Madini ya Dhahabu ya shilingi bilioni 3.4 yakamatwa Bandarini yakitoroshwa

Madini ya Dhahabu ya shilingi bilioni 3.4 yakamatwa Bandarini yakitoroshwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ametangaza kukamatwa kwa madini ya dhahabu kilo 15.78 bandarini yalipokuwa yakitoroshwa.

Ameyasema hayo leo tarehe 11 Septemba, 2024 Jijini Dar es Salaam alipokutana na alipozungumza na vyombo vya habari kuuhabarisha umma wa Watanzania juu ya tukio hilo.
WhatsApp Image 2024-09-11 at 17.21.43.jpeg
"Nchi yetu inazo sekta kadhaa za uzalishaji ambazo mapato yake ndiyo msingi wa maendeleo ya uchumi wetu ikiwemo sekta ya madini. Sasa basi, tunapokuwa na watu wachache ambao wanajihusisha na shughuli hizi za utoroshaji wa madini na hivyo kuikosesha Serikali mapato hatuwezi kuwavumilia"

"Kilo hizo 15.78 kwa bei ya leo zina thamani ya takribani bilioni 3.4 fedha ambazo kwa sasa zote watoroshaji hawa wanakwenda kuzipoteza. Serikali tunakwenda kufuta leseni zao wakitiwa hatiani na mahakama na kuwaweka kwenye orodha ambayo hawataruhusiwa kumiliki Leseni ya kufanya biashara yeyote katika mnyororo wa thamani wa madini Nchini Tanzania", alibainisha Mhe. Mavunde.
WhatsApp Image 2024-09-11 at 17.21.45.jpeg
Kwa kwa mujibu wa mahojiano ya awali wakati uchunguzi unaendelea, watuhumiwa wamesema madini hayo ya dhahabu walikuwa wanasafirisha kutoka bandari ya Dar es Salaam kuelekea Visiwani Zanzibar.

Uchunguzi na Mahojiano na watuhumiwa yanaendelea,na pindi kazi hii ikikamilika tutawapandisha mahakamani kujibu mashtaka”Alisema Mavunde.
WhatsApp Image 2024-09-11 at 17.21.48.jpeg
Akihitimisha taarifa yake, Waziri Mavunde alipongeza kazi inayofanywa na Kikosi kazi cha kuzuia utoroshaji wa madini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na kutoa rai kwa wafanyabiashara nchini kuacha tabia ya utoroshaji kwani inarudisha nyuma juhudi za Serikali kukuza uchumi wa Nchi yetu.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-09-11 at 17.21.44.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-11 at 17.21.44.jpeg
    38.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-11 at 17.21.48(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-11 at 17.21.48(1).jpeg
    53.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-09-11 at 17.21.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-11 at 17.21.49.jpeg
    52.1 KB · Views: 4
Mkakamata sana maana mlivuruga mifumo ya Magufuli , sasa mtapata kazi ya zaidi.. Huku Lyimo akipambana na watu wa madawa nyie mtapambana na hamtoweza kuwakamata wote .

Ni bora usafirishaji wa madini ufanyie clearing na wakala wa serikali .
 
Kuna vituko tz hizo hela si ndogo sana kuna watu wanazipiga hizo b wilayani huko na hawafanywi chochote wanaishia kuhamishwa.Ww fatilia safari za waziri mkuu kila anapoenda analia tu watu wametafuna hela b kadhaaa.
 
Mpaka mazeri amalize muda wake asilimia kubwa ya madini ya Tanganyika yatakuwa yametoroshewa Zanzibar!!

Kuna haja ya kuwa na rais wa Jamhuri anayetokea Tanganyika angalau kidogo atakuwa na uchungu na rasilimali za nchi.
 
Yupo sahihi wafutiwe tu
Ila ilikuwa aanike majina kama wizi wengine
Hakuna kufichana
 
Hao ni wafutiwe leseni zote za biashara na kufukuzwa kabisa kutoka nchini kwa uhujumu wa uchumi
=======
Cha kusikitisha unakuja kusikia baadae ni wale wale wawekezaji uchwara. Washacheza

Tusubiri kushitakiwa kwa kukamata madini yetu wenyewe, na kwa kuwanyima leseni kwa sheria zetu wenyewe. Tafran tupu.
 
Back
Top Bottom