Maelekezo: Mnaweza vipi kutoa (withdraw) pesa PayPal Tanzania?

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
PayPal kuna changamoto ya kupokea na ku-withdraw pesa nchini Tanzania. Kuna features huzioni kule PayPal kama ukifungulia account Tanzania, hivyo kufanya ugumu kwa mtu kulipwa pesa kutoka nje. Hii imekuwa ikigandamiza fursa mbalimbali za kimtandao kwa vijana ambao wameamua kutafuta fursa mtandaoni.

Nataka kujua kama kuna watu humu Jamiiforums wanatumia huduma ya PayPal, je wanafanya vipi hili kupokea na ku-withdraw pesa wakiwa Tanzania. Maana kuna kibunda changu mahali sasa nashindwa kukichomoa kwa sababu sioni features za ku-withdraw kwa kutumia PayPal in Tanzania, sasa naogopa kutransfer kuja PayPal account.
 
Ushauri:Waweza tumia skrill kutoa kwa airtel money ni papo kwa hapo.
 
Kwanza paypal tz haipokei pesa.
Inabidi ufungue paypal ya kenya au nchi inayokubali lakini nashauri kenya. Inabidi uwe na line ya safaricom copy ya kitambulisho cha mwenye line so akaunti itakuwa na jina la mwenye line. Pesa ikifika waitoa via safaricom wajitumie kwa mtandao wa tz.
Njia nyingine fungua akaunti ya paypal ya marekani, then fungua payoneer unga akaunti ya payoneer kwenye paypal pesa itatoka paypal kuja payoneer unaweza itoa atm au kuituma kwenye bank yako.
 
Uzi ufungwe hapa.
 
Tanzania tunapokea refund tu hatupokei pesa
 
Hebu njoo nikutengenezee PayPal ya Uk ambayo unaweza pokea pesa popote duniani
 
Hizo links zako za HAPA miyeyusho kwelikweli
 
Mkuu uliweza kuwithdraw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…