Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Licha ya kuripotiwa kuwepo kwa suluhu kwenye baadhi ya madai ya Wafanyabiashara waliyowasilisha Serikalini na kufanyika kikao cha pamoja lakini mpaka kufikia Saa tatu Asubuhi hali ya mgomo inaonekana kuendelea maeneo ya Kariakoo ambapo maduka mengi yameendelea kufungwa.
Itakumbukwa kwamba jana June 24, 2024, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitoa wito kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo kufungua maduka yao na kuwataka wasitishe mgomo.
Hata hivyo alidai Serikali inaweza kuweka ulinzi eneo la Kariakoo hata kwa mwezi mzima, kama wataamua kutofungua maduka mpaka madai yao yatakapopatiwa majawabu.