Pre GE2025 Madiwani wapendekeza jimbo la Dodoma mjini ligawanywe

Pre GE2025 Madiwani wapendekeza jimbo la Dodoma mjini ligawanywe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Halmashauri ya Jiji la Dodoma imejipanga kutoa huduma kwa wananchi wote kwa kuzingatia mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini wenye mapendekezo ya kuligawa jimbo hilo kuwa Jimbo la Mtumba lenye kata 20 na Jimbo la Dodoma Mjini lenye kata 21.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Frederick Sagamiko, mara baada ya majadiliano na Madiwani kuhusu taarifa iliyowasilishwa na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Albert Kasoga kuhusu mapendekezo ya mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini, wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani uliofanyika Machi 12,2025.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Mgawanyo huu kwa sasa unalenga mgawanyo wa jimbo kuwa majimbo mawili, bado tutaendelea kuwa na halmashauri moja kwa maana ya utoaji huduma kwa ngazi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Jiji litaendelea kuwajibika katika utoaji wa huduma katika majimbo yote mawili”.
amesema Dkt. Sagamiko

Jimbo la Dodoma Magharibi litakalokuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 1,290.6, wapiga kura 385,000 kata 21, mitaa 123, shule za msingi 49, shule za sekondari 21, vituo vya afya vitano na zahanati 21.

Hata hivyo, kwenye mapendekezo hayo madiwani wamependekeza majimbo hayo yaitwe Jimbo la Mtumba (Dodoma Mashariki) na Jimbo la Dodoma Mjini (Dodoma Magharibi)

Ambapo kata zilizopo Jimbo la Dodoma Mjini (Dodoma Magharibi) ni Majengo, Madukani, Nkuhungu, Kizota, Kilimani, Mbabala, Uhuru, Kikuyu kusini, Kikuyu Kaskazini, Hazina, Mnadani, Mkonze, Matumbulu, Nala, Chamwino, Chang'ombe, Chigongwe, Mbalawala, Zuzu, Ntyuka na Mpunguzi.

Na kata ambazo zipo Jimbo la Mtumba (Dodoma Mashariki) ni Kiwanja Cha ndege,

Makutupora, Ngh'ong'ona, Tambukareli, Makole, Mtumba, Dodoma makulu, Chahwa, Msalato, Iyumbu, Nzuguni, Ipagala, Miyuji, Ihumwa, Kikombo, Chihanga, Viwandani, Hombolo Makulu, Hombolo Bwawani na Ipala

jimbo dodoma.png

Madiwani wa Jiji la Dodoma wamesema mapendekezo yao yakipitishwa watafurahi kwa kuwa jimbo hilo ni kubwa na lina kata nyingi za kuhudumia. Kwa sasa jimbo hilo linaongozwa na Anthony Mavumbe ambaye pia ni Waziri wa Madini.

Wendo Kutusha ambaye ni diwani wa viti maalumu amesema Jimbo la Dodoma Mjini lina kata 41 ambazo ni nyingi kulinganisha na majimbo mengine Tanzania, ambapo yana jumla ya kata nane tu.

Amesema kama mapendekezo yao yatapitishwa wananchi watakuwa wamesogezewa huduma karibu, tofauti na sasa ambapo jimbo linatakiwa kuhudumia kata nyingi ambazo wakati mwingine hazifikiwi na huduma.

Kinachofanyika Dodoma ni sawa na maeneo mengine ambayo yanaendelea na utaratibu wa kupendekeza kugawanywa kwa majimbo.

Hatua hiyo inatokana na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kutangaza kuanza mchakato wa kuchunguza na kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi.

Katika maandalizi hayo, INEC ilisema itaanza kupokea mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali Februari 27 hadi Machi 26, mwaka huu.

INEC ilitangaza utaratibu huo Februari 26, 2025 ambapo Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma alisema Tume hiyo itaanza mchakato wa kuchunguza na kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi hadi Machi 26, 2025.

Source: Mwananchi
 
Halmashauri ya Jiji la Dodoma imejipanga kutoa huduma kwa wananchi wote kwa kuzingatia mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini wenye mapendekezo ya kuligawa jimbo hilo kuwa Jimbo la Mtumba lenye kata 20 na Jimbo la Dodoma Mjini lenye kata 21.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Frederick Sagamiko, mara baada ya majadiliano na Madiwani kuhusu taarifa iliyowasilishwa na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Albert Kasoga kuhusu mapendekezo ya mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini, wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani uliofanyika Machi 12,2025.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Mgawanyo huu kwa sasa unalenga mgawanyo wa jimbo kuwa majimbo mawili, bado tutaendelea kuwa na halmashauri moja kwa maana ya utoaji huduma kwa ngazi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Jiji litaendelea kuwajibika katika utoaji wa huduma katika majimbo yote mawili”. amesema Dkt. Sagamiko
Hata ikulu igawanywe
 
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma imependekeza jimbo la Dodoma Mjini kugawanywa na kuwa na majimbo mawili ya uchaguzi kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi jana Jumatano Machi 12, 2025, Ofisa uchaguzi wa Jiji la Dodoma, Albert Kasoga amesema mgawanyo wa jimbo hilo umezingatia mambo yote muhimu ili kutoathiri hali ya kiuchumi ya jimbo moja kutoka kwa lingine.

Amesema mgawanyo huo utatoa majimbo mawili ambayo ni Jimbo la Dodoma Mashariki litakalokuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 1,187.9, wapiga kura 412,000, kata 20, mitaa 99, shule za msingi 59, shule za sekondari 25, vituo vya afya vinne na zahanati 20.

Jimbo la Dodoma Magharibi litakalokuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 1,290.6, wapiga kura 385,000 kata 21, mitaa 123, shule za msingi 49, shule za sekondari 21, vituo vya afya vitano na zahanati 21.
1741869860827.png
 
Back
Top Bottom