SoC02 Maendeleo halisi ni yapi?

Stories of Change - 2022 Competition

Stella medrinah

New Member
Joined
Sep 15, 2022
Posts
1
Reaction score
1
MAANA YA MAENDELEO HALISI
Maendeleo ni uboreshaji wa maisha kutoka hali ya chini kwenda hali juu kiuchumi, kijamii, kiteknolojia nk. Katika ngazi ya kitaifa inaweza kupimwa kwa maendeleo ya uchumi wa taifa lakini katika ngazi ya mtu binafsi inapimwa kwa viwango vya maisha, upatikanaji wa huduma za kijamii na mahitaji ya kimsingi. Maendeleo ya mtu binafsi yanachochea maendeleo ya taifa lakini je, maendeleo ya taifa yanachochea maendeleo ya mtu binafsi (raia)? Je maendeleo ya nchi yanletwa au kupelekea maendeleo ya watu ndani ya taifa hilo? Haya ni maswali ambayo tunapaswa kujiuliza kwa vile watu wengi wanachukulia maendeleo ya taifa kuwa ni mafanikio makubwa hata pale ambapo hali ya maisha ya watu ni duni.

Hili limeonekana katika sekta nyingi ikiwemo elimu ambapo kuna shule nyingi na elimu bila malipo katika shule za umma lakini bado wanafunzi hawawezi kupata elimu bora, kama vile madarasa ya kutosha, walimu na vifaa vya kufundishia. Elimu bure ni nzuri kwani kila mtu anaimudu lakini je ni kweli inakidhi mahitaji ya mwanafunzi na baada ya kumaliza inamhakikishia ajira yake? ukweli ni hapana, watu wengi hawana ajira licha ya elimu waliyonayo na ukosefu wa maafisa katika sekta nyingi pia, hivi mfumo wetu wa elimu unalenga kuwaelimisha watu tu au ni kuwaelimisha na kuwafanya wapate kitu kutoka katika elimu hiyo na hivyo kuboresha maisha yao.

Huduma za afya, serikali imejenga hospitali nyingi na sasa hivi wananchi wanapata hospitali hata vijijini lakini wahudumu wa afya na dawa je vi au gharama zake mwanchi anazimudu? na kwa nini kuna ukosefu wa wahudumu wa afya ilhali kuna wasomi wengi wa vitengo hivyo wasio na ajira na kuna gani la kuelimisha watu na kutengeneza taaluma wakati hawawezi kuajiriwa? Serikali inapaswa kuliangalia hili, vifaa mahispitali viongezwe ili kuboresha huduma na pia wataalamu wa matumizi sahihi ya vifaa hivyo pia waongezwe katika hispitali zetu.

Utalii, hii ni sekta ambayo inaipa serikali mapato yake mengi kwani watalii kutoka kote ulimwenguni kutembelea nchi yetu ili kugundua vivutio tofauti kama vile mbuga za wanyama, milima, makumbusho na zingine nyingi. Hebu tujiulize kwamba kati ya wazawa au wageni, nani ana uwezekano mkubwa wa kutembelea hifadhi zetu za taifa? Ni wazi kwamba ni wageni ndio huja kwa wingi kuliko wazawa, na inasikitisha sana kuona kwamba wenyeji hawana uwezo wa kutembelea maeneo katika nchi yao lakini wageni wanaweza.

Ni watanzania wachache sana ambao wameweza kufika hifadhi ya Serengeti kulinganisha na wageni au mlima Kilimanjaro na vivutio vinginevyo. Je haya ni maendeleo ya kweli, maendeleo ya nchi au maendeleo ya mwananchi. Kuna miundombinu mingi na mifumo ya usafiri ambayo wananchi wengi hawawezi kumudu kama vile safari za ndege na treni na bado tunaita maendeleo haya.

Kuna sekta nyingi sana zinazochangia pato la taifa letu lakini ni nadra kufikiwa na wananchi. Maendeleo ya taifa yanapaswa kuwa mnufaika kwa wananchi wa taifa husika vinginevyo si maendeleo kweli. Serikali ijaribu kuzingatia maisha ya wananchi wengi wao wakiwa vijijini kabla ya kupanua na kuendeleza maeneo ambayo tayari kwa namna fulani yameboreka katika viwango ili taifa likue kwa ujumla na siyo baadhi ya maeneo. Baadhi ya sekta zimekwenda vizuri kama vile usambazaji wa umeme na barabara katika maeneo ya vijijini lakini upatikanaji wa maji bado ni tatizo katika maeneo mengi. Maendeleo yaanzie katika kiwango cha chini, mahitaji ya msingi na huduma za kijamii ziwe kipaumbele cha kwanza tunapozungumzia maendeleo ndipo sekta nyingine zifuate.

Baadhi ya wananchi wanaishi maisha duni sana na badala ya kuboresha maisha yao, hali inazidi kuwa ngumu kwao kwa mfano wauzaji wadogo (machinga) serikali imewatengenezea masoko maalum na ya kudumu lakini je inawasaidia kweli, wanunuzi wanaishi karibu na masoko hayo na vipi kuhusu usafiri na kodi? Wauzaji wengi wanafahamu wapi wataweza kupata wateja, unapomjengea muuzaji huyu soko la kudumu yaweza kumfanya akapoteza wateja wake wa mahali alipozoea na hivyo kumletea hasara. Jambo hili ni hatua kubwa kwa nchi yetu lakini kwa baadhi ya wauzaji imezidi kuwaumiza kuliko kuwaendeleza. Aina hii ya maendeleo ni kwa imejikita zaidi kwa ngazi ya taifa na serikali lakini kwa mtu mmoja mmoja, imechangia kwa asilimia ndogo.

Haki za binadamu, je haki za binadamu zinafatwa na je zinapovunjwa kuna lolote linafanyika kusidia na je wanaovunja haki za binadamu ni kwasababu hawajui sheria au ni makusudi. Mfano mzuri ni wafungwa na washtakiwa, wengi hawatendewi haki wanapigwa na kuteseka magerezani na askari waanofanya hivi sio kwamba hawaijui sheria ama haki za wafungwa hao. Washtakiwa wengi pia wanakaa mahabusu mdarefu mpaka kuja kuskilizwa kesi na wanakua wakiteseka mahabusu kitu ambacho kiubinadamu sio haki kabisa.

Serikali iwatazame watu hawa pia kwani kua mfungwa tayari ni adhabu ambayo mtu anatumikia kwahiyo mateso, ukatili na kupigwa sio sehemu ya adhabu. Pia ofisi nyingine za kutoa huduma kwa wananchi zimekua zikikiuka haki za bunadamu kwa kuomba rushwa jambo lililopelekea wananchi kukosa imani au kuumizwa pia na si magerezani tu na maogisini bali hata mashuleni na sehwmu nyingine nyingi kwahiyo elimu itolewe kuhusu haki za binadamu na rushwa na pia hatua zichukuliwe ili kuweza kumlinda mwananchi.

Serikali imejitahidi sana kuboresha taifa letu na kufikia hapa ulipo uchumi wetu, ni hatua kubwa sana lakini inapaswa kuangalia zaidi maisha ya mwananchi kwanza na kwa hivyo watu wote wataishi maisha ya kawaida yanayokidhi mahitaji ya msingi na hakutakuwapo pengo kubwa kati ya wananchi matajiri na maskini. Hapo tutafikia maana halisi ya maendeleo.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…