Maelezo ya namna kuwa retailer wa premier betting changamatoto na faida zake

Luno G

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2012
Posts
2,549
Reaction score
1,849
Baada ya kupitia nyuzi kadhaa humu jamvini nimegundua kwamba wapo baadhi ya wadau wanaotaka kujua baadhi ya mambo kuhusu namna ya kuwa wakala wa premier betting, kwasababu mimi najua baadhi ya mambo kuhusu hii premier betting nimeona wacha nianzishe uzi huu ili kupitia uzi huu watu waweze kupata baadhi ya taarifa juu ya kile walichotaka kujua. Lakini pia kupitia uzi huu watajitokeza baadhi ya wadau wengine wenye taarifa nyengine za ziada kuhusu hawa premier betting ambao nao pia watatueleza ili wote kwa pamoja tuweze kuhabarika.
Baada ya mwanzo huo mfupi nitajaribu kueleza kwa ufupi sana juu ya baadhi ya mambo ambayo wadau wengi wamekuwa na shauku ya kutaka kupata taarifa zake,


UNAWEZAJE KUWA RETAILER WA PREMIER BETTING?


Ili kupata mashine inakupasa uwe na wadhamini wawili ambapo kila mdhamini inabidi ukupe kopi ya kitambulisho cha kupiga kura au leseni au pasi ya kusafiria, lakini pia inabidi akuandikie barua ambayo itajieleza kwamba amekubali kukudhamini, mwisho inabidi kila mdhamini awe na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa.Wewe muombaji pia inabidi uwe na kopi ya kitambulisho kimojawapo kama nilivyoanisha hapo juu, uwe na barua ya kuomba kuwa wakala na mwisho pia uwe na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa.


Ukishakuwa na vitu hivyo vyote mkononi utatakiwa kufikisha pale makao makuu yao karibu ya soko kuu ya kariakoo shimoni nyuma ya ilipo benki ya watu wa zanzibari. Ukipeleka pale watakagua kama vipo sawa kasha kuna fomu watakujazia na kukupa ila wadhamini wako wakasaini kwenye hiyo fomu. Wadhamini wako wakishakamilisha kusaini kwenye hiyo fomu utairudisha kule ofisini kwao ambapo kuna fomu nyengine pia watakujazia na kisha baada ya hapo utaambiwa utapigiwa simu kwaajili ya kwenda kufanya training. Mara nyingi huwa haizidi siku saba hadi kupigiwa simu ili kwenda kufanya training.


Training huwa ni ya siku moja tu ila kuna changamoto kutoka kwa hao wanafundisha hiyo training ukiwa na hasira unaweza jikuta unaondoka siku hiyo hiyo bila ya kumaliza hata hiyo training(ambao wamewahi kufanya training watakuwa wanawafahamu Aisha na Amanda). Baada ya kumaliza training utapangiwa sehemu ya kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo kwa muda wa siku nne ambapo utapaswa kukaa kwa masaa matatu kwa kila siku ndani ya hizo siku nne.


Wakati wa kufanya mafunzo kwa vitendo utapaswa kutoa reports kutoka kwa huyo agent ambaye utapangwa field kwake, report hizo utatakiwa uzipeleke siku ya tano kule HQ na baada ya kuzikabidhi utapewa elfu 20 ya nauli.
Baada ya mchakato wote huo utaambiwa utapigiwa simu mashine yako ikiwa tayari, kiukweli kwasasa inachukua muda mrefu kidogo hadi kuja kupatiwa mashine mfano mimi binafsi ilinichukua miezi miwili hadi kupigiwa simu kwenda kuchukua mashine hivyo uvumilivu unahitajika.


Mashine yako ikiwa tayari utapigiwa simu ili kwenda kuchukua ila siku ya kwenda kuchukua inabidi ukumbuke vizuri juu ya nmana ya kutumia mashine la sivyo unaweza pokonywa mshine hivi hivi(hili lilitaka kunitokea mimi binafsi as sio mtu wa kubet na ilipita muda kidogo tangu tuelekezwe namna ya kutumia hivyo nilisahahu baadhi ya vitu)


JE KUNA GHARAMA ZOZOTE HADI KUIPATA MASHINE?

Tofauti na masuala ya labda Airtel money, Tigo pesa, M pesa, mashine za max malipo nk mashine hizi za kubet za premier betting hutolewa BURE kabisa na wakati unapewa siku ya kwanza unakuta ndani yake inasalio la laki moja hivyo unachouza unatoa kamisheni yako ya 7% na kilichobaki unawatumia. Mfano umeuza 50000 utakata kamisheni yako ya 3500 itabaki 46500 ambayo utapaswa kuwatumia na kwenye mashine itabaki 50000. Kesho yake ukiamka asubuhi utaikuta laki nyengine hivyo ile iliyobaki ya jana itakuwa imeondoka na jana yake.


Unaweza jiuliza je hiyo laki yote ikiisha, itakuaje? Unachotakiwa ni kukata kamisheni yako na kuwatumia 93000 yao kisha utawapigia simu kuwaomba salio jengine ambalo watakutumia baada ya muda mfupi. Hivyo ukimaliza salio ukiwaomba jengine watakutumia na kama hautamaliza basi lile litakalo baki hautalikuta kesho yake na badala yake utaikuta laki nyengine.


JE WAKALA ANANUFAIKAJE?

Wewe kama wakala utapata kamisheni ya 7% ya kile utachokiuza mfano ukiuza mikeka ya 100000 basi unatakiwa kuwatumia 93000 na wewe utabaki na 7000 yako. Lakini pia wewe kama wakala utapata kamisheni ya 1% ya malipo utayofanya kwa wateja walioshinda mikeka yao mfano mtu alibeti na akashinda 34000 akaja kwako kuomba umlipe then ukamlipa basi utapata kamisheni ya 1% ambayo itakuwa ni sawa na 340. Ila kwa sasa mawakala wadogo hawapaswi kulipa pesa kuanzia laki moja kwenda juu.


Kama utapata kijiwe kizuri shughuli hii inalipa sana mfano mimi nilifanya mafunzo kwa vitendo maeneo ya tandika kwa siku nne nilizokaa pale kiwango cha chini alichouza kilikuwa ni laki 8 na ushee na siku aliyouza pesa nyingi kwa siku nilizokaa pale ilikuwa ni 1.3. Sasa chukulia hiyo hiyo laki 8 inamaana alipata kamisheni ya 56000 kwa siku moja.
Lakini pia uzuri mwengine wa shughuli hii ni kwamba ida ya watu wanaojaribu kuacha kubet ni ndogo kuliko idadi ya watu wanaojifunza kubet kila leo hii inamaana uhakika wa watu bado ni mkubwa sana. Siku hizi hadi kina mama watu wazima wanabet,i siku hizi hadi kina dada wanabeti lakini pia, siku hizi hadi watu wazima wenye miaka kuanzia 50 nao wanabeti. Lakini pia kuna hao wanaoitwa majoker watu wanabet hadi laki 1 hivyo nasisitiza tena kwamba suala la wateja si tatizo kubwa sana.


FAIDA ZA KUWA WAKALA

-Kwanza ni kupata kamisheni ya 7% ya mauzo na 1% ya malipo

-Lakini pia biashara hii inaweza ukaichanganya na biashara nyengine mfano genge nk

-Unaweza ukaa hata kibarazani na kisturi chako tu na ukapiga mzigo

CHANGAMOTO ZAKE

-Kuna wakati network husumbua sana hivo kukwamisha shughuli kufanyika

-Kunawakati biashara hii inatabia ya kuua biashara nyengine utakayoichanganya nayo pamoja mfano kama utaweka library ya kukodisha cd na mashine ya betting basi kuna uwezekano mkubwa biashara hiyo ya cd ikafa

-Kuna baadhi ya imani zinadai mchezo huu ni halamu

-Asilimia kubwa ya wateja wake ni vijana hivyo jiandae kuvumilia matusi na baadhi ya vitendo vya kihuni

Na
Kwa Ngoda Premier Betting,
"bashiri na utajirike"
Ahsanteni
 
Vp naskia ndumba zimo sana tu. Kuna jamaa yupo bgruni siku akienda kubet lazima ashinde watu wakamshtukia kumbe anapulizia dah...vipi hiyo haikuathiri wewe kama wakala?
 
Hiyo safi maana akishinda na WAKALA ananufaika na 1% iwapo atalipwa na WAKALA huyo
Vp naskia ndumba zimo sana tu. Kuna jamaa yupo bgruni siku akienda kubet lazima ashinde watu wakamshtukia kumbe anapulizia dah...vipi hiyo haikuathiri wewe kama wakala?
 
Wamenitapel laki 3 yangu sina ham nao washenz awo
 
Habari za humu ndani.
Naona huu uzi ni wa mwaka 2014...
Naomba kujua kama utaratibu bado ni huo huo au vipi?
Nina frem nimeweka mashine za wachina zile za kubahatisha, then nataka kuweka na hizi za Premier betting sasa hizo process mbona jasho[emoji36]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…