Madini ujenzi yanalipa

Madini ujenzi yanalipa

Full 8

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
313
Reaction score
271
Nchini kwetu Tanzania tumekua na bahati ya kuwa na madini mbalimbali kama dhahabu, almasi na Tanzanite.

Madini mengine ambayo hayapewi kipaumbele ni madini ujenzi ambayo hutumika sana katika viwanda vya saruji, malu malu na viwanda vya kemikali na madini kama ulanga mweusi ambao nimesikia kampuni ya sumsung hutumia katika kutengeneza screen za smartphone zao.

Kitaaluma mimi ni mjioloji(Mtaalam wa miamba).
nimekua na wazo la kutumia fursa ya madini ujenzi kwa malengo ya;

1. Kuongeza kipato changu binafsi

2. Kutoa ajira kwa vijana wengi wanaomaliza katika vyuo vyetu ambao wanakumbana na tatizo la ajira, hasa katika industry ya mining.

3. Kutimiza dhana ya " HAPA KAZI TU" kutumia effectively muda wangu wa ziada kwa manufaa ya baadae.

- Hadi sasa niko katika hatua ya kuchukua leseni za maeneo yenye madini ujenzi hasa granites na carbonate hard rocks ambazo hutumika sana katika kuzalisha kokoto/aggregate na tiles.

Mahitaji.
1. Ningependa kupata ushauri kwa watu ambao wameshajihusisha na industry hii.
2. Partinaship na links kwa watu au kampuni zinazofanya kazi katika sekta hii ili niweze fanya nao kazi. kwani suala la machinery(crushers, trucks ) ni changamoto kutokana na kuwa na gharama kubwa kuvipata.

Nawasilisha.
 
keep ahead mkuu ila nami naipenda hii bussiness mbelen lakini hasa kutengeneza tiles roofing materials ipo siku TUSUBIRI WAHUSIKA WAKUSAIDIE
 
wadau nangojea msaada wenu
 
kuna wahindi na wachina wanaojihusisha na industrial minerals, mwenye contact nao plz
 
Back
Top Bottom