Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Mke wa Dk. Slaa abanwa
Adaiwa kutoa siri za ubadhirifu Hanang
na Ramadhani Siwayombe, Hanang
MKE wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, Rozi Kamili, ambaye ni diwani wa Kata ya Basotu (CCM), yupo matatani baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Madiwani wa Halmashauri ya Hanang', akituhumiwa kutoa siri za ubadhirifu wa fedha ndani ya halmashauri hiyo.
Licha ya kamati hiyo ya maadili kuwahoji lakini juzi imeshindwa kutangaza hatua za kinidhamu atakazochukuliwa diwani huyo na wengine watatu wa halmashauri hiyo wanaotuhumiwa kwa kukiuka kanuni za maadili za madiwani.
Madiwani wengine waliohojiwa na kamati hiyo ambao wanasubiri maamuzi ni Anju Mang'ola (CCM), Kata ya Gehandu, Leonard Gepchojiga (CCM), Kata ya Mogitu na Venosa Bura, Viti Maalumu (CHADEMA).
_________________________ Weka kando iyo kisa iko nakutokea.
Je Slaa ameshindwa kumshawishi Mkewe ajiunge na Chadema ?
Ikiwa ameshindwa kumshawishi Mkewe itawezekana kweli kuwashawishi WaTanzania waipinge na kuikataa CCM ?
Kweli ni Demokrasia lakini si kwa mke na mume ,tumeona kwengineko mara zote kwenye kampeni ya kugombea Uraisi Mgombea huwa anafuatana na Mumewe ,sasa watu hawa mbona wanatuchanganya ?
Ao ndio tuamini kuwa ni mapandikizi katika upinzani ,ile kesi ya kuwekewa vinasa sauti imeishia wapi ? Mbona imekufa tu na hakuna lolote ? This is too macha !!

Last edited by a moderator: