Ninafangasi katika vidole vya miguu hasa nikivaa viatu mara kwa mara zinatokeza, pia nina m-ba katikati ya mapaja na baadhi ya maeneo mengine ya mwili. Nimetafuta dawa ktk maduka ya kawaida na kuna dozi ya ASFULVIN vidonge 30 kila siku kimoja, nimeshauriwa kuvimeza usiku. Tangu nianze kumeza yapo matukio yafuatayo yanayonitokea:-
1. Kuharisha bila kuumwa tumbo
2. Kichwa kuuma
3. Nikinywa maji, soda,juisi nahisi uchungu mdomoni.
Je hali hii husababishwa na vidonge hivyo? nini ushauri wenu enyi watibu wema?
Heri ya mwaka mpya.
Ninafangasi katika vidole vya miguu hasa nikivaa viatu mara kwa mara zinatokeza, pia nina m-ba katikati ya mapaja na baadhi ya maeneo mengine ya mwili. Nimetafuta dawa ktk maduka ya kawaida na kuna dozi ya ASFULVIN vidonge 30 kila siku kimoja, nimeshauriwa kuvimeza usiku. Tangu nianze kumeza yapo matukio yafuatayo yanayonitokea:-
1. Kuharisha bila kuumwa tumbo
2. Kichwa kuuma
3. Nikinywa maji, soda,juisi nahisi uchungu mdomoni.
Je hali hii husababishwa na vidonge hivyo? nini ushauri wenu enyi watibu wema?
Heri ya mwaka mpya.
Heri ya mwaka mpya na pole kwa maradhi mkuu MAKOLE,Kwa uelewa wangu kinachokutokea ni side effects za dawa unazotumia, kwa fungus za miguuni,i presume ni katikati ya vidole nakushauri utumie CLOTRIMAZOLE au MYCOTA POWDER (Mycota ni ghali kiasi) hizi unapaka katikati ya vidole asubuhi na jioni kila baada ya kuoga na pia unaweza kunyunyuzia ndani ya socks kabla ya kuzivaa na hii itasaidia kunyonya jasho na kuondoa harufu,matibabu haya undelee nayo kwa wiki 6 hadi miezi miwili.Kwa fungus ya kwenye maungio ya mapaja unaweza pia kutumia mojawapo ya powder hizo hapo juu au pia unaweza kutumia MYCOTA SPRAY,kwa maeneo mengine nakushauri utumie ANTIFUNGAL CREAM yoyote.Cha msingi zingatia yafuatayo;
1.Usafi wa mwili na mavazi ikiwa ni pamoja na kuoga,kupasi na kubadilisha socks kila siku.
2.Jitahidi sana kutumia Socks za COTTON ambazo zinanyonya jasho miguuni.
3.Matibabu ya Fungus yanachukua muda mrefu,mara nyingi sio chini ya wiki sita na matokeo ya tiba huanza kuonekana baada ya angalau siku 10 hadi wiki 2 hivyo uwe mvumulivu.
kama utafanikwa kupona usisahau kuja kutoa mrejesho!
hii dose nilishawahi tumia MAKOLE ukiipatia haina shida ila ndio mpaka iishe na kilo zimeongezeka, niliambiwa na dakatri kupunguza madhara yake unatakiwa kumeza mara baada ya chakula chenye mafuta, kama nyama nono au chakula chenye cheese. Nilifata ushauri haiukusumbua, ni dawa inanguvu sana. Pole sana, natumaini sasa umeshapona.MAMA D wewe ni nouma, bado nipo dozini. hali c mbaya sana
kama inasumbua gawa dozi unywe asubuhi na jioni badala ya mara moja.Jamani ndugu natumia dawa ya griseofulvin..jamani huu mziki mbona hatari maana kichwa kinagonga hatari..nilishauriwa na dokta baada kutumia creams nyingi kama whitfields ointment,sonaderm,clotrimazole na candiderm kushindwa ndio nikapewa japo naanza kuona ka uhafadhar lakin hii side effect yake jaman daah..nishaurin nifanye nin ndugu
Shukran sana kwa ushaurikama inasumbua gawa dozi unywe asubuhi na jioni badala ya mara moja.
207. GRISEOFLUVIN
Dawa ya fangasi (kichwani,miguuni,sehemu za siri,). haitumiki kwa maambukizi madogo madogo.tumia pamoja na vyakula vya mafuta. jikinge na jua kali. usitumie pombe. inaweza chukua muda mrefu kupata matokeo. zingatia usafi. chukua tahadhari uendeshapo mitambo/gari.
Madhara: Kizunguzungu,kichwa kuuma na ukurutu