Madonna ashindwa kesi ya barua ya kutemwa na Tupac Shakur

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Malkia wa muziki wa Pop kutoka nchini Marekani na mshindi wa tuzo za Grammy, Madonna ameshindwa kesi ya haki ya kulinda kutotolewa kwenye jamii kwa mambo yake binafsi na marehemu Tupac Shakur.

Mwaka jana, mwana mama huyo alikwenda mahakamani kuzuia mnada uuzwaji wa barua ya kutemwa na Tupac. Hata hivyo, jitihada zake hizo zimegonga mwamba.

Barua hiyo ambayo iliandikwa na hayati Tupac ambaye alikuwa mpenzi wa Madonna katika kipindi ambacho hakikufahamika, inatarajiwa kuuzwa kwa mnada mwezi Julai mwaka huu.

Tupac aliandika barua hiyo kwenda kwa ex wake huyo Januari 15, 1995 ikiwa ni miezi 18 kabla ya kifo chake. Sasa barua hiyo inatarajiwa kuuzwa kwa kianzio cha dola 100,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 228 za Kitanzania.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…