Ni kama nimesikia kwamba tufikirie kuanza kuchimba madini yaliyopo katika baadhi ya hifadhi zetu.
Hoja haipingwi kwa kupigwa rungu lakini nilikuwa nadhani tufikirie na yatokanayo baada ya kuanza kuvamia hizi mbuga na kuanza kufukua chini.
Huenda ikawa mazingira tuliyoyapigania kwa muda mrefu na kuifanya Tanzania kuwa kivutio yakaporomoka na kuharibiwa na kuifanya Tanzania isiwe ya kuvutia tena.
Ni kweli kabisa na hili halina shaka kwamba Simba na Tembo huwa hawali madini yaliyop chini ardhini lakini hakuna shaka vilivile kwamba vilivyopo juu ya ardhi vina thamani tena endelevu.
Kwa sasa tuendelee tu na madini yaliyopo nje ya hifadhi kwani ni mengi tu na hayaishi leo na hata hivyo kuna changamoto nyingi ambazo hatujazitatua za madini yanayochimbwa katika maeneo mengine nje ya hifadhi.
Tujikite kwanza huko,tuache kwenda mbio.