maelezo ya 10 millioni

Abdillahjr

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
694
Reaction score
319
Wakuu heshima kwenu,
Nina cash 10 million tshs,naombeni mnisaidie wazo la biashara,nitashukuru mawazo na mchanganuo wenu,nipo tayari kufanya hiyo biashara kuanzia mwezi huu na mkoa wowote.
 
Jaribu u-promotor hasa wa masumbwi au wasanii wa bongo flava. Unachukua wasanii wenye vimajina wanaenda kufanya shoo huko mawilayani.
Inalipa sana hii biashara. Milioni 10 inatosha kabisa.
 
Sikupi wazo la biashara ila nakupa angalizo moja tu, ..... wazo la biashara toka kwa mtu ambaye hana ujuzi na biashara ni hatari sana. Kuwa mwangalifu sana mkuu
 
njoo huku nilipo nunua ng'ombe kwa laki tatu hadi nne mnenepeshe kwa miezi miwili peleka pugu kauze kwa laki nane na zaidi. Gharama ya kunenepesha ng'ombe mmoja ni laki na nusu. Usafiri ng'ombe mmoja ni elfu 30000. Ananenepeshwa kwa kutumia mashudu ya pamba
 
Wakuu heshima kwenu,
Nina cash 10 million tshs,naombeni mnisaidie wazo la biashara,nitashukuru mawazo na mchanganuo wenu,nipo tayari kufanya hiyo biashara kuanzia mwezi huu na mkoa wowote.
Mkuu sikuzote biashara hutegemea na mtu maana biashara zote zinalipa, ial pia sio kila biashara ni kwa kila mtu, sasa wewe tuambia unauzoefu na kitu, au una ujuzi gani, au unapenda nini. Tutaanzia hapo kukushauri
 
Jaribu u-promotor hasa wa masumbwi au wasanii wa bongo flava. Unachukua wasanii wenye vimajina wanaenda kufanya shoo huko mawilayani.
Inalipa sana hii biashara. Milioni 10 inatosha kabisa.

Asante kwa wazo mkuu japo hilo wazo la upromoter sio kitu ambacho nipo tayari kukifanya,napendelea usambazaji wa bidhaa yoyote halali lakini sio "sembe" ila thanks a lot!
 
Mkuu sikuzote biashara hutegemea na mtu maana biashara zote zinalipa, ial pia sio kila biashara ni kwa kila mtu, sasa wewe tuambia unauzoefu na kitu, au una ujuzi gani, au unapenda nini. Tutaanzia hapo kukushauri

Nina elimu ya chuo lakini sipendelei kuajiriwa,nimeshawahi kuzngua biashara ya kusambaza vitu kwenye hoteli za kitalii ila usimamizi na udogo wa mtaji vikaniangusha lakini sasa nimejifunza vya kutosha.

Na mwisho kabisa amefanya kazi kwenye kampuni ya ununuzi na uuzaji wa madini na ninaongea kwa ufasaha lugha tatu za kimataifa
 
Uko wapi mkuu, ni wazo zuri pia!!
 
Uko wapi mkuu, ni wazo zuri pia!!
 
Hapo kwenye red inaonesha umeshagundua chanzo cha kushindwa mara ya kwanza kwa nini usiboreshe uendelee na hiyo biashara maana unauzoefu tayari
 
Hapo kwenye red inaonesha umeshagundua chanzo cha kushindwa mara ya kwanza kwa nini usiboreshe uendelee na hiyo biashara maana unauzoefu tayari

Kweli mkuu,lakini nataka nipate wazo bora zaidi kwani ya mwanzo niliifungua ili inside mambo yangu ya shule na mkate wa Lila siku,hii ya sasa nataka iwendio ya kuendesha maisha yangu na familia pia,kiendesha uchumi wangu!!
 
Nenda Iringa kanunue shamba la mitiki iliyokaribia kukomaa kwa 5m, ambalo lina miti zaidi ya 600 na unasubiri miaka 2 au mmoja ikomae zaidi. Baada ya hapo ukikata hiyo miti na kuchana mbao itakuingizia faida zaidi ya 18m.
 
wazo la biashara unalo ndani ya kichwa chako ila hauliamini, kaa chini fikiria kwa makini utaligundua
kama unataka biashara ya kukupa faida upewe wazo inamaanisha hata usimamizi wa hiyo biashara
utahitaji kupewa mawazo pia. FIKIRIA KWA MAKINI hakuna biashara rahisi na hakuna biashara ngumu
ni moyo na utayari wa kweli.
 
Uko wapi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…