Tetesi: Madiwani kulipwa mshahara wa Tsh 1,000,000 kwa lipi?

Wanastahili maana hamna maendeleo bila madiwani kaka
Acha utani
Diwani ni kapuku tu, serikali kuu ndio kila kitu. Diwani haelewi chochote. Tunajenga bwawa la umeme, diwani anaelewa nn? Tunajenga sgr diwani anaelewa nini?
 
Ni sahihi, ila kigezo cha elimu kiongezwe angalau elimu ya kidato cha 4
 
Mbona million 1 ni pesa ya kawaida sana kwq cheo na majukumu ya diwani
 
Diwani ana kazi kubwa kuliko mbunge,mbunge kazi yake bungeni ni kusema "Ndiyooooooooooooooo" na kupiga piga meza ovyo!.

Maendeleo yote ya masoko,barabara mitaani n.k ni kazi nzuri za madiwani!
 
Hapo ndio nisipoona kazi ya mbunge,bora hiyo kazi ya mbunge angepewa diwani tu!naona ndio wenye kazi kubwa au cheo cha mbunge na diwani niwe kimoja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…