Madonna: 'Mwanangu atakuwa rais wa Malawi'

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Nyota wa muziki wa pop nchini Marekani Madonna amesema kuwa mwanawe David Banda atakuwa rais wa Malawi siku zijazo katika ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa Twitter akimsifu mvulana huyo mwenye umri wa miaka 12.

Mwanamuziki huyo wa Marekani ana watoto sita ,wanne akiwa aliwahasili kutoka Malawi. Madonna amekuwa na uhusiano mbaya na mamlaka ya taifa hilo la kusini mashariki mwa Afrika.

Mwaka 2013 Malawi ilimshutumu Madonna kwa kutumia ushawishi wake kuwatishia maafisa wa serikali akisisitiza mchango wake kwa taifa hilo mbali na kutaka kupewa heshima.

Meneja wa Madonna aliishutumu serikali ya Malawi kwa kiuwa na chuki dhidi ya shirika la hisani la nyota huyo la Raising Malawi ambalo alilianzisha 2006 mwaka huohuo aliomuasili David.

David Banda ndio mkubwa kati ya watoto hao wanne. Uasili wake ulizua hisia kali miongoni mwa raia kwa kuwa sheria ya Malawi inawataka wazazi waliomchukua mtoto kuishi ndani ya taifa hilo mwaka mmoja kabla ya kuasili mtoto.

Kikwazo hicho kiliondolewa kwa nyota huyo wa muziki ambaye alimwambia Oprah Winfrey wakati huo kwamba hakuna sheria za kuasili ambazo zilikuwa zinadhibiti uasili wa kigeni.

Mwaka 2009, mahakama ya taifa hilo ilikataa ombi la Madonna la kuasili msichana chini ya sheria kwamba hajaishi katika taifa hilo la Afrika kwa miezi 18 ili kuweza kuasili.



Baada ya kukata rufaa mahakama ya juu ilimpatia haki za kuasili mwanawe wa pili kutoka Malawi Mercy James.

Mwaka uliopita ,Malawi ilimpatia nyota huyo ruhusa nyengine ya kuasili tena na akawa mama wa pacha wa kike Esther na Stella Mwale.

Chanzo: BBC Swahili
 

Attachments

  • _100114203_madonnanson.jpg
    18.5 KB · Views: 77
Madona angechukua uraia wa Malawi ingenoga zaidi
 
Ani-adopt na mimi nije kuwa Presidaa wa inji hii. Raia wote mtafurahi.
 
Akishaniasili hukohuko nakula na mzigo!daahhh haya kibongo sio maisha aseee siku nikiondoka nchi hii sirudi aseee kama baghdad bana
Haaa haaa...wabongo full kudata, yaan chenga hakuna linaloeweka hapa
 
Kuna kipindi nilisikia mama halisi wa huyo mtoto anamtaka mwanae sijui iliishia wapi!??

Hata mimi ningekua huyo mtoto nisingekubali kurudi kwa mama halisi...
[emoji3] [emoji3] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…