Binafsi napongeza sana mjadala huu.
Niseme tu kwamba watanzania tulishatiwa umaskini mkubwa kifikra. Tumeminywa kiasi kwamba hivi sasa mtu si tu kwamba hawezi kusema ila hawezi hata kusema kwamba hawezi kusema.
Watanzania tunaendeshwa na genge la watu tu. Hatuwezi kujiamulia tuongozwe na nani, kwa mfumo gani na kwanini? Mafisadi ndo wanaamua nani awe rais muhula huu na atafuatia nani. Unadhani wanaweza wakatumia pesa zao kupanga safu kwa manufaa yako? Never!
Ndio maana viongozi hawa wakishaingia madarakani hawamsikilizi mwananchi hata kidogo. Na wana haki ya kufanya hivyo. Si wanamsikiliza aliyeaingiza madarakani! Hii si ndo kawaida, uongo jamani?
Tatizo lilipofikia sasa, ni kwamba sisi hao hao ambao kesho tutakufa na watoto wetu wataangamia, ndo tunakubali kuolewa na mafisadi na kuuza utu wetu, namaanisha uhuru wetu, mamlaka yetu, haki yetu, vyote tunawapa kwa vijipesa uchwara tu. Tunajisaliti wenyewe, tunasaliti familia zetu, tunamsaliti hata muumba wetu. Mbaya zaidi, hao hao mafisadi, wanatugawa kwa propaganda za maslahi yao, wanapandikiza chuki za kidini, kikabila, kikanda, kichama...! Jamani, watanzania tuamke, inatia hasira. Kuna wat wengine wenye rohi nyepesi na uzalendo hafifu wanaweza wakaamua kutafuta nchi nyingine na kuomba uraia huko kujihifadhi inhawa huu si uungwana, lakini watafanyaje na washauzwa?
Hivi jamani, kweli mtu aje amechafuka tope mwili mzima unanuka na watu wanamfukuza aende akaoge halafu anakuja kwako anakuambia "wananifukuza kwa vile mimi ni mpagani", ni lazima ukubali na usahau machungu ya nchi yako na badala yake uanze kupigana na jirani yako kwamba wapagani tunapigwa vita? Na wewe unayetaka kutumia ngao hii dhaifu kabisa huoni kweli kwamba unalipua bomu la skadi? Una akili kweli wewe? Hauna hata porojo zingine nafuu kidogo kwa taifa na watanzanaia?
Oh, God help me...!
Nawaomba ndugu zangu tuwe kitu kimoja. Tanzania inayoporwa ni moja, sote tumo humuhumu na tunauzwa huku tunaona. Fisadi hana dini, hana huruma wala upendo, japokuwa anaweza kuwa na jina la dini na hata kabila. Leo atajifanya ni rafiki yako ili afanikiwe mambo yake lakini madhara yake utayapata.
Let us fight as one. Tuvunje ukimya, tuna haki ya kuamua tunataka Muuungano wa namna gani, Rais mwenye mamlaka yenye mipaka ipi, tasisi huru zinazoteuliwa kwa uwazi na haki na kwa kumshirikisha vipi mwananchi, mfumo wa serikali upo, serikali yenye wajibu upi kwa wananchi na wananchi wanaweza kuiwajibisha vipi inaposhindwa kutimiza wajibu, jeshi la polisi lenye uwezo upi na wajibu upi, rasilimali zigawanywe vipi baina ya watanzania na hasa katika kutoa elimu na huduma muhimu za jamii. Kubwa kabisa, TUNAWABANA VIPI WATAWALA WATEKELEZE YALE YOTE TUTAKAYOYAWEKA KATIKA HIYO KATIBA MPYA!.
Asanteni wana JF kwa fursa.