Madudu yanayofanywa na uongozi wa riadha Tanzania

Madudu yanayofanywa na uongozi wa riadha Tanzania

mhuogomkavu

Senior Member
Joined
Jun 23, 2017
Posts
116
Reaction score
102
Kwanza niwape pole kwa mnayoyapitia tangu mwaka 2016 baada ya kuingia uongozi mpya kwenye Shirikisho la Riadha.

Ninafahamu walio wengi hawatafahamu nini kinachoendelea ndani ya Riadha Tanzania kwani wengi wamejikita kwenye michezo mingine.

Ni hivi, tangu aingie madarakani Rais wa Riadha Tanzania Anthony Mtaka style yake ya kuongoza imekuwa ni ya kupiga deal. Nafahamu huko kwenye Ukuu wa Mkoa anapewa heshima na watu ila masikini hawajui ya kwenye riadha tunateseka.

Nilikuwa naongea na wanariadha fulani, ni mateso makubwa na ufisadi wa kutisha huko. Natamani haya majipu yamulikwe haraka na tutapike nyongo zote mwaka huu kabla haujaisha

Hawa viongozi wa Shirikisho wanalifanya Shirikisho kama Taasisi binafsi mpaka kufikia hatua ya kukataa kutumia Ofisi halali iliyopo katika Uwanja wa Taifa karibu na Uwanja Taifa lakini wao wanataka wafuatwe kwenye Ofisi zao! Viongozi wengine wanapohitaji fedha za kuendesha shughuli za Shirikisho wanajua wanachokifanya. Ni maumivu makubwa sana!!

Rais wa Shirikisho bwana Anthony Mtaka na Makamu wake William Kallaghe inafikia wakati mnashinikiza baadhi ya viongozi wa Riadha Tanzania kuandaa ripoti za matumizi za uongo au hewa ilimradi tu fedha hizo zionekane zimetumika kumbe wamezitia ndani. Mtakumbuka alichofanyiwa Katibu Mkuu aliyejiuzulu bwana Willhelm Gidabuday ambaye alilazimishwa kuandaa ripoti ya matumizi ya Tshs milioni 87 ilihali hakuna matumizi ya aina hiyo. Muulizeni Gidabuday popote alipo. Alitaka kuongea na Waandishi wa Habari kuonyesha wizi huu ila alizuiwa

Nakumbuka ujumbe wake kuita wanahabari baadae akasema ana matatizo ya kifamilia. Nakumbuka aliandika hivi wakati anaahirisha;

“TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ;

YAH: KUAHIRISHA KWA PRESS CONFERENCE
Ndg Wanahabari,
Napenda kuwajulisha kuwa NIMEAHIRISHA KWA MUDA kile nilichopanga kuzungumza Nanyi kesho Alhamisi March 5/2020 kutokana na dharura ya kifamilia.
Hadi hapo mtakapojulishwa.
Ahsanteni.
Wilhelm F. Gidabuday.”

Sijui ni nani alimkingia kifua Anthony Mtaka🤔 na sijui huyu Gidabuday yupo wapi na mafaili haya ya ubadhilifu!

Nakumbuka pia mwaka 2017 ilikuwa mwezi Machi kama sikosei Wanariadha walishiriki Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika nchini Uganda lakini baada ya kurudi nchini Mtaka na genge lake badala ya kuwapongeza alimporomesha matusi Gidabuday kisa amewalipa Wanariadha na Makocha stahiki zao. Je, huo ndo utumishi mwema kweli? Hivi watu huko nje ya Ukuu wa Mkoa wanajua mateso haya tunayopata? Huyu anastahili madaraka zaidi au ndio atatumaliza? Kama hivi tu tunaumizwa hivi kwa mfano akaelekea kwenye zile ndoto anazozitaka tutapona kweli?

Tena haitoshi wakati Wanariadha wakiwa Uganda nakumbuka Anthony Mtaka Ulipeleka ujumbe wako kuwavuruga wanamichezo kule. Ushahidi nitauleta muda si mrefu! Haya mambo tumechoshwa nayo. Rudi ukawe mkuu wa Mkoa wa Simiyu utuachie Shirikisho.

Juzi juzi hapa baada ya kuona Dodoma wamefanya Marathon nikakumbuka Washindi wa Mbio za Dodoma Hapa Kazi Marathon kukuzonga kwa miaka minne tangu 2016 hadi 2019 wakidai zawadi zao, ukaona uwaite Arusha Wanariadha, Makocha na viongozi wa Arusha kwenye Baa moja maarufu, bila kumjulisha Katibu Mkuu ukawagawia fedha kwa walioenda Uganda na wale waliokuwa wanadai Mabati. Na fedha ulizowalipa zilitoka kwenye mfuko maalum wewe unaujua. Hizo pesa zilikuwa na matumizi mengine ila wewe ukazichepusha. Kama unabisha, tupe taarifa za matumizi ya pesa za Shirikisho☹️. Miaka 4 hujawahi kuandika ripoti ya matumizi ya pesa na bado unataka kuitwa kiongozi muadilifu! Mikutano haifanyiki na umejificha kwenye kichaka cha utendaji mzuri serikalini ila kwenye Riadha mambo yanaharibika.

Fedha zimekuwa zikiingizwa kwenye Shirikisho bila taarifa rasmi na zinatolewa. Hivi zile pesa zaidi ya milioni 20 tulizopewa na Tanesco zilizokuwa kule Benki ya Azania historia yake ipoje na ziko wapi?

Bwana Mtaka anatumia kofia yake ya Mkuu wa Mkoa kuitisha vikao vya Shirikisho na kuanza kuwajadili viongozi ambao wanakwenda kinyume na matakwa yake hata kama wako sahihi. Mara nyingi anawatisha kwa kutumia wadhifa wake na hata wajumbe wengine wanaogopa kumpinga ndio maana mnaona tupo kimya kwa muda mrefu. Sasa basi!

Hivi kweli Uongozi wa riadha hautaki kuwalipa Wanariadha wanaodai zaidi ya Tshs. 6,000,000/= tangu mwaka 2015!!!!! 😳Tena wanariadha hawa walifanya vizuri sana kwenye Mbio za Nyika za Dunia Beijing na wengine walioahidiwa motisha baada ya kufanya vizuri kwenye Kilimanjaro Marathon‼️

Ndugu zangu, kiukweli Riadha Tanzania tuna Viongozi wanaokatisha tamaa, Viongozi ambao wanajali maslahi yao na kutumia shirikisho kama sehemu ya kujitengenezea fedha.

Huu ni wakati wa kufanya mabadiliko makubwa. Tusiogope!

SERIKALI TUNAOMBA SIKIENI KILIO HIKI MAANA TUNAUMIZWA SANA🙏
 
Gidabuday mzee naona uchaguzi umekaribia so unaimendea nafasi kwa kuchafua wengine😅😅😅.
Muda wote huo hukuona huu ubadhirifu Ila leo karibia na uchaguzi kweli??
 
Hii kitu ni very serious, mamlaka husika zichukue hatua, msisubiri madhara makubwa yatokee ndio mje kuchukua hatua, msije mkamtafuta mchawi badae mambo yakishaharibika.
 
Kutwa kufanya mabonanza na marathon zisizoeleweka, mbio za siku 1 zinatumia karibu milioni 300 kufanyiwa maandalizi, badala ya fedha hizo kutumika kuwaandaa vijana hata wawili kwa miaka 2 ili waive na kuleta medani hapa nchini.

Unakuta mbio za namna hiyo ya marathon zinafanyika karibu 6 kwa mwaka 1, na bado shirikisho sijui linasema kuna uongozi..mpaka leo tunarejea kina Filbert Bayi utafikiri baada yao Taifa lilisimama kabisa..hakuna ubunifu zaidi ya madili hayo ya udhamini wa marathoni nk
 
Juzi juzi hapa nilisoma ujumbe wa waandishi wa habari za michezo kuhusu Shirikisho la Riadha Tanzania na Madudu yake na nikaamua kuu share humu. Nilikumbuka mbali sana hasa katika Ile habari ya upigaji na alichotaka kufanya kupitia Press Conference aliyotaka kufanya kiongozi wangu wa zamani, Wilhelm Gidabuday ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa RT.

UZI: Madudu yanayofanywa na uongozi wa riadha Tanzania

Nakumbuka alisema “Napenda kuwajulisha kuwa nitakuwa na mazungumzo nanyi siku ya Alhamisi March 5/2020 Jijini Dar es Salaam, Saa nne Kamili Asubuhi. (10am), Waandishi mtajulishwa venue siku moja kabla ili muweze kufika. Hili halikutimia.

Nakumbuka nilimpigia simu na akasema, Mkutano wake na Waandishi wa Habari ulikuwa ni kutoa taarifa kwa Umma ili wafahamu mambo mbalimbali yaliyokuwa hayaendi sawa pale RT.

Kwa moyo mwema alitaka kuzima sintofahamu inayozushwa na wahusika wakuu wa RT ambao waliamua kufanya Shirikisho kuwa mali binafsi.

Watu wakaniuliza:

1). Kwanini Gidabuday ilibidi ajiuzulu nafasi yake ya Ukatibu Mkuu RT na akawaachia wengine kuendelea kutafuna fedha za Wanariadha kupitia kichaka cha kuratibu mchezo wa Riadha hapa Tanzania?

2). Kwanini Gidabuday alikuwa kimya sana na alipotaka kuongea alipigwa spana kali sana? Sijui yupo wapi huyu Kijana wa Watu!

3). Mnajua kwanini alitaka kuweka wazi nyaraka iliyostahili kuwa ya siri hadharani? Na wakati huo huo yeye anaumia roho yake?

Atakayeweza kujibu haya basi awapigie simu Viongozi wa RT waachie ngazi mara moja. Uozo huu hauwezi kuendelea kuvumilika na sasa tunakwenda kuchagua viongozi wengine wa Shirikisho. Tunataka Viongozi waadilifu.

Nakumbuka baada ya kuona wizi mzito kwenye Shirikisho Katibu Mstaafu wa BMT alisema; nanukuu ”nami nieleze mazito, bila kupepesa macho yaliyopo kwenye Riadha na Shirikisho kwa Ujumla wake.

Kuna ambao wanadhani wata - reverse hayo machafu kwangu; lakini mimi siogopi chochote , maana Duniani Tunaishi Mara Moja tu ; Never Twice... akamalizia kwa kusema * Karibuni sana.....W.F.Gidabuday.*

TUNAHITAJI RT MPYA NA VIONGOZI WAPYA.
 

Kwa nini Viongozi wa Riadha Tanzania wamejikita kwenye ubadhilifu wa fedha zaidi kuliko riadha?​


Shirikisho la Riadha Tanzania linapika katika kipindi kigumu sana. Tangu kuchaguliwa viongozi walioko madarakani sasa, mchezo wa Riadha umekuwa ni wa kushiriki na kushindwa. Nchi za wenzetu tunaona mafanikio ila kwetu Viongozi wanakula pesa, wanachangisha pesa na wanadhulumu washiriki wa mashindano hayo.​

Huu ni mwanzo wa safari mbaya ya Viogozi wote wa Riadha Tanzania. Kaeni chini, jipangeni upya MTUPISHE. Nendeni mkafanye siasa hili Shirikisho mtuache wenye utalam nalo tufanye kazi.​

Nitarudi na makabrasha yao hao​

 
Shirikisho la Riadha Tanzania Lina Mizengwe Mingi, Ni jana tu, kulifanya Uchaguzi wa viongozi wa Mkoa ,walishindwa kupata Mwenyekiti wa chama cha Riadha Mkoa wa Arusha.

Hivyo, Serikali iingilie kati na Kuvunja au Kusambaratisha Uongozi Wote kwa Ujumla.
 
Gidabuday mzee naona uchaguzi umekaribia so unaimendea nafasi kwa kuchafua wengine😅😅😅.
Muda wote huo hukuona huu ubadhirifu Ila leo karibia na uchaguzi kweli??
Wewe ndio Umechelewa Kufahamu, Gidabuday yuko Sahihi.
 
Back
Top Bottom