Madini yangu kuhusu FOREX Trading!

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Kwa kiasi kikubwa nimeepuka kujihusisha na huu mjadala lakini nimeona nitoe haya madini ili kuwasaidia hasa wale wenye nia ya kuingia lakini wanapotoshwa na either usiri wa wanaoipromote au misinformation ya wale wanaoiponda. Nitatoa haya madini kwa ufupi.
  • watu wengi (ikiwemo platforms za forex) wanaopromote forex trading, target yao ni hela ya training na training materials. Nilifuatilia platform moja inaitwa 'swipetrade', kuna jamaa alisema wazi ametengeneza hela nzuri tu mule ila akasema wazi as a platform, pamoja na kwamba wanakupa tools zenyewe za kufanya trading, target yao hasa ipo kwenye kutoa mafunzo na ndipo wanapotengeneza pesa yao, na unaweza kwenda kuitumia hiyo knowledge popote, kwa sababu ni universal knowledge siyo specific kwa platform. Kwa mnaoandama watu wanaocharge 200K kwa training, niwaambie hiko siyo kitu kigeni, unfortunately.
  • FOREX siyo biashara ngeni. Inaweza kuwa ngeni kwako, lakini imekuwepo enzi na enzi. Hata kwenye Biblia inazungumzia biashara ya aina hiyo (2 Wafalme 7:1-2, Mhubiri 11:1-6).
  • Forex trading inatumika hasa hasa kuongeza mtaji wa biashara zingine. Hii hata wafanyabiashara wakubwa ndivyo wanavyofanya. Watu wanatumia faida wanayopata kwenye forex trading wanaenda kufungua mahoteli, viwanda na hata kuinvest kwenye stock za makampuni mengine. Kwa hiyo unapowatuhumu watu kuwa wanatumia hela yao kuinvest kwenye kilimo, unakuwa haujua nature na purpose ya forex trading.
  • Online Forex trading inafuata same principles kama za bureau de change au wale wauzaji wa fedha mipakani. Exactly same principles! Tofauti tu ni kuwa kwa online unakuwa haushikilii hard cash. Dunia imeendelea jamani, mitandao haipo tu kwa ajili ya udaku, kuchat na kupoteza muda, serious businesses zinafanyika humu. Watu wananetwork, wanashirikiana kufanya biashara, wanaexchange goods and services bila hata kufahamiana kwa sura au kujuana sauti.
  • Forex trading inahitaji uwe unafuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea duniani. Pamoja na kusoma na kujifunza jinsi actual trading inavyofanyika, unahitaji kuwa mfuatiliaji wa karibu wa mambo ya kiuchumi, kifedha, kisiasa ndani ya nchi mbalimbali lakini pia yanayohusiana kati ya nchi na nchi (bilateral relationships).
Short Story: Miaka kadhaa nyuma, kuna mama mmoja wa kiyahudi niliyekuwa nafanya kazi na mume wake aliwahi kuniambia siri moja (na unajua wayahudi wanajua siri zote za mambo ya fedha). Aliniambia kuna mchezo wajanja wanafanyaga, mfano inabidi waidhinishe malipo fulani (mfano, mishahara, malipo ya tenda, nk.), hao watu wanachelewesha ile hela, wanaichukua wanaenda kuiinvest sehemu kwa siku kadhaa, wakipata chao, ndiyo wanairelease, no trace of any wrongdoing! Hapo imagine, umechukua bilioni kadhaa ukazitupia kwenye forex trading ukitumia trustworthy experienced broker, hapo tunaongelea hela ndefu. Guess ni biashara gani pekee unaweza kufanya kitu kama hicho? Nasubiri jibu! Usishangae Tanzania hii hii watu wamekuwa wanapiga hela ndefu tu kwenye Forex trading kimya kimya.

SIRI YA UTAJIRI: nitakupa siri moja ambayo unaweza kuwa haujawahi kuisikia. Kama unataka kuwa na utajiri usioyumba kirahisi na ambao hata vizazi vyako vijavyo vifaidike, usiweke hela yako kwenye uchumi mmoja, kwa maana ya usiuweke kwenye nchi moja. Kwa mfano, leo hii, TZ ikitokea hali ya sintofahamu na kama hela yako yote umeiwekeza katika uchumi wa TZ, inaweza kupukutika overnight, ndani ya masaa 24 unatoka kuwa milionea na kuwa ombaomba. Realistically, siyo rahisi kwa mtu wa kawaida kuanza kusafiri kutafuta fursa Zambia, Rwanda, Kenya, USA, Japan, nk. Forex trading ndiyo njia rahisi zaidi inayokupa hiyo nafasi kwa sababu unaposhiriki, ni kama vile unainvest kwenye uchumi wa nchi hizo, hata kama ni kwa muda mfupi. Unaposhikilia dola ukitegemea thamani yake ipande ili uiuze, kuna factors za kiuchumi ndani ya Marekani zikitokea na kweli zikapandisha thamani ya dola, wewe unafaidika pale utakapouza ile dola.

NAKARIBISHA MAONI.
 
ahahaha ngoja nisogeze kiti, nikusaidie maana watakuja na mapovu si ya nchii hii.


 
acheni ushamba kwa kupenda ganda la ndizi
 
Mambo mageni yanapoingia mjini lazima yasumbue watu akili.
Lakini mako yatakaa sawa tu
 
Pia kwa nature ya biashara inavyohitaji akili kubwa,watakaokuwa wanafaidika ni wachache sababu kuhimili propaganda zinazoendesha hii market lazima uwe na 'extra powers'
 
Tanzania inaangamia kwa kukosa watu wenye hekima na maarifa
 
Nakuja kuifanyia update hi ya mambo kadhaa niliyoyaacha.
 
Wasipokuelewa hapa, watakua na shida mahali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…