Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Geita limesema kwa asilimia 95 limetekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kukamilisha miradi mbalimbali ambayo inaendelea kujengwa na iliyokamilika katika Halmashsuri hiyo .
Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bi. Khadija Said wakati wa uwasilishaji taarifa ya utekelezaji shughuli za maendeleo ngazi ya kata kwa kipindi cha Oktoba na Desemba 2024 huku akikiri kuwepo kwa miradi ya CSR kutokukamilika kwa wakati na kusema miradi hiyo tayari imeanza kutekelezwa.