo wa dhahabu na platinum. Leo ni Jiji Bora kabisa Africa.
Biteko alikuja kufuta utaratibu wa wawekezaji kujenga vyoo na vituo vya polisi halafu wakajidai sana wanaleta MAENDELEO ya jamii zinazozunguka migodi.

Hoja ninayoiona hapa ni Kwa halmashauri husika Kuweka mipango Bora ya matumizi ya ardhi ikiwepo upanuaji na upangaji wa miji mipya yenye miundombinu ya kisasa. Geita ya miaka kumi iliyopita sio ya Leo.
 
Asante Dotto Biteko
 
Ukweli ni kwamba, kati ya miji yenye mipangilio ya hovyo kabisa, ni Geita na Kahama.
 
Habari ya sukuma gang imetokea wapi tena kwenye issue ya mipango miji? Sielewi ni kwa nini watu wazima mnapenda sana kushadadia ukabila pasipo sababu.
Issue ya msingi ni kwamba miji yetu mingi haikupangwa vizuri toka mwanzo, haijalishi uko usukumani, umakondeni, ufipani, uchagani, au wapi! Designers wetu wanapaswa kufanya kazi bora zaidi ya wanavyofanya sasa.
Tanzania kiuhalisia haina wataalam wa mipango miji. Kazi ya kupanga miji, hata tungekuwa na wataalam walioishia darasa la 4 lakini wenye akili nzuri na upeo, lazima wangrfanya vizuri zaidi kuliko hawa wataalam wa mipango miji majina.
 
Biteko kafanya kazi kubwa sana tangu alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya bunge iliyochunguza ishu za biashara ya Madini ya Tanzanite. Tangu amekuwa naibu Waziri Hadi Leo tumeshuhudia CSR za kueleweka zikitolewa na makampuni makubwa kama GGM. Kwa ambao hawajafika kwenye miji ya Geita, Katoro ndani ya miaka mitano iliyopita basi waende Sasa halafu wataona nini Biteko anafanya ktk tasnia ya Madini. Ikumbukwe stadi iliyofanywa na UNESCO juu ya uwiano wa ukuaji wa miji iliyo karibu na migodini hasa ya wachimbaji wadogo kumekuwa na uhusishwaji wa Moja Kwa Moja na uwepo wa shughuli za uchimbaji wa Madini. Mfano miaka ya 1890 mji wa Johannesburg ilikuwa ni camp ya wachimbaji wadogo wa dhahabu na platinum. Leo ni Jiji Bora kabisa Africa.
Biteko alikuja kufuta utaratibu wa wawekezaji kujenga vyoo na vituo vya polisi halafu wakajidai sana wanaleta MAENDELEO ya jamii zinazozunguka migodi.

Hoja ninayoiona hapa ni Kwa halmashauri husika Kuweka mipango Bora ya matumizi ya ardhi ikiwepo upanuaji na upangaji wa miji mipya yenye miundombinu ya kisasa. Geita ya miaka kumi iliyopita sio ya Leo.
Lakini ukweli hauwezi kubadilika kuwa mji wa Geita, licha ya kubadilika, mpangilio wake ni hovyo kabisa. Hakuna mwezi unapita, bila kupita Geita, naifahamu vizuri sana Geita.

Mji upo live sana, ikithibitisha kuwa unakua kwa haraka kiuchumi. Lakini ukuaji huo umekuwa hauna mpangilio, na kuufanya kuonekana ni mji mchafu kutokana na vibanda na shughuli mbalimbali kutokuwa na mpangilio wowote.
 
Ni kweli ndio maana mji unaweza kupangwa vizuri zaidi katika maeneo mapya
 
Ofisi ya mkuu wa mkoa - Bilioni Saba!!

Hapo kuna makosa ya kiuandishi ama!!?
 
Back
Top Bottom