madiwani kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba

madiwani kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,425
Reaction score
4,768
Ningependa kujua msimamo wa chadema juu ya wajumbe wa mabaraza ya katiba nchini.
Nimesikia kuwa mabaraza haya ya katiba wilayani yataundwa na madiwani wa majimbo husika + wajumbe wengine wa kuchaguliwa wapatao 8.

Tatizo langu linahusu hapo kwenye madiwani kuingizwa kama wajumbe wa mabaraza haya kwani kama tunavyojua ccm ina madiwani wengi kuliko vyama vingine.je hili halitaathiri maamuzi ya mabaraza haya kiasi cha kuifanya katiba iwe yenye maslahi ya ki-ccm?

Nawasilisha...
 
mwisho wa siku tusije kulalamika kuwa mchakato wa katiba umebakwa na ccm
 
jukwaa la katiba limepinga ushiriki wa madiwani katika mabaraza ya katiba ya wilaya.this is a good move!
 
huu utaratibu co sawa kabisa. yote hii inataka kufanywa,mosi, kukwepa gharama na wakati huohuo kuyabeba maccm. haikubaliki kabisa. uwekwe utaratibu wa kuchagua watu wengine tofauti na madiwani. tume ya warioba imepewa kasma ya kutosha kuhakikisha katiba inapatikana. wakileta katiba mbovu wallahi watalaaniwa na mwenyezi mungu mwingi wa rehema.
 
kwa madiwani kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba na kutotaja sifa za wanaopaswa kuwa wajumbe inaonesha hao watu washapangwa na wanajulikana. Jaji anapaswa kwanza alete rasimu ya katiba tuisome kisha sisi wananchi ndio tutaamua kutokana na content kwamba kwa rasimu hii wanaoweza kushiriki katika mabaraza ni watu wa aina fulani. Lakini jaji anataka mabaraza kwanza jee tukichagua watu wasioweza kujadili maudhuiyaliyomo kwenye rasimu tutafanyaje?
 
naona serikali imeobebesha tume zigo hili!
 
Back
Top Bottom