Maelezo kwa kifupi ya jinsi ya kuanzisha chuo cha elimu ya ufundi stadi nchini

Maelezo kwa kifupi ya jinsi ya kuanzisha chuo cha elimu ya ufundi stadi nchini

Kelela

Senior Member
Joined
Nov 7, 2020
Posts
191
Reaction score
308
MAELEZO KWA KIFUPI YA JINSI YA KUANZISHA CHUO CHA ELIMU YA UFUNDI STADI NCHINI

1 Utangulizi

Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi(VETA) ilianzishwa chini ya sheria Na.1 ya mwaka 1994 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2006 kwa lengo la kusimamia, kuratibu na kuendesha elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini. VETA inasimamiwa na Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VET Board) pamoja na Bodi za Kanda (Zonal Boards) ambazo zinaendeshwa na ofisi katika kanda tisa (9) nchini.

2 Miongozo ya jinsi ya kuanzisha vyuo vya ufundi stadi

Ili kukidhi viwango vya ubora katika kutoa mafunzo VETA imeandaa miongozo ya jinsi ya kuanzisha vyuo vya ufundi stadi katika sekta kumi na mbili (12) na kila sekta ina idadi ya fani zinazomwezesha mwanafunzi kusoma na kwenda kuajiriwa au kujiajiri.

Sekta hizo ni: Ufundi Vyuma, Ufundi Magari, Ufundi Umeme, Kilimo na Usindikaji wa Chakula, Madini, Ujenzi na Uchoraji Ramani za Majengo, Hoteli na Utalii, Teknolojia ya Nguo na Ufumaji, Urembo, Usafirishaji, Biashara na Uchapaji.

Miongozo hii imeainisha viwango vinavyoweza kumsaidia mtu binafsi au taasisi katika kufanya maandalizi ya kuanzisha chuo katika sekta husika na wale wanaomiliki vyuo husaidia kufanya maboresho kwa ajili ya usajili.

2.1 Maelekezo hayo yanahusisha viwango katika maeneo yafuatayo:

i. Michoro ya majengo (kama madarasa, maabara, karakana, majiko, maktaba, stoo, vyoo na ofisi);

ii. Ujuzi na idadi ya walimu na wafanyakazi katika sekta husika;

iii. Idadi ya vifaa na zana za kufundishia katika fani husika ikiendana na idadi ya wanafunzi na walimu; na

iv. Muundo wa uongozi wa chuo.

2.2 Utaratibu

i. Mwombaji mwenye nia ya kuanzisha chuo cha ufundi stadi anatakiwa kutuma barua maombi kwenye kanda husika,

ii. Mwombaji atapewa mwongozo au miongozo kulingana na sekta anayotarajia kutoa mafunzo.Miongozo hiyo inalipiwa gharama kidogo tu.

iii. Mwombaji atajifanyia ukaguzi na kufanya maandalizi kulingana na mahitaji ya miongozo hiyo.

iv. Kama mwombaji anakidhi mahitaji ya kuanzisha chuo ataandika barua kwa Mkurugenzi wa kanda kuomba usajili wa awali;

v. Ofisi ya kanda watampatia mwongozo wa jinsi ya kuandika pendekezo la mradi (proposal).

vi. Mwombaji ataandika pendekezo la mradi na kurudisha ofisi ya kanda kulingana na maelekezo.

vii. Ofisi ya kanda watapitia andiko la mradi na kama limefikia viwango basi, ofisi ya kanda watapanga kukagua eneo husika na baadhi ya maandalizi ya kuanzisha chuo,chanzo cha fedha na vifaa.

viii. Ofisi ya kanda ikiridhika na ombi la kuanzisha chuo,basi,mwombaji atapatiwa barua ya utambulisho kwa usajili wa maandalizi (Preparatory registration). Barua hii ya usajili wa maandalizi itamwezesha mwombaji kufanya maandalizi ya kuanzisha chuo cha ufundi na katika hatua hii mwombaji harusiwi kutoa mafunzo kabisa.

Hivyo basi wadau wote wa Elimu wenye nia ya kuanzisha vyuo vya Ufundi tunaomba mtembelee ofisi zetu za kanda ili kupata miongozo ya jinsi ya kuanzisha vyuo.

Miongozo hiyo inamsaidia mwombaji kurahisiha utaratibu wa kusajili chuo kwani VETA ni washauri wakuu katika hatua zote za uanzishaji.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na ofisi zetu za kanda kwa anuani zifuatazo:

Na.

Ofisi za Kanda Mikoa Anuani

1 Kanda ya kati

Dodoma, Singida na Manyara S.L.P 2084, Dodoma

Simu:026 2322383

Nukushi:0262324120

Barua pepe: vetacentralzone@veta.go.tz

2 Kanda ya Dar es Salaam

Dar es Salaam S.L.P 40274, Dar es Salaam

Simu:026 2862651

Nukushi:026 2862651

Barua pepe: vetadsmzone@veta.go.tz

3 Kanda ya Mashariki

Pwani na Morogoro S.L.P 1955, Morogoro

Simu:023 4526

Nukushi:023 4526

Barua pepe: vetaeasternzone@veta.go.tz

4 Kanda ya Ziwa

Mwanza,Mara na Kagera S.L.P 1983 Mwanza

Simu:028 2573013/4

Nukushi: 028 2573013

Barua pepe: vetalakezone@veta.go.tz

5 Kanda ya Kaskazini

Arusha, Kilimanjaro na Tanga S.L.P 1738, Moshi

Simu:027 2754468

Nukushi:027 2754468

Barua pepe: vetanorthernzone@veta.go.tz

6 Kanda ya Kusini Mashariki

Mtwara na Lindi S.L.P 700, Mtwara

Simu:123 2333821,2333453

Nukushi: :023 2334078

Barua pepe: vetasoutheastzone@veta.go.tz

7 Kanda ya Kusini Magharibi

Mbeya,Rukwa na Katavi S.L.P 2498, Mbeya

Simu:025 2504369/72

Nukushi: :025 2504370

Barua pepe: vetasouthwestzone@veta.go.tz

8 Kanda ya Magharibi

Kigoma,Tabora na Shinyanga S.L.P 1218, Tabora

Simu:026 26048990

Nukushi: :026 2604890

Barua pepe:vetawesternzone@veta.go.tz

9 Kanda ya Nyanda za Juu

Iringa, Njombe na Ruvuma S.L.P 818, Iringa

Simu:026 2702351

Nukushi:026 2700693

Barua pepe: vetahighlandzone@veta.go.tz

Kwa mawasiliano na taarifa zaidi:

VETA Makao Makuu,

S.L. P. 2849,

Dar es Salaam

Tanzania

Baruapepe: info@veta.go.tz au pr@veta.go.tz

Simu: +255 22 2863409

(2015)

Nukushi: +255 22 2863408

Tovuti: www.veta.go.tz
 
Back
Top Bottom