Maelfu waandamana Marekani kupinga utawala wa Trump katika maandamano ya “No Kings”

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Oktoba 18 na 19, 2025, maelfu ya wakazi wa jimbo la Illinois, New York, Washington DC, Chicago, Miami na Los Angeles, Boston wamejitokeza mitaani kushiriki maandamano ya “No Kings” yanayofanyika kote Marekani na duniani. Maandamano haya ni sehemu ya harakati kubwa ya kupinga kile kinachoitwa utawala wa kiimla wa Rais wa zamani Donald Trump.


Your browser is not able to display this video.

Awali, maandamano haya yaliandaliwa sambamba na gwaride la kijeshi lililofanyika mjini Washington kuadhimisha miaka 250 ya Jeshi la Marekani, likiambatana na siku ya kuzaliwa ya Trump. Mnamo Juni 14, maelfu ya waandamanaji walijitokeza katika majimbo mbalimbali nchini Marekani kupinga kile walichokiita “jaribio la Trump kujitwalia madaraka kama mfalme.”

Taarifa kwenye tovuti rasmi ya waandaaji inasomeka:


Katika jiji la Chicago, maandamano haya yanafuatia jaribio la Trump kutuma Jeshi la Taifa (National Guard) huko Illinois, ambalo lilikatizwa na mahakama ya shirikisho na uamuzi huo kuthibitishwa tena na mahakama ya rufaa.



Katika jiji la Boston, maelfu walikusanyika kwenye Boston Common kushiriki maandamano hayo, ambapo Meya wa mji huo Michelle Wu alishiriki pamoja na wanasiasa, wanamuziki na wanaharakati waliwahutubia wananchi, wakilaani sera za Ikulu ya Trump kuhusu uhamiaji, ufadhili wa tafiti na utofauti katika sehemu za kazi

​


Wakati huo huo, maafisa wa uhamiaji (ICE) wameendelea kufanya msako katika jiji na vitongoji vyake, ambapo kwa mujibu wa Idara ya Usalama wa Ndani (DHS), watu zaidi ya 1,500 wamekamatwa kupitia oparesheni iitwayo Operation Midway Blitz. Hata hivyo, ni watu 10 pekee kati yao waliotambuliwa kuwa na rekodi za makosa ya jinai ya vurugu.

Kwanini yanaitwa “No Kings”?​

Kaulimbiu ya “No Kings” imebuniwa na 50501 Movement, harakati ya kitaifa inayopigania demokrasia na kupinga kile wanachokiita mwenendo wa kiimla wa utawala wa Trump.

Jina 50501 linamaanisha majimbo 50, maandamano 50, harakati moja.

Maandamano ya awali mwaka huu yamekuwa yakimlenga Trump na Elon Musk, aliyekuwa mshauri wake katika idara mpya ya Government Efficiency Department, iliyoundwa kupunguza matumizi ya serikali. Waandamanaji wamekuwa wakimtaka Trump “kuondolewa madarakani,” wakimlinganisha na mfalme badala ya rais aliyechaguliwa kidemokrasia.

Kwanini wanandamana?​

Kitaifa, maandamano ya “No Kings” yamepangwa kupinga siasa za kiimla, upendeleo kwa mabilionea, na uongezaji wa nguvu za kijeshi katika utawala wa nchi.

Huko Illinois, waandaaji wanasema lengo lao ni kupinga mateso na unyanyasaji dhidi ya majirani, watoto na familia wanaolengwa katika misako ya wahamiaji.

Katika tamko lao, wameelezea tukio la uvamizi wa ICE katika jengo la makazi lililoko South Shore, ambapo maafisa wa serikali waliwakamata wakazi kadhaa – raia na wasio raia – wakiwemo watoto, baada ya kuwafunga kwa kamba mikononi.

======= For English Audience ======​
Huge crowds have taken part in "No Kings" protests against President Donald Trump's policies in cities across the US, including New York, Washington DC, Chicago, Miami and Los Angeles.

Thousands packed New York City's iconic Times Square and streets all around, with people holding signs with slogans like "Democracy not Monarchy" and "The Constitution is not optional".

Ahead of the demonstrations, Trump allies accused the protesters of being linked with the far-left Antifa movement, and condemned what they called "the-hate America rally". Several US states had mobilised the National Guard. But organizers said the events, which drew nearly seven million people, were peaceful.

In New York, sections of the crowd regularly erupted into chants of "This is what democracy looks like" as a near-constant drumbeat boomed in the background.

Helicopters and drones could be seen flying overhead, and police stood on the sidelines. The New York Police Department said more than 100,000 people had gathered across all five of the city's boroughs, and that no protest-related arrests were made.

In Times Square, a police officer standing by estimated that over 20,000 were marching down 7th Avenue.

SOURCE: BBC & The Havard Crimson
 

Attachments

  • 📍Chicago.mp4
    15.8 MB
Leo ndo nimetambua Wamarekani ni wapumbavu, kama mwanzo walimtoa madarakani walimludisha aje kufanya nini tena, wakamfanyia figisu Joel Bendeqa aonekane ni mzee dishi limeanza kuyumba hataweza kuwaongoza, na hata Camera aliye kaimu nafasi yake mkamkataa leo yamewafika mmeanza kutoa milio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…