Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Naweka hapa chini maelezo ya ziada kuhusu historia ya Khanga za Boimanda kama alivyoniandikia dada yangu Ummie Alley Hamid kutoka Zanzibar.
Katika maelezo yake kanikumbusha mambo ambayo nilikuwa nimeyasahau.
Vazi la khanga lilikuwa vazi muhimu na maarufu kwa mama zetu.
Nakumbuka ilikuwa ikitoka khanga mpya kuna gari linapita mitaani likitangaza
na hiyo khanga imewekwa kama tangazo na mtu akiieleza ile khanga ilivyo na
maneno ambayo yameandikwa kwenye khanga hiyo.
Pamoja na matangazo hayo kuna muziki unapigwa kupitia maspika katika gari
hiyo.
Katika maspika hayo katika miaka ile ya 1950 katikati utamsikia Salum Abdallah
muziki wa Egyptian au Al Watan ukipigwa kutoka gramaphone iliyokuwa ndani ya
gari.
Kuna khanga ambayo nakumbuka imepita mtaani kwetu Kipata na mtangazaji
akawa anayaeleza maneno yaliyoandikwa akisema, ''Mvua ya nyemi nyemi haimkatazi
mgeni kwenda kwake wala mwenyeji kula chake.'':
Msome aliyoniandikia dada yangu Bi. Ummie Alley Hamid hapo chini katika yale
yaliyopungua katika makala yangu:
"Kaka Mohamed Said leo umenifumbulia fumbo ambalo nilikuwa silijuwi la mtu anaeitwa Boimanda.
Nikiwa mdogo nisiozidi miaka 10, hapa Unguja zilitoka kanga jina BOIMANDA KODI KAINGIA BILA YA HODI.
Kanga wakati ule zikinadiwa kwa kupiga upatu, wanawake wakisikia upatu wanakimbilia milangoni kutizama mali gani mpya imetoka.
Kanga za Boimanda zilikuwa na rangi ya manjano, nyeusi na nyeupe.
Kama sikosei zilikuwa design ya msumeno.
Nazikumbuka kwa sababu Mar. Bibi yangu Bi Zuweina Bint Suleiman Almarjeby (Allah yrhamha), alizipenda sana na alizifungisha.
Kufungisha kanga ulikuwa unatowa “arbuni” au “rubuni” (advance) ya kiasi ulichonacho kama pesa 4 (senti kumi) au zaidi.
Mpiga upatu anakupa risiti na kisha unakwenda kulipa kidogo kidogo Mtendeni kwa “Miwani Mkubwa” au “Miwani Mdogo” hadi utimize shilingi 2 bei ya doti ya Kanga kisha unakwenda kuchukua mvao wako.
Wanawake wengi walishindwa kumaliza malipo na “vijisenti” vyao viliishia “arijojo” kuwanufaisha mabepari wafanya biashara.
Mar. Bibi nilimuuliza nani Boimanda? Akanambia ni Mwendawazimu wa Dar es salaam anaingia nyumba yoyote ile bila ya hodi pindipo akisikia neno “kodi”.
Kwa kweli sikuelewa vizuri na utoto wangu lakini hadi leo nakumbuka kanga za BOIMANDA KODI KAINGIA BILA YA HODI.
Ahsante sana Sh. Mohamed kwa historia hii ambayo imenigusa na kunikumbusha mambo ambayo sikuyaona ila nimeyasikia na leo nikiwa nishaingia uzeeni ndio napata utango na usuli wake.
Allah amrehemu Bibi yangu na Boimanda na wote uliowataja waliotangulia mbeke ya haki. Na wewe JAZAKA LLAHU L KHAIR."