SoC04 Maendeleo katika taifa huja kwa mipango ya muda mrefu na utekelezaji

SoC04 Maendeleo katika taifa huja kwa mipango ya muda mrefu na utekelezaji

Tanzania Tuitakayo competition threads

Balunyu95

Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
23
Reaction score
21
Baada ya miongo kadhaa kupitia nchi ya KIMANILWE NTEMI, ilipitia misukosuko mingi, ikiwemo rushwa, uchu wa madaraka. Hali hiyo ilisababisha nchi kukosa mwelekeo kwasababu Kila mtawala aliyekuwa anaingia sio kwajili ya kulisaidia taifa liende mbele bali kwa manufaa binafisi na kujilimbikizia Mali za umma, hayo yote ni kutokana na mifumo mibovu iliyokuwa imewekwa katika nchi hiyo

Hali hiyo ilipelekea kuathiri hasa katika upande wa elimu ya sayansi na tekinolojia kutokana na uwepo wa mitaala isiyoeleweka, kwa mfano shule za msingi katika somo la sayansi wanafunzi walikuwa wakifundishwa mada zinazohusiana na komputa kwa maelezo tu lakini unakuta watoto hata hawaijui komputa ilivyo wala ndo kitu Gani hasa maeneo ya vijijini.

Ilipelekea pia changamoto ikasababisha ukosefu wa wabunifu, hii yote ilipelekea na uwepo wa mipango mibovu na kutokuwa na kipaumbele na mikakati, hali hiyo iliathiri sana maendeleo ya nchi kwa ujumla hata katika utekelezaji wa miundo mbinu

Baada ya muda alipatikana kiongozi mzaleondo aliyekuwa ana machungu na maendeleo ya nchi yake, Wala rushwa walimchukia sana kwa maslah binafisi lakini nchi ilianza kuona matunda yake na mabadiliko yakaanza kutokea.

Aliweka kipaumbele katika kila sekta hali iliyopelekea kila mtumishi kuwajibika, mashuleni wakapatiwa vifaa vya kujifunzia kama komputa na vinginevyo hali iliyopelekea kupatikana kwa wataalamu wengi katika fani tofauti tofauti. Viwanda vikajengwa na uzalishaji wa vitu tofauti tofauti ukaanza nchi ikawa tegemeo na mataifa mengine.

Hitimisho ili nchi iendelee inahitaji kuwepo na mipango ya mdarefu hasa katika mabadiliko ya elimu, sio kila kiongozi anayeingia anakuja na maoni yake. Pia uwajibishwaji kwa wala rushwa unatakiwa kupewa kipaumbele, na pia vyombo vya ulinzi viingilie kati anapotokea kiongozi asiyekuwa na mwelekeo yupo kwajili ya masrahi binafisi na viongozi wake hali hii itasaidia kwa Tanzania kuendelea katika nyanja mbalimbali kwa miaka kumi ijayo
 
Upvote 5
Kila mtawala aliyekuwa anaingia sio kwajili ya kulisaidia taifa liende mbele bali kwa manufaa binafisi
Havitoani, kila siku. Mtu anaweza kabisa kulijenga taifa na kutimiza pia matakwa yake binafsi. Maslahi. Haki inataka nchi ipate, mwananchi apate na kiongozo naye apate. Win win win.

Hitimisho ili nchi iendelee inahitaji kuwepo na mipango ya mdarefu hasa katika mabadiliko ya elimu, sio kila kiongozi anayeingia anakuja na maoni yake
Hakika, yawepo maono ya nchi kama nchi na kila kiongozi anayafanyia kazi. Ajenda ni ya ki taifa
 
Back
Top Bottom