Madini ya uranium naweza kupata wapi soko lake?

beleza

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
397
Reaction score
144
Kuna sehemu ya nchi jirani nimekutana na jamaa mmoja anauza madini kwa mzungu flani hivi baada ya kumdadisi kwa kina nikahisi ni Madini aina ya uranium sababu nilitaka anipe sample nione lakini akasema hawezi kuyafungua mpaka avae nguo zake maalum ndio afungue, ila katika maongezi yetu aliniambia nikipata soko niende atanipatia ninayotaka na nilimuuliza ni aina gani akasema ni uranium na nikamuuliza hizo nguo kapata wapi?

Akajibu huyo mzungu ndio kamletea vipi linaweza kuwa deal hili au majanga kwa TZ? Sababu ni lazima nije nayo Tanzania.

Naomba msaada kwa anaelewa soko lake na inaruhusiwa na serikali?
 
Peleka Syria Isis wanayahitaji sana na wanalipa hela ndefu sana
 
Reactions: MC7
Njoo nayo tu, serikali iko poa sana...kama watazngua watakuweka mahala salama tu
 
Unaweza ku supply kiasi gani??tani??kg100 ??Tuanzie hapo
 
Hizi ni taarifa nzuri za kiintelijinsia ambazo taasisi zetu uchwara zimelala zikisuburi kupelekewa uthibitisho badala ya kuzifanyia uchunguzi. .
 
Peleka Syria Isis wanayahitaji sana na wanalipa hela ndefu sana

Asante sana kwa ushauli wako.na nimekuelewa sana .kwa jinsi comment zilivyo nahisi tanzania haifai kuja nayo.asanteni sana wote kwa michango yenu.
 
Asante sana kwa ushauli wako.na nimekuelewa sana .kwa jinsi comment zilivyo nahisi tanzania haifai kuja nayo.asanteni sana wote kwa michango yenu.
Tanzania tunayo ya kutosha sisi wenyewe tunatafuta soko zuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…