Madrid Na Man City Kuingia Vita Ya Dunia Kwa Mbappe Rekodi Yake Itachukua Miaka Mingi Kuvunjwa

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri wazi kuwa yupo katika vita nzito ya kuwania saini ya mshambuliaji kinda wa AS Monaco ya Ufaransa, Kylian Sanmi Mbappe Lottin dhidi ya Mabingwa klabu bingwa barani Ulay klabu ya Real Madrid.

Pep Guardiola amesisitiza kuwa “chochote kinaweza kutokea”, kuhakikisha wanafanikiwa katika mbio zao za kumsajili, Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 18 na kuwazidi wapinzani wao Real Madrid.

Mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) klabu ya AS Monaco inatarajia kuweka rekodi ya dunia ambayo huenda ikachukua mihongo miwili ama mitatu mpaka kuvunjwa kwake hii ni kutokana na kuhitaji dau la pauni milioni 161 ikiwa ni sawa na Euro milioni 180 ili kumuachia mshambuliaji wao Mbappe.

Vita ya klabu hizi sasa imeamia katika mchezo wao wakirafiki unaotarajiwa kuchezwa siku ya Alhamisi ya wiki hii katika dimba la Los Angeles Memorial Coliseum uliopo nchini Marekani.

Guardiola amesema vita yao ya kumsajili, Mbappe haija kwisha bado watapambana kuahikikisha wanafanikiwa.
“Mchezaji bado yupo na timu yake ya Monaco”. Guardiola ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari

“Chochote kinaweza kutokea bado tunaendelea kutafuta wachezaji watakao jumuishwa katika kikosi lakini Mbappe ataendelea kusalia katika mahitaji ya timu.”

City mpaka sasa imeshatumia zaidi ya pauni milioni 200 katika dirisha la usajili na Guardiola anawakingia kifua wapinzani wao wa Hispania kuwa hawatashinda katika vita hiyo.

“Madrid hawana zaidi ya vile Manchester City walivyo navyo”, amesema Guardiola.
Dirisha la usajili nchini Uingereza linatarajiwa kufungwa Agosti 31, huku Ligi kuu ya nchi hiyo (Premier League) ikitarajia kuanza Agosti 12 mwaka huu.

My take : Ninamsikitikia sana Pep kwa kutamka kauli yake kwamba Real Madrid hawana zaidi yao Man city, kwa ninavyomjua bwana mapesa Perez kwa kauli hio ya majigambo hio pauni milioni 161 wanayotaka Monaco perez kwa kauli ya Pep anaweza kuinua simu yake na kuwaambia hio naizidisha mara 2.
Dogo naona anachekeleea tu huko aliko kupiganiwa na miamba ya soka raha sana, wewe unayeuza mchezaje unaweka bei ya juu kupita maelezo, wakala nae anachekelea anajua ataanza kufata nyendo za Jorge mendes, mchezaji nae ataweka mshahara wake mara 2 ya anaolipwa.



Maelekezo na Maamuzi kutoka Juu
 
Mkuu huwezi shindani na hizi oil clubs kwa pesa... Man city washavunja rekodi ya all time kutumia pesa nyingi katika dirisha moja la usajili... Hawa waarabu wanataka 'prestige' tu na hawajali kuhusu faida... Madrid yeye mpaka auze ndo asajili... Man city wanaleta vyombo tu

Achana na mbappe kituko ni kwamba ma gwiji wa uhamisho di marzio na mino raiola wameripoti kua PSG wako tayari kulipa release clause ya neymar ambayo ni €220M.. Hamna Ku bargain wala mini

Hizi oil clubs isingekua ffp kuwawekea mipaka ya kusajili wangewanunua Ronaldo na messi wote wakae benchi... Waarabu sio watu
 
Yaan nataman hawa wachezaji wangekutana na kizazi cha pesa hivi Kluivert,de Lima, Ronaldinho(the baddest ever),zidane,pirlo kipind kijana,Thierry ,deco (fundi),giuly,makelele,neuvile, Gerald,van nisterlooy,rivaldo na wengine weng.
.
.
Kyenekyaka nkighanile une

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh halafu lazima mwarabu wa psg amchukue neymar

Maelekezo na Maamuzi kutoka Juu
 
Wachezaji huwa wanaangalia sifa ya timu na uzuri wa ligi, Messi au Cr7 hawezi kwenda ufaransa wakati ligi ni ya kawaida sana

Don't tress urself with knowing all answers to every question. Don't worry nobody will be clever enough to ask you
 
Upo sahihi ,madrid hana ubabe kwa hawa waarabu , madrid ana ubabe kwa clabu za wanachama kama yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…