Kama unawazo la kufanya biashara ya uber pia ni vyema ukapitia hapa ujue changamoto na mukihitaji naweza ongelea upande wa pili Advantages ili uweze kujua kabla ya kuamua.
Unaambiwa utamu wa ngoma ingia uone!
Nimekuwa nikisumbuliwa na madereva wangu wa uber kwa kutofikisha hesabu 30,000/=kwa siku na mafuta ni yangu nimemwekea nusu tank siku ya kuanza.
Sikuchukua uamuzi mgumu ikabidi nimsimamishe mmoja ambaye kila siku aishi sababu bahati nzuri nikapata likizo nikaamua nijaribu kujifunza mazingira ya hii biashara kwa madereva. Nimeona yafuatayo
1, Uber calculator inacount pale tu unapofikia mteja so unapotoka kumfata haihesabu ili iingize kwenye nauli na unaweza ukawa upo kinondoni ukapata request ya magomeni sasa piga hesabu utoke kinondoni to magomeni bure alafu mpeleke mtu kutoka magomeni hospital to mwembechai kwa elfu tatu tu.
2, Uber calculator inasitisha kuhesabu malipo pale tu unapomfikisha mteja so kurudi gharam za mafuta ni juu yako na kuna maeneo ukimpeleka mtu hupati wa kurudi naye unaweza ukasubiri hata two hours
3, Foleni za dar; kuna foleni kiasi kwamba japo wanadai nauli is equal to time and lenth spent but tofauti ni ndogo san yani unaweza kutoka posta unaenda Tabata unatumia masaa mawili nauli ni only ten thousands.
4, Nauli wanazotoza; uber wanatoza less than 50% ya tax na wanachoangalia wao eti ni mda tu na umbali bila kukumbuka TRA tunalipa 318,000 kwa mwaka 70,000 Halmashauri, tunafanya service ndogo ndogo kama oil na kubwa kama kubadilisha tyre nk wao hawaoni hili.
5, Asilimia wanazochukua kwa sisi wamiliki wa hivyo vyombo is not fair wao wanakata 25% ya kila safari bila kujua hiyohiyo 75% tunanunua petrol, kufanya service,kulipa fine za barabarani na hapo hapo dereva apate posho yake.
6,Gari kuwa nyingi katika eneo moja kwa mfano utakuta kila dereva anang'ang'ania maeneo kama posta, upanga, masaki na osterbay hivyo kufanya trip kuwa za kubangaiza sana dereva anaweza kaa lisaa hajapata trip hivyo ni ngumu kufikisha hesabu.
7, Gharama za ziada yani unakuta kunagharama ambazo sio calculated kwenye biashara ila lazima dereva akumbane nazo kama kuwa na smartphone yenye uwezo sio kila smartphone inaweza, kuwa na internet bundles all the time na kuwa na charge wakati wowote kwani tangu nianze kutumia play store apps sijaona app inakula charge kama ya uber driver yani mpaka simu inapata moto but hizi gharama hawazioni wao wanang'ang'ana na 25%.
8, Usumbufu wa matatizo ya kimtandao yani siku kukiwa na tatizo la mawasiliano ya simu au internet huwez fanya biashara na kwetu Tz matatizo hayo ni kawaida sana.
Nimeamua yakuwa kama itafika january 2019 Uber watashindwa kutatua kero zetu wamiliki tulizozipeleka natoa gari zangu zote na kuziuza nifanye biashara nyingine na si mimi tu bali hili ni tamko la baadhi wamiliki tuliloliamua.