Madini ya Lulu: Watu wengi hawajui thamani yake, haibadiliki

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Iwapo chaza wangekuwa wanakuzwa na kuvunwa lulu kama ilivyo katika nchi nyingine ni wazi mapambo ya plastiki kutoka China yasingekuwa na nafasi na wananchi wangetengeneza ajira na mapato ya serikali yangeongezeka.


Kito hicho ni tofauti na madini ya almasi, dhahabu, Tanzanite, Ruby na madini mengine ambayo yanachimbwa, lakini Lulu inatokana na wanyama jambo ambalo watu wengi hawalifahamu.


Lulu imekuwa kito cha kufikirika nchini kwani watu wachache wanaitambua na Serikali haina mipango ya kufanya chaza kwa ajili ya biashara.

Inaitwa Lulu kwa lugha ya Kiswahili. Kwa lugha ya Kiingereza ni Pearl. Hicho ni kito cha thamani ambacho mara nyingi kinakatwa, kusuguliwa na kungarishwa kwa namna mbalimbali na kutumiwa pamoja na madini mengine kama dhahabu au fedha na kutengenezwa mapambo kama pete, hereni, mikufu au vikuku.

Lulu inatajwa siku nyingi kuanzia katika misahafu ambavyo ni vitabu vitakatifu kwa waumini wa dini ya Kiislamu hadi katika Bibilia na hadithi nyingine za kale. Nchini kuna utajiri mkubwa wa Lulu, lakini hakuna jitihada zozote za kuvuna kito hicho cha thamani ambacho moja ya sifa yake kuu ni kutobadilika rangi yake kwa namna yoyote katika kipindi chote cha kudumu kwake labda iharibiwe kwa tindikali.

Lulu ni nini?

Kito hicho ni tofauti na madini ya almasi, dhahabu, Tanzanite, Ruby na madini mengine ambayo yanachimbwa, lakini Lulu inatokana na wanyama jambo ambalo watu wengi hawalifahamu.

Kwa jicho la pili ni eneo lingine ambalo vijana wanaweza kujiajiri kwa wingi, lakini endapo Serikali itakuwa nyuma ya vijana.

Kulingana na takwimu mbalimbali, Lulu hupatikana katika viumbe hai aina ya chaza ambao wanafanana na konokono wadogo na mara nyingi wanyama hao hupatikana chini ya bahari na kwa kawaida wanaliwa.

Tafiti mbalimbali zinabainisha kwamba watu wengi huwakusanya chaza hao na kuwachemsha kabla ya kubomoa gamba lao na kuitoa nyama ambayo inaliwa zaidi na watu wa makabila ya mwambao wa Pwani na kuna ambao wanahusisha na masuala ya tiba.

Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Shaaban Kikoti anasema chaza wanavuliwa sana Ufukwe wa Kigamboni na wanachemshwa wakiwa katika makopo au magaloni mbele ya jengo la Ikulu na kinamama ambao baadaye huuza.

Anasema ingawa hakuna takwimu sahihi, lakini nyama hiyo inahusishwa na kuongeza virutubisho mwilini na kuchochea ongezeko la homoni ambazo zinaongeza nguvu za kiume kwa wanaume na upande mwingine gamba la mnyama huyo hutumika kama mapambo majumbani na kwingineko.

Mhadhiri Mwandamizi wa Kemia ya Mazingira Bahari katika Chuo Kikuu Dar es Salaam, Idara ya Sayansi Bahari, Aviti Mmochi anasema Lulu ni moja kati ya mazao ya bahari ambayo kama yangetumika vizuri yangewanufaisha wakazi wa Pwani na Taifa kwa ujumla kuliko sasa.


Mtalaamu na mtafiti huyo anasema kwa kawaida chaza ana magamba na chakula chake hukipata baada ya kuyachuja maji ambayo kwa kawaida anayavuta baada ya kufungua na kufunga magamba yake na wakati wa tendo hilo kuna mabaki ambayo ni chakula kwake hubakia.

Wakati mwingine mchanga unabaki ndani ya jumba lake na kumkera na kuutengeza aina fulani ya ute na kukifungia kitu hicho ili kisiendelee kuzunguka ndani ya mwili wake na bahati mbaya au nzuri anasema malighafi hiyo huwa inangaa sana.

Mmochi anasema nchini wanyama hao wanaharibiwa kwa kuliwa na baadhi ya watu mapema kabla hawajapevuka vya kutosha na mbaya zaidi hakuna ufugaji wa chaza uliolenga uzalishaji wa lulu tofauti na inavyofanyika katika nchi nyingine.

Iwapo chaza wangekuwa wanakuzwa na kuvunwa lulu kama ilivyo katika nchi nyingine ni wazi mapambo ya plastiki kutoka China yasingekuwa na nafasi na wananchi wangetengeneza ajira na mapato ya Serikali yangeongezeka, anasema mhadhiri huyo.

Serikali haina mpango

Hivi sasa Lulu imekuwa kito cha kufikirika nchini kwa kuwa ni watu wachache ambao wanaitambua na Serikali na taasisi zake hazina mipango ya kufanya ufugaji wa chaza kwa ajili ya biashara.

Mmochi anasema Lulu inapatikana kwa kuwafuga chaza katika maeneo maalumu ambayo yanakuwa yamepangwa na kabla ya kufanya uzalishaji wa lulu ni lazima uchonge kitu kulingana na mahitaji yako.

Mtu unaweza ukakata kipande cha chupa, plastiki kwa umbo la moyo, chozi au msalaba kisha unakipaka gundi Super Glue, anabainisha.

Anasema mfugaji wa chaza atamwangalia jinsi rangi zake zilivyojipanga na kusogeza nyama zake kidogo na ukipachika kitu hicho katika rangi anazozipenda mnyama huyo anarudishwa katika maji kuendelea na maisha yake na kitu hicho kinamkera hivyo anazalisha ute mwingi zaidi kukikabili.

Ute huo hubadilika na kuwa mgumu mithili ya mfupa katika umbo tarajiwa, anasema. Anaeleza kwamba hatua hiyo hupitia katika kipindi cha miezi tisa hadi mwaka mmoja kabla ya chaza kutolewa nje ya maji.

Anasema akitolewa unavuna lulu kwa kutoa nyama yake na jumba lake kusafishwa na kulisugua ili kupata lulu safi ambayo inakuwa imejitengeneza kulingana na ulivyotaka na anabainisha kwamba chaza huyo unaweza kumtoa walau mara moja kila mwezi na kuangalia jinsi anavyoendelea.

Mmochi anasema baada ya kuisugua lulu unakata kipande kulingana na mahitaji yako na kipande cha vipande vinavyobaki vinatengenezwa heleni au kitu kingine cha namna hiyo.

Bei ya lulu ni kati ya Sh30,000 hadi Sh50,000 na ubora wake hubaki kama ulivyo bila kuathiriwa na kitu kingine.Mmochi anasema wengi hawaelewi, lakini Lulu ina mwonekano na mvuto usio wa kawaida tofauti na madini mengine.
 
Natumai waziri wa uvuvi amelala kama kawaida ya watendaji wa tanzania!Ni suala la kuwaelimisha wananchi uvunaji wake na soko lake
 
Natumai waziri wa uvuvi amelala kama kawaida ya watendaji wa tanzania!Ni suala la kuwaelimisha wananchi uvunaji wake na soko lake

Hilo ndiyo hasa Tatizo letu Watanzania, Bongo zimelala tunasubiri serikali, ONA FURSA IFANYIE KAZI KIMYAKIMYA USIAMSHE MTU, WATU WATAAMKA WAKIONA UNAPIGA PESA.
 
Hizi ndizo zinazoitwa fursa ambazo wenye uwezo wanatakiwa wazikamatie.
Hii habari ya serikali haijafanya,serikali ifanye-Ni dalili za kufilisika kifikra.
 
Mzuqa

Tangu udogoni nasikia lulu madini yenye thamani kuliko yote. Ila hayaonekani hata picha na wala yanapochimbwa na kupatikana ukilinganisha na dhahab almas Tanzanite etc.

Kuna story za vijiweni uswahilini Wadau wanapokunywa kahawa utawasikia wanasema lulu inapatikana ndani mdomoni mwa Samaki chini kabisa baharini.

Mwanajamvi yeyote anayeyafaham haya madini ya lulu atueleeze yakoje yana rangi gani yanapatikana wapi.

Hadi kanisani tulishafundishwaga mbinguni kuna milango pavement na barabara za dhahab na lulu.


Je lulu kweli inaegzisti ama ni porojo za kusadikika. Nimegoogle kichizi holaaa.

Wadau tiririkeni
 
Lulu si madini ya kuchimbwa bali hupatikana ndani ya kombe za chaza ( oyster shells), aina ya samaki na wazamiaji huzama hadi kwenye sakafu ya bahari kuwakusanya chaza hao wenye lulu ndani ya kombe(ganda) zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikuelezea kutokana na uzoefu wangu!
Nilishawahi kufanya shuguli za baharini
Pearl ipo Nliona lulu ina rangi ya silver
Yenye uweupe....mbona lulu inapatikana ndani ya aina ya kiumbe cha bahari Inaitwa oyster Jamii fulani ya konokono Sema ni nadra sana kuipata

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kwa kiingereza lulu inaitwaje
 
Lulu ( pearl) are bio gemstone that are white and brown- grey in color. Wanategenezwa na wadudu wa baharini walioko kwenye jamii ya bivalve mollusc. siyo wote wadudu wa jamii wanawazalisha Bali kunamazingia yasiyoyakawaida hutokea ili wazalishe yaani kwa kimombo abnormalities hutokea katika mwili wa wadudu hao ndiyo wanawazalisha.

Hata hivyo kisayansi huko Japan na baadhi ya mataifa ya Asia yanafanya ufugaji wa bivalve hao na kuwawekea chemical mwiliwao ili waweze kudhalisha Pearl ( lulu). Unaweza Google Pearl aquaculture utaona watu wanavyovuna. Hizo story za joka ni za kwenye kahawa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kwa kiingereza lulu inaitwaje
Pearl....Inaitwa
Baharini kuna vitu vingi vya thamani
Kuna kitu kinaitwa "ambari"nayo inasemekana inatokana ndani ya samaki
Huwa anaitema na Hupatikani nchi kavu
Kg1 huuzwa $ zaidi ya 15000 iko kama kinyesi cha ngombe au nyasi zilizoshikamana
Nayo niliigumiaa
Mtu mwingine anaweza fikiri hadithi

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…