Mabao mawili ya Karim Benzema,moja la Cristiano Ronaldo na lile la Angel Di Maria yalitosha kuipa ushindi wa 4-1 timu ya Real Madrid dhidi ya Racing Santander na kuifanya iendelee kuongoza ligi ya Hispania.Ushindi huo wa watoto wa Mourinho umewafanya kuizidi Barcelona jumla ya point 13 hivi sasa.Barcelona watakuwa uwanjani leo kukabiriana na wanaoshika nafasi ya tatu katika ligi hiyo,Valencia katika uwanja wa Camp Nou.Madrid waanze sherehe za ubingwa?