Mshume Kiyate
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 6,764
- 896
CHADEMA imewaweka kitimoto madiwani wake watatu wa Manispaa ya Arusha kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho katika hoja ya kumtambua meya wa jiji hilo, Gaudence Lyimo.
Habari zilieleza kuwa madiwani hao walijadiliwa katika kikao kilichofanyika kwenye hoteli ya Bristol chini ya mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na katibu mkuu Dk Willibrod Slaa. Baada ya kukiri makosa hayo katika kikao hicho kilichofanyika Machi 24 mwaka huu, madiwani hao waliomba radhi kwa maandishi na kuahidi kutorudia kitendo hicho kilichochukuliwa kama usaliti wa chama.
Taarifa zimewataja madiwani hao kuwa pamoja na diwani wa kata ya Sekei, Chrispine Tarimo, diwani wa kata ya Eunutoto, Elbariki Malley na diwani viti maalumu, Rehema Mohamed. diwani Tarimo alisomewa tuhuma za kukisaliti chama kuhudhuria kikao cha kamati ya Elimu,Afya na uchumi. Elbariki yeye alisomewa tuhuma za kuambatana na Meya wa Arusha kwenye ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara.
Source: Mwananchi Machi 29, 2011