Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Ameyasema hayo leo tarehe 11 Septemba, 2024 Jijini Dar es Salaam alipokutana na alipozungumza na vyombo vya habari kuuhabarisha umma wa Watanzania juu ya tukio hilo.
"Nchi yetu inazo sekta kadhaa za uzalishaji ambazo mapato yake ndiyo msingi wa maendeleo ya uchumi wetu ikiwemo sekta ya madini. Sasa basi, tunapokuwa na watu wachache ambao wanajihusisha na shughuli hizi za utoroshaji wa madini na hivyo kuikosesha Serikali mapato hatuwezi kuwavumilia."
"Kilo hizo 15.78 kwa bei ya leo zina thamani ya takribani bilioni 3.4, fedha ambazo kwa sasa zote watoroshaji hawa wanakwenda kuzipoteza. Serikali tunakwenda kufuta leseni zao wakitiwa hatiani na mahakama na kuwaweka kwenye orodha ambayo hawataruhusiwa kumiliki Leseni ya kufanya biashara yeyote katika mnyororo wa thamani wa madini nchini Tanzania," alibainisha Mavunde.
Kwa mujibu wa mahojiano ya awali wakati uchunguzi unaendelea, watuhumiwa wamesema madini hayo ya dhahabu walikuwa wanasafirisha kutoka Bandari ya Boti Dar kwenda Zanzibar
"Uchunguzi na mahojiano na watuhumiwa yanaendelea, na pindi kazi hii ikikamilika tutawapandisha mahakamani kujibu mashtaka," alisema Mavunde.
Soma Pia: Mbeya: Mbaroni wakitorosha Madini yenye Thamani ya Shilingi 1.5 Bln. Waziri Mavunde aagiza kufutwa kwa leseni zao ndani ya nchi
Wakati huo huo Mavunde ameipongeza kazi inayofanywa na Kikosi kazi cha kuzuia utoroshaji wa madini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na kutoa rai kwa wafanyabiashara nchini kuacha tabia ya utoroshaji kwani inarudisha nyuma juhudi za serikali