Madiwani wa iliyokuwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam walitoka wapi?

Madiwani wa iliyokuwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam walitoka wapi?

Penologist

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Posts
790
Reaction score
1,923
Habari za wakati huu wakuu, natumaini wote tu wazima buheri wa afya na mafua ya kubana yatupitie mbali, twende kwenye mada moja kwa moja.

Mamlaka za Serikali za Mitaa zinajulikana kama halmashauri, hizi mamlaka zipo ngazi tofauti tofauti kuanzia chini hadi ngazi ya juu. Ngazi za chini ni halmashauri ya kijiji na serikali ya mtaa, inafwata mamlaka ya mji mdogo (town council), inafwata halmashauri ya wilaya (district council) na halmashauri ya mji (town council), inafwata halmashauri ya manispaa (municipal council) na ya mwisho ni halmashauri ya kijiji (city council).

Hizi halmashauri zote zinaongozwa na vyombo vitatu ambavyo ni:
(1) wawakilishi wa wananchi (councillors) hawa huchaguliwa na wananchi mfano ni wenyeviti wa vitongoji kwenye halmashauri ya kijiji au madiwani kwenye halmashauri ya wilaya.

(2) Wataalam hawa hiajiriwa au kuteuliwa mfano ni wahasibu,maafisa mipango,maafisa kilimo mkurugenzi na watendaji.

(3) Kamati zinazoundwa kushuhulikia mambo mbalimbali hizi zinaweza kuwa za muda mrefu au muda mfupi (committee) wajumbe wake wanapatikana kwa kuteuliwa au kuchaguliwa.

Kwa kawaida Halmashauri ya manispaa ikipandishwa hazi ndiyo inakuwa jiji,mfano manispaa ya arusha ulivyo pandishwa hazi ikawa jiji la Arusha madiwani wakawa councillors wa halmashauri ya jiji la Arusha, mwenuekiti wa halmashauri akawa Mayor wa jiji la Arusha, mkurugenzi wa manispaa akawa mkurugenzi wa jiji, wataalam na experts wakawa wataalam wa jiji.

Ila kwa Dareslaam ni tofauti mkoa mzima wenye ulipandishwa hazi ilihali manispaa zote zikibakia kuwa halmashauri zinazojitegemea (autonomous councils).

Swali linakuja sasa councillors wa jiji la Dar es Salaam walikuwa wanachaguliwa na wananchi wapi ikiwa kila manispaa ilikuwa tayari na madiwani wake?

2. Wataalam na expert wa jij la Dar es Salaam walikuwa wanafanya kazi gani ikiwa kila manispaa ilikuwa na wataalam wake na mkurugenzi wake?

3. Committees za jiji la Dar es Salaam zilikuwa na kazi gani na chanzo chake kilikuwa nini ikiwa kila manispaa ilikuwa na committees zake.

4. Baada ya jiji hewa kuvunjwa wale wataalam watapelekwa wapi,hao councillors hewa watapelekwa wapi mkurugenzi wa jiji hewa ataenda wapi, committee za jiji hewa zitaenda wapi?

Wataalam wa local government administration njooni apa mseme hii sanaa ilikuwaje.
 
Hamashauri zote 3 zipewe hadhi ya jiji.

Temeke, kinondoni, Ilala.
 
Hamashauri zote 3 zipewe hadhi ya jiji.

Temeke, kinondoni, Ilala.
Unaweza ukawa sahihi, ebu tufikiri kama tanga ni jiji kwanini Kinondoni isiwe jiji? Hivi Tanga inaingia Mara ngapi kwa Kinondoni?
 
Zamani walikuwa wanatokana na hao hao waliochaguliwa na wananchi wa hizo Knondoni, Ilala nk nk, ilikuwa ni kama kakamati kadogo. Halafu kunakuwa na Meya wa City ambaye yeye ni kama ceremonial figure tuu hana makali yoyote, nadhani mnamkumbuka Mzee Sykes, Jerry Slaa na wa miaka ya karibuni sikumsikiaga maana Makonda aliwafunika sana tuu. Ndio hizo nafasi za ulaji tuu zisizo na tija.
 
Magufuli anavuruga nchi, the next gov will be having a lot to dismantle! Hii Katiba inabid hata kama kwenda "msituni" kuifuta maana mamlaka aliyonayo Rais ni makubwa sana sana sana. Anafanya lolote analosikia kulifanya , we are treated like objects at his disposal, we can be fired and hired at his free will!
 
Hii ni ya Pawpaw na Papai, Councillor na Diwani ni nani na nani! Alisema hawakuchaguliwa na wananchi! Si unajua ule uliotarajiwa kuwa uchaguzi wa mwenye dola hashindwi na CCM itatawala zaidi ya miaka tisini ijayo! Hilo ndilo jibu la swali lako.
 
Back
Top Bottom