SoC03 Madini ya thamani yaliyofichwa duniani

SoC03 Madini ya thamani yaliyofichwa duniani

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Jun 25, 2023
Posts
45
Reaction score
32
Katika miaka ya hivi karibuni, kumeibuka mijadala kuhusu viumbe vya ajabu visemekavyo ni vyenye akili nyingi kuliko wanadamu ambavyo vinasaidia watu wa mataifa makubwa kufanya mambo makubwa wanayoyafanya.

Swali ni je! NENO LA MUNGU LINASEMAJE?

"MUNGU Akasema, Na Tumfanye mtu kwa MFANO WETU, kwa SURA YETU; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. MUNGU Akaumba mtu kwa MFANO WAKE, kwa MFANO wa MUNGU Alimwumba, mwanamume na mwanamke Aliwaumba. MUNGU Akawabarikia, MUNGU Akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi." (Mwanzo 1:26-28)

Kumbe! Hakuna kiumbe chochote duniani chenye uwezo mkubwa wa akili kuliko mwanadamu; HAKIPO NA HAKITAKUJA KUTOKEA, kwani uwezo wa KUTAWALA viumbe vyote vyenye uhai viendavyo juu ya nchi MUNGU Ametupa sisi wanadamu.

Swali ni je! Ili mwanadamu aweze kuwa na NGUVU YA KUUTAWALA ULIMWENGU, anapaswa kuwa na nini?

NENO LA MUNGU LINASEMA: "Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, Amefanana na wanyama wapoteao." (Zaburi 49:20)

Tafsiri yake ni kuwa; mtaji pekee wa mwanadamu KUUTAWALA ULIMWENGU na viumbe vyote vyenye uhai ili asifanane na wanyama wala si madini ya dhahabu yaliyopo kule Geita, si madini ya Tanzanite yaliyopo kule Mirerani, si madini ya Almasi yanayopatikana kwa wingi kule Botswana wala si madini yoyote mengine na fedha ya rangi yoyote wala ya Taifa lolote zaidi ya MADINI YAITWAYO AKILI YA ROHONI.

Kama ingekuwa madini ya almasi, dhahabu, tanzanite, mafuta, na kadhalika ndiyo yanayotoa uwezo wa mwanadamu au Taifa kuutawala ulimwengu basi mpaka sasa mataifa yenye nguvu duniani yangekuwa ni kutoka Afrika au Mashariki ya Kati kwani ndipo mahali ambapo ardhi yake imejaa wingi wa madini ya kila rangi na kila hali.

Akili ya Rohoni ni nini?

Akili ya Rohoni ni HEKIMA NA MAARIFA YA MUNGU yaliyo ndani ya mwanadamu, kama yale ambayo MUNGU Alimbariki nayo Mfalme Sulemani hata akawa Mfalme mwenye Nguvu kuliko wafalme wote duniani (1 Wafalme 4:30-34); yaani aliweza kuutawala ulimwengu. Hii ni kwa sababu: "HEKIMA ni NGUVU ZAKE mwenye HEKIMA, Zaidi ya wakuu kumi waliomo mjini." (Mhubiri 7:19)

Kwa MTAJI WA AKILI YA ROHONI MUNGU ALIUMBA MBINGU, DUNIA NA VYOTE VILIVYOMO NA ANATAWALA DUNIANI NA MBINGUNI MILELE. (Mithali 3:19-20)

HEKIMA NA MAARIFA YA MUNGU YANAPATIKANAJE??

NENO LA MUNGU LINASEMA: "Ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika UPENDO, wakapate UTAJIRI wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa SIRI YA MUNGU, yaani, KRISTO; Ambaye NDANI YAKE YEYE HAZINA zote za HEKIMA na MAARIFA zimesitirika." (Wakolosai 2:2-3)

Tafsiri yake ni kuwa; hakuna mwanadamu yeyote duniani awezaye kupata NEEMA YA HEKIMA NA MAARIFA YA MUNGU ILI KUPATA
AKILI YA ROHONI AMBAYO NDIYO MTAJI WA KUUTAWALA ULIMWENGU kama hajakubali na KUAMINI kutoka moyoni kuwa BWANA YESU KRISTO NI MWANA WA MUNGU NA NDIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU; ALIYEKUJA DUNIANI KUTUOKOA NA DHAMBI ZETU, ALIKUFA MSALABANI KWA AJILI YETU KISHA AKAFUFUKA NA DAMU YAKE IMWAGIKAYO MSALABANI INAONDOA KABISA DHAMBI HATA IWE NI DHAMBI YA AINA GANI.

Mwanadamu yeyote anapomkataa na kutomwamini BWANA YESU KRISTO anaishia kuwa na hekima na akili za kibinadamu ambazo mwisho wake ni kuwa mtumwa na kutawaliwa na wanadamu na mataifa makubwa ambayo hadharani humpinga BWANA YESU KRISTO ili kuupoteza ulimwengu na kuzuia nafasi ya wanadamu wengine na mataifa mengine KUUTAWALA ULIMWENGU kwa sababu, ili shetani na ufalme wake aweze kuutawala ulimwengu ni lazima kwanza awatumie watu wake na mataifa yake aliyowekeza ufalme wake ili awachonganishe wana wa MUNGU na mataifa ya MUNGU dhidi ya MUNGU kwa kulipindua NENO LA MUNGU ili wana wa MUNGU wasipate nafasi ya KUTAWALA na yeye aendelee kutawala ulimwengu. (Mwanzo 3:1-6)

Unapoona kuna wanadamu na mataifa yanampinga BWANA YESU KRISTO na bado yanafanikiwa kuutawala ulimwengu ujue ni falme ambazo shetani amewekeza nguvu zake na falme hizi ni chache dunia nzima (Ufunuo wa Yohana 17:10-13) hivyo anataka falme hizi chache pekee ndizo ziendelee kuutawala ulimwengu kwa kutumia njia ya kuudanganya ulimwengu umfuate ili uendelee kuwa UTUMWANI lakini hakuna mwanadamu wala Taifa ambalo halipo kwenye orodha ya falme hizi chache ambalo shetani atalipa nguvu zake za soda za kuutawala ulimwengu hata kwa sekunde mbili hata ufuate masharti yake mpaka uingie naye baharini bali ni BWANA YESU KRISTO PEKEE, hivyo kuendelea kumkataa na kumpinga BWANA YESU KRISTO hususan katika BARA LA AFRIKA; AMBAPO NEEMA YA MUNGU IMETUJILIA SASA, ni kuendelea kumkataa TAJIRI YETU WA KAMPUNI YA UTAWALA WA ULIMWENGU na huku AJIRA YA KUUTAWALA ULIMWENGU tunaitaka, lazima bahasha zichakalie mikononi kwa sababu nani atakuajiri iwapo unamtukana, unamkataa na kumkana TAJIRI YAKO MWENYE NAFASI KUBWA ya Kukuajiri huku unampigia makofi na vigelegele tajiri wa adui yako, aliyekuwekea upanga shingoni akufanye mateka kisha akuangamize!? (Waefeso 1:17-23)

Uzuri ni kwamba shetani anamjua vizuri BWANA YESU KRISTO na akishamaliza kuudanganya ulimwengu hurudi MIGUUNI PAKE kutetemeka kwa sababu anajua kuwa BWANA YESU KRISTO NDIYE 'BOSS MKUU' MFALME WA MBINGUNI NA DUNIANI. (Waefeso 1:17-23)

SIFA ZA BWANA YESU KRISTO

DAMU YAKE
NI NJEMA KULIKO DAMU YOYOTE DUNIANI, NA ONDOLEO LAKE LA DHAMBI KWA YEYE AAMINIYE NI LA MILELE kuliko damu za wanyama wala wanadamu (Mathayo Mtakatifu 26:28) (Waebrania 12:24) (Warumi 3:23-26); kwani damu za wanyama na wanadamu haziondoi dhambi. (Waebrania 10:4)

JINA LAKE LINAMKOMESHA na KUMWONDOA shetani, mashetani na kila roho chafu popote zilipo. (Matendo ya Mitume 16:16-18); kisha LINATUPA mahitaji ya mioyo yetu (Yohana Mtakatifu 14:13-14)

NI MPATANISHI NA MWOMBEZI WETU KWA BABA YETU WA MBINGUNI (1 Yohana 2:1-3)

NENO LAKE Ndilo liletalo AKILI YA ROHONI, kwani NENO LA BWANA YESU KRISTO NI ROHO TENA NI UZIMA NA YENYE UWEZO WA KUZIWEKA HURU; Fikra Zetu, Roho Zetu, Miili Yetu, Tanzania, Afrika na Ulimwengu Mzima na hatimaye Wana wa MUNGU tuweze KUUTAWALA ULIMWENGU PAMOJA NA BWANA YESU KRISTO. (Yohana Mtakatifu 6:63) (Yohana Mtakatifu 8:31-32) (2 Wakorintho 3:17) (Ufunuo wa Yohana 20:4)

Mwanadamu au Taifa lolote linalotawala ulimwengu halitawali kwa akili zake, bali 'hupiga chabo' na kulifuata NENO LA BWANA YESU KRISTO kwa siri kubwa kwani wanajua UKWELI kuwa pasipo HUYU MWAMBA hakuna anayeweza 'kutoboa' kwenye ulimwengu huu; lakini wakitoka nje wanampinga KRISTO ili ulimwengu usifahamu kuhusu SIRI HII.

NI NURU, hivyo Anapokosekana mahali giza hutawala mahali hapo (Yohana Mtakatifu 1:1-5) (Yohana Mtakatifu 8:12)

NI RAFIKI MWEMA NA MZURI MWENYE UPENDO kuliko ndugu, jamaa na marafiki wa dunia hii (Yohana Mtakatifu 15:12-15)

NI FUNDI; FUNDI STADI WA KAZI NAMBA MOJA (Mithali 8:30-31) (Marko 6:2-3)

ALIPOKUJA DUNIANI HAKUSOMA ELIMU YA DUNIA HII, LAKINI ALIKUWA NA ELIMU NA HEKIMA ILIYOWASHANGAZA WANADAMU; KWA SABABU ALIKUWA NA ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI (Yohana Mtakatifu 7:15-17) (Luka Mtakatifu 2:46-47) (Mathayo Mtakatifu 13:52)

NDIYE MWUMBAJI NA MBUNIFU NAMBA MOJA (Yohana Mtakatifu 1:1-4)

UMAARUFU WAKE NI MKUBWA; ALIFAHAMIKA, ANAFAHAMIKA NA ATAZIDI KUFAHAMIKA MILELE NA TUNAOMWAMINI NA WASIOMWAMINI.

NI MWANASANAA NAMBA MOJA ALIYESHANGAZA ULIMWENGU NA WANASAYANSI KWA KUVUNJA SHERIA YA KI-SAYANSI IITWAYO The law of floating which states that; "if the density of the body is greater than the density of the fluid, the body sinks." KWA KUTEMBEA JUU YA MAJI HALAFU MWAMBA HAKUZAMA NA HAWAKUMFANYA KITU. (Marko Mtakatifu 6:48-51)

NDIYE MWALIMU NA FUNDI MKWELI NA MWAMINIFU (Yohana Mtakatifu 8:31-32) (Marko Mtakatifu 6:2-3);

NI MWANATEKNOLOJIA NAMBA MOJA KWANI;

  1. NI MTANGAZAJI WA HABARI (Isaya 61:1-2) (Luka Mtakatifu 4:16-19)
  2. NI MWANDISHI MWENYE ELIMU YA UFALME WA MUNGU (Mathayo Mtakatifu 13:52)
  3. NI MWALIMU AMBAYE WANAFUNZI WAKE NA MITUME WAKE NI WAANDISHI WAZURI KWA AJILI YA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO. (Warumi 16:3) (1 Yohana 2:1) (2 Timotheo 4:19-22) (Luka Mtakatifu 1:1-3)
  4. NDIYE MBUNIFU NA MWANZO WA ELIMU, TEKNOLOJIA, UJUZI, HEKIMA NA MAARIFA. (Kutoka 31:1-6) (Kutoka 35:30-35) (Wakolosai 2:2-3) (Mathayo Mtakatifu 13:52)

Kwanza kabisa tunatakiwa tufahamu kuwa AKILI YA ROHONI ndani yetu wanadamu huingia kwa NEEMA YA MUNGU yaani ni ZAWADI ambayo MUNGU Humtunuku mwanadamu yeyote Amtakaye baada ya mwanadamu kuziacha njia zake mbaya, na kuigeukia NJIA, KWELI NA UZIMA Ambaye ni BWANA YESU KRISTO Aliyetuletea NEEMA YA MUNGU NA KWELI duniani. (Zaburi 51:6) (Mithali 1:1-7) (Yohana Mtakatifu 14:6) (Yohana Mtakatifu 1:17)

Pili, wanadamu tunatakiwa KUMWOMBA MUNGU KWA IMANI ATUPE HEKIMA pale tunapohisi tumepungukiwa HEKIMA. (Yakobo 1:5-7)

Tatu, wanadamu tunatakiwa KUSOMA NENO LA MUNGU KWA KUONGOZWA NA ROHO YA MUNGU yaani baada ya kutubu na kumgeukia MUNGU na WALA SI KWA SHERIA yaani kusoma NENO LA MUNGU huku una mambo yasiyompendeza MUNGU moyoni, kwa sababu falsafa za watu za kupoteza na kuuangamiza au kuua wanadamu na ulimwengu zilianzia hapa; na NENO LA MUNGU LINASEMA: "Andiko huua bali ROHO Huhuisha." (2 Wakorintho 3:6)

Nne, ni MAFUNZO YA ELIMU tunayoyapata, yanatakiwa kuwa ni MAFUNZO YA ELIMU YA MUNGU Ambayo yanafundisha kwa HADHI YA JUU SANA kuhusu UBUNIFU, TEKNOLOJIA NA SANAA KWA VITENDO ili kutuwezesha kufanya mambo makubwa na mapya duniani kama ambavyo MUNGU Alifanya katika Mwanzo 1-2, kwani tumeumbwa kwa SURA NA MFANO WAKE.

Kuutawala ulimwengu wanadamu huchukulia lazima uwe Rais wa Taifa fulani pasipo kufahamu kuwa KUUTAWALA ULIMWENGU tafsiri yake ni kuwa wa kwanza duniani kwenye kila eneo la kazi na maisha kwa ujumla; Elimu, Afya, Ndoa, Familia, Biashara, Kazi, Talanta, Taaluma, Teknolojia, Ubunifu, Siasa na kila kilicho chema. (Mwanzo 1:26-28)

Kumsikiliza na Kumtii MUNGU kwa KILA Anachokisema; Akisema YESU KRISTO NI MWANANGU MPENDWA WANGU MSIKILIZENI YEYE.... UKASEMA "SAWA MKUU"

Akisema zama za kutakaswa dhambi kwa damu za wanyama zimekwishapita sasa ni DAMU YA MWANANGU MPENDWA WANGU YESU KRISTO PEKEE Imwagikayo Msalabani inao uwezo wa kukuondolea dhambi hata kama zilijificha uvunguni... UKAJIBU "SAWA MKUU"

Akisema chochote kile tukatii na kutekeleza Alichokisema kutoka moyoni lazima MUNGU Atuheshimishe na Atupe NEEMA YA kufanya zaidi ya KAZI Alizozifanya BWANA YESU KRISTO Alipokuja hapa duniani. (Yohana Mtakatifu 14:12)

Lakini MUNGU Akikwambia YESU KRISTO NI MWANANGU ukakataa uzuri Hakulazimishi bali Anakuacha ili uende na ufanye unachotaka kufanya, MUNGU NI MFALME WA DEMOKRASIA hivyo Halazimishi na Hashikii mwanadamu upanga; Aidha uchague UZIMA au MAUTI, KUTAWALA au KUENDELEA KUWA MTUMWA hiyo ni juu ya mwanadamu wala Halazimishi; japo kwa UPENDO Anataka kila mwanadamu aingize japo kidole kwenye UFALME WA MBINGUNI, aonje WEMA WAKE JINSI ULIVYO. (Kumbukumbu la Torati 30:19-20)

Chaguo ni la mwanadamu; asikilize NENO LA MUNGU au maneno ya wanadamu shauri lake atavuna alichopanda kwa sababu YEYE MUNGU YUKO RAHANI, Mbinguni ni vioo, lulu, dhahabu, bilauri na vito vya thamani; kazi kwetu huku Afrika ambapo barabara za kilomita mbalimbali zimetandikwa mikeka ya vumbi. (Ufunuo wa Yohana 4:1-6) (Ufunuo wa Yohana 21:11-21)

UPANGA WA MUNGU Huinuka kwa wale wanaofanya VITA NAYE. (Ufunuo wa Yohana 19:19-21)

Mwanadamu anapoasi NENO LA MUNGU ameasi ELIMU YA MUNGU hivyo MUNGU Humnyang'anya UFALME WAKE NA MAFUNZO YA ELIMU YAKE na Huiacha Teknolojia juu ya mwanadamu iwe laana badala ya BARAKA ili impige makonzi; kwa vita, magonjwa, umaskini, njaa na kila aina ya unyonge na utumwa.

BWANA YESU KRISTO KUWA NDANI YETU NASI NDANI YAKE NDIYE HUTUPA MADINI YA THAMANI YALIYOFICHWA DUNIANI YAANI AKILI YA ROHONI ili tuwe HURU na tuwe chini ya BWANA YESU KRISTO lakini tuwe JUU ya Teknolojia na Ubunifu ili TEKNOLOJIA IGEUKE KUWA BARAKA KWETU nasi tusiendelee kuwa watumwa; yaani kazi unafanya zaidi ya wanayofanya wao lakini unaishia kwenye mipaka ya taifa lako, kila ukijitahidi utanue mipaka ulimwengu ukutambue unabuma au unaishia mataifa mawili matatu unalala mauti; BWANA ATUEPUSHIE HILI KWA JINA LA YESU KRISTO.

Shetani anawinda ELIMU YA MUNGU NA KUIFICHA ili aendelee kuwa karibu na MUNGU na aendelee kutumia teknolojia na Ubunifu kuupiga ulimwengu matukio, njia pekee anayoitumia ni kujipendekeza kwa MUNGU kisha kulisikia na kulitii NENO LA MUNGU kwa SIRI na kwa SIRI Anatetemeka MBELE ZA BWANA YESU KRISTO Kwani anafahamu ndiye TAJIRI WA UFALME WA MBINGUNI, huku hadharani huwadanganya wanadamu kuwa BWANA YESU KRISTO si lolote si chochote ili wanadamu waliasi NENO LA MUNGU waendelee kufukuzwa NJE YA UFALME YA MUNGU, wawe mbali na MUNGU na kuwa watumwa wake shetani. (Mwanzo 3:24) (Danieli 11:32)

Sasa ni kazi yetu wana wa MUNGU kumwondoa shetani karibu na MUNGU ili tukae karibu na BABA YETU WA MBINGUNI na ELIMU YA MUNGU IKIWEMO TEKNOLOJIA iwe chini yetu kwani huwezi kuutawala ulimwengu kama TEKNOLOJIA, SANAA NA UBUNIFU vipo juu yako, bali ni lazima viwe chini, na ili TEKNOLOJIA iwe chini yetu wanadamu ni lazima baada ya MUNGU tuhakikishe sisi tunakuwepo chini yake kwa KULISIKIA NA KULITII NENO LAKE ili ulimwengu uendelee kuona MIUJIZA; kwani tukimwachia shetani hii nafasi basi atawatumia watu wake na falme zake kuendelea kuupiga ulimwengu matukio.

Kwa kutambua haya yote, ndipo baadhi ya wanadamu duniani waliuwahi MFUMO WA ELIMU na 'kuuparanganya' kwa kuiondoa HEKIMA YA MUNGU yaani kuiharibu KWELI YA BWANA YESU KRISTO YENYE KUWEKA HURU na kutupa wanadamu AKILI YA ROHONI kisha kuingiza mawazo yao na hekima zao hata wakaziinua juu ya HEKIMA YA MUNGU ili ulimwengu uendelee kuwa utumwani. (Yohana Mtakatifu 8:31-32) (2 Wakorintho 10:3-5); kwa kuanzisha vita kati yao na BWANA YESU KRISTO kupitia ELIMU. (Ufunuo wa Yohana 17:14)

Hii ndiyo sababu Mfumo wa Elimu uliopo sasa hususan barani Afrika umechakachuliwa na baadhi ya wanadamu ili kuendelea kulifanya bara la Afrika kuwa bara la watumwa. Mfumo huu wa Elimu haumwandai Mwanafunzi kuwa mwenye AKILI YA ROHONI yaani HEKIMA YA MUNGU ili Autawale ulimwengu, bali humwandaa Mwanafunzi na wanadamu wote kuwa na akili za mwilini tu huku AKILI ZAO ZA ROHONI zikiwa ndiyo fikra zilizotekwa nao hao baadhi ya wanadamu ulimwenguni hata kupelekea kuishi mawazo yao; wakisema twende kushoto wanaelekea huko, wakisema tuiname wanainama, wakisema tupae wanapaa, wakisema mwabudu shetani ili upate nguvu ya kutawala kwenye eneo fulani wanaabudu, wakisema sasa ndugu abiria tunaingia Sodoma Gomora basi wanaelekea huko, wakisema MUNGU hayupo wanasema sawa, wakidangnywa MUNGU ni fedha, wanyama, wanadamu au madini wanakubali; yaani mwanadamu anafanana na mnyama hata kupelekea kukosa KUTAWALA NA KUWAJIBIKA NA KUSUDI LAKE ALILOUMBIWA NA MUNGU KUJA KULIFANYA HAPA DUNIANI LAKINI BADALA YAKE kuendeshwa na kutawaliwa na watu pasipo kujua kuwa wao ndio wamegeuzwa kuwa viumbe hivi vya ajabu katika ulimwengu wa roho yaani kwa lugha ya ki-mwili tunaita watumwa lakini ki-roho tunaita roho ya msukule; roho iliyompata Mfalme Nebukadreza baada ya kumwacha MUNGU (Danieli 4:33-34). Roho hii humpata mwanadamu pale ambapo fikra za mwanadamu zinaanza kuamini MUNGU hayupo au kuanza kumfananisha MUNGU na vitu vyenye uharibifu kama vile madini, fedha, wanadamu, wanyama, mawe, miti, na kuanza kuviabudu hivyo kisha kumwacha MUNGU.

Fikra za mwanadamu huyu zinakuwa zimetekwa na kuendeshwa na falme za dunia hii zilizopewa mamlaka na shetani kupitia Elimu iliyochakachuliwa na mawazo yao badala ya MUNGU (2 Wakorintho 10:3-5); huku wanatoka hadharani na kudanganya ulimwengu kuwa kuna viumbe vya ajabu vyenye akili kuliko wanadamu pasipo kueleza kuwa viumbe hivi vya ajabu ni wanadamu wawaibiao AKILI ZAO ZA ROHONI katika ulimwengu wa roho kupitia biashara ya miili na roho za wanadamu ambayo pia inafanyika katika ulimwengu wa roho kupitia Mfumo wa Elimu isiyo ya MUNGU ulio katika dunia hii. (Ufunuo wa Yohana 18:12-13)

'Of course' ni viumbe visivyoonekana kwa sababu ni katika ulimwengu wa roho na vita yetu si juu ya damu na nyama bali ni juu falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili na juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho (Waefeso 6:12); hivyo Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla hatutakiwi kupigana naye mwilini ili kumwangusha adui huyu, kwa kumrushia maneno ya kashfa wala ya kumtishia, wala kuinua mabomu ya nyuklia, wala kuinua makombora na mabomu yaliyoshindikana ulimwenguni kwani adui huyu hapiganwi na hakuna mwanadamu wala Taifa litakaloweza kumwangusha kwa vita ya mwilini bali ni vita ya ROHONI PEKEE ambapo ili kuishinda vita hii ni MUNGU KWA NEEMA YAKE Kuinua Mwanadamu, Wanadamu na Taifa ili kumtungua adui huyu kwa mabomu na makombora ya nyuklia yaliyo rohoni huku mwilini tukimwonesha adui huyu tabasamu maridhawa. (Waefeso 6:10-18)

Mfumo wa ELIMU na Mfumo wa UTAWALA tulionao Tanzania, Afrika na Duniani ni Mfumo uliodhamiria kututenga wanadamu na MUNGU; ili roho chafu iliyozima ufahamu wa Mfalme Nebukadreza ikumbe wasomi na wanadamu wote duniani hususan Afrika na kuendelea kuwa watumwa mpaka tunapokubali kumgeukia MUNGU ndipo FAHAMU zetu zinapoturudia. (Danieli 4:33-34)

Tafsiri yake ni kuwa, ili kumwangusha adui wa ulimwengu huu na falme zake wala hakuhitaji makombora, nyuklia, dhahabu, fedha, almasi, na utajiri wa mwilini, bali kunahitaji UTAJIRI UNAOANZIA ROHONI MPAKA MWILINI ambao ni MADINI YA AJABU YALIYOFICHWA DUNIANI nayo ni AKILI YA ROHONI yaani HEKIMA YA MUNGU yapatikanayo katika ELIMU YA MUNGU; NDIYE BWANA YESU KRISTO MWENYEWE. (2 Wakorintho 10:3-5) (Wakolosai 2:2-3)

ELIMU YA MUNGU NI IPI?

Andiko kuhusu ELIMU YA MUNGU ni Andiko langu pia liitwalo KUSHINDA VITA YA ELIMU ambalo naliambatanisha 'attach' pamoja na andiko hili lakini pia lipo kwenye ukurasa wangu wa Jamii Forums uitwao Neema ya BWANA kipengele cha Stories of Change.

Tafsiri yake ni kuwa; VITA KUU DUNIANI NI VITA YA ELIMU; HIVYO KWA NEEMA YA MUNGU KUSHINDA VITA YA ELIMU NDIYO KUSHINDA KWENYE TEKNOLOJIA, UBUNIFU, UCHUMI, AFYA, SEKTA YA MADINI, NDOA, FAMILIA, NA KILA ENEO LA ROHONI NA MWILINI hatimaye KUUTAWALA ULIMWENGU; kwani kukosa AKILI YA ROHONI yaani HEKIMA YA MUNGU kunaweza kumfanya mwanadamu aliyelala na njaa akaamka asubuhi kwa unyonge akaombe makombo ya chakula kwa Mama N'tilie huku njiani akipiga mateke vipande elfu vya dhahabu akidhani ni mawe yanamtaka ajikwae adondoke.

UTAJIRI NA HAZINA ya Taifa lolote kubwa duniani ni AKILI YA ROHONI ITOKANAYO NA HEKIMA YA MUNGU; yaani ELIMU YA MUNGU ambayo inatoa mafunzo ya HADHI YA JUU YA TEKNOLOJIA, SANAA NA UBUNIFU kwa VITENDO. (Mwanzo 1-2) (Kutoka 31:1-6) (Kutoka 35:30-35)

Hii ni kwa sababu matunda ya UBUNIFU NI YENYE THAMANI KUBWA na hayana ukomo, ni matunda ambayo huzalishwa kama chemichemi ya Maji ambayo kila siku hutoa Maji mapya. Hii ndiyo sababu kwa mataifa yaliyoendelea; WABUNIFU WENYE AKILI YA ROHONI; HEKIMA YA MUNGU; kwao ni wenye THAMANI kuliko fedha na dhahabu.

Kumbuka: tusitegemee akili zetu wenyewe kwani kwenye akili zetu wanadamu ndipo shetani alipo (Mathayo Mtakatifu 16:23); hivyo turuhusu HEKIMA YA MUNGU ifanye kazi ndani yetu ili ituletee UHURU WA FIKRA, UHURU WA ROHO NA UHURU WA MWILI, UHURU WA TANZANIA, UHURU WA AFRIKA NA UHURU WA DUNIA NZIMA. (Mithali 3:5-6) (Yohana 8:31-32)

HITIMISHO
Madini ya THAMANI yaliyofichwa DUNIANI ni AKILI YA ROHONI kwa wanadamu kutokana na baadhi ya watu kuharibu MFUMO WA ELIMU Aliotuwekea MUNGU na kuzifanya Akili za wanadamu wa ulimwengu huu ziyaishi maneno na mawazo ya wanadamu wenzao kina Plato, Socrates, Aristotle na wengineo ili kuwazuia waendelee kuwa watumwa badala ya kuacha wanadamu tujifunze kupitia MFUMO WA ELIMU Aliotuwekea MUNGU ili AKILI zetu zimtambue BWANA YESU KRISTO, tuyaishi MANENO YAKE NA HATIMAYE TUWE HURU NA TUUTAWALE ULIMWENGU PAMOJA NA BWANA YESU KRISTO. (2 Wakorintho 10:3-5) (Yohana Mtakatifu 8:31-32) (Ufunuo wa Yohana 20:4)

Imeandaliwa na Mwanafunzi wa BWANA YESU KRISTO; hivyo mimi niliyeandika andiko hili ninakiri kuwa BWANA YESU KRISTO NDIYE ROLE MODEL WANGU PEKEE.
 

Attachments

Upvote 2
Back
Top Bottom