Madini ya Zinc yanayopatikana kwenye pweza yanaongeza uzalishaji wa homoni ya kiume

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili umethibitisha nyama ya pweza (supu ya pweza) inasaidia kuongeza hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa.

Madini ya Zinc kama moja ya madini yanayopatikana kwenye pweza yanaongeza uzalishaji wa homoni ya kiume (testosteroni) ambayo huhusika katika kusisimka kwa mwanaume na tendo la ndoa. Omega 3 ambayo hupatikana kwenye pweza ni muhimu kwa kinga ya mwili & ukuaji wa ubongo wa mtoto.

Nyama ya pweza ina madini kama zinc, chuma, kalsium, fosforasi, potasiumu na seleniam. Pia ina vitamini A, B, C pamoja na Omega 3 kirutubisho kinachohusishwa na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, saratani na huzuni/kushuka moyo (depression).



Tiba Fasta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…