MADUKA YA FEDHA ZA KIGENI

Saeed Eddy

Member
Joined
Nov 21, 2018
Posts
5
Reaction score
1
Baada ya miaka 16 nje ya nchi na mara ya Kwanza nimerudi Tanzania na kuona vitu vya ajabu Sana. Moja wapo no zoezi la kufungwa Maduka ya FEDHA ZA KIGENI. Hii imesababisha kupoteza muda mwingi Sana wa watu kwenda mabenki kubadilisha pesa, na rate ya kubadilisha pia kuwa mbaya Sana kwasababu hakuna competition tena.
Ugumu wa hatua hii ya kufunga Maduka yote yanayobadilisha pesa za KIGENI ni kwamba, Wakati wa jioni au wikiendi wageni hawawezi kupata sehemu ya kubadilisha fedha zao. Mgeni Anatoka Mombasa kuja Dar es salaam. Anafika Dar jioni. Mabenki yamefungwa, na hakuna sehemu nyengine. Je hii itamtia hamu mgeni kutangaza nchi ya Tanzania nje?
Vile vile Rai's Magufuli alisema nenda ulaya kama utaona Maduka ya pesa za KIGENI vichochoroni. Hapana sio kweli. Ulaya yote imejaa Maduka ya FEDHA ZA KIGENI. In fact kila kichochoro, kuna Maduka ya FEDHA ZA KIGENI. Na mengine yako wazi 24hrs
Kuna Sheria nyengine lazima ziangaliwe vizuri. Kuna Mambo mengi ambayo yanataka kurekebishwa. Kama immigration airport kuchukua vidole 4, halafu 2 thumbs na USO pia. Yaani ni vitu ambavyo havifanywi na serekali yoyote duniani. Unalinda borders zako Wakati wa kungia, lakini Wakati wa kutoka, kwanini kupoteza muda?
Kuna nchi nyngi sasa hazina immigration Wakati wa kutoka. Wameondoa kabisa gates za immigration Wakati wa Ku exit nchi. Moja wapo ni US and UK.
 
Kashauriwa vibaya. Tunarudi nyuma Sana. Sasa soko la black market rate limeanza upya kama kipindi cha Julius.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…