Hivi kwanini tusi washawishi Watanzania tuungane Tanzania Nzima Kudai Katiba mpya?
Tuungane kuidai Katiba mpya
Silver25;
Hiyo kazi ya kushawishi Watanzania kuungana Tanzania nzima kwa sasa inafanywa na UKAWA(Umoja wa Katiba ya Wananchi). Kinachotakiwa kwa sasa ni kuwaunga mkono UKAWA ambao wameamua kutoka nje ya BMK ili kwenda kuwahamasisha Watanzania kuungana na kupinga udhalimu na ubeberu wa CCM wa kulazimisha Katiba ilingane na matakwa yao yaani SERIKALI 2!
Bado kuna changa moto nyingi sana kuja kuipata Katiba mpya hatimaye Tanzania kwenda kuwa na Uchaguzi Huru na Haki ambao utawapa Watanzania utawala wanaoutaka wao na si kama sasa kuwa kila Uchaguzi ni CCM! Watanzania lazima tujue kuwa KUPIGA KURA ni haki ya Kikatiba ya kila Mtanzania aliye na umri wa MIAKA 18 na kuendelea. Tunataka KATIBA ambayo itatupatia TUME HURU(NEC) YA UCHAGUZI itakayosimamia Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa haki bila upendeleo wala shinikizo lolote toka CCM na Serikali yake kama ilivo sasa.
Tunajua kutokana na Madaraka makubwa aliyo nayo Rais wa CCM amekuwa ndiye anayemteua Mwenyekiti wa TUME YA UCHAGUZI na Wasaidizi wake. Tunajua kuwa Wakurugenzi wa MAJIJI na HALMASHAURI ndiye wanaosimamia Chaguzi zote Kubwa na Ndogo na wote hawa ni Wateule wa Rais wa CCM! Katika mazingira kama haya,hivi Watanzania tunategemea kuja kuiondosha CCM madarakani kweli?? Jibu ni NEVER! Mwenyekiti wa TUME na Wakurugenzi wa Miji na Majiji hawawezi kuruhusu CCM ishindwe hata mara moja! Watachezea matokeo tu ili kuinusuru CCM.
Tunajua DAFTARI LA WAPIGA KURA halijaboreshwa tangu mwaka 2010 kwa maksudi mazima. CCM wanajua kizazi cha Vijana waliokuwa na umri wa miaka kuanzia 13 mpaka 17 mwaka 2010 kwa sasa wana HAKI YA KUPIGA KURA lakini CCM na NEC(Tume ya Uchaguzi) wamenyamaza kimya. Wanajua idadi ya Vijana hawa inaweza kuwa sawa na idadi ya KURA alizopata Rais wa CCM Bwana Kiwete mwaka 2010 ambazo zilikuwa ni kama 5m+. CCM wanajua vijana wanataka mabadiliko wameshachoka na vizee na vibabu vya CCM wanataka vijana wenzao walioko Vyama vingine vya Siasa nje ya CCM kushika Madaraka.
Juzi tumesikia kwenye media mapema mwaka huu kuwa NEC wamepewa Dola milioni 200+ kwa ajili ya KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA lakini mpaka sasa si NEC wala SERIKALI ya CCM wanashughulikia uboreshaji huo. Wamenyamaza kimya kwa makusdi. Wanataka mpaka Uchaguzi wa Serikali za MITAA na Uchaguzi Mkuu ukikaribia ndiyo waanze porojo na longolongo za kuanza kuboresha daftari, lakini ukweli ni kwamba CCM hawana mpango huo kwa sababu wanatka kubakiza idadi ileile waliyoipata mwaka 2010 iendelee kuwepo ili waje kujidai wameshinda kwa kishindo!
Mimi nawaomba UKAWA wanapopita kuelimisha Watanzania kuhusu Katiba Mpya lazima wazungumzie mambo matatu muhimu sana. Kwanza ni UMUHIMU WA KUWA NA TUME HURU YA UCHAGUZI kwenye Katiba tunayoipigania. Pili ni UMUHIMU wa KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA na tatu na mwisho ni UMUHIMU WA KILA MWANANCHI KWENDA KUPIGA KURA SIKU YA UCHAGUZI. Hii itawaamusha Wananchi na itasaidia mbele ya Safari tunapoelekea kwenye Chaguzi hizi muhimu.
Nimalize kwa kuwakumbusha Watanzania kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Kwamba tulijiandikisha Watu zaidi ya milioni 20 kulingana na hesabu za Tume ya Uchaguzi-NEC kama si za kuchakachua. Lakini siku ya Uchaguzi ni watu Milioni 8 tu walijitokeza kupiga kura hii ikiwa ni asilimia 40(40%) ya Watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura. Rais wa CCM Bwana Kiwete alipata kura 5m+ zilizompa Urahisi(siyo Urais) na hii ni sawa na asilimia 25(25%)ya Watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura!!Hii maana yake nini. Kwamba Rais wa CCM yuko Madarakani kwa Kura 25% ya Watanzania waliojiandikisha kupiga kura kwa maana hiyo 75% hawakuitaka CCM iingie madarakani.Hii ni kasoro kubwa lazima iangaliwe na kurekibishwa tunapoelekea kwenye Katiba Mpya na Chaguzi kuu zijazo.
Kuna haja pia ya kuangalia uwezekano wa kutunga sheria kwa Wapiga kura ambayo itambana KILA MPIGA KURA ALIYEJIANDIKISHA kwenda kupiga kura. Kwamba swala la KUJIANDIKISHA NA KUPIGA KURA IWE NI LAZIMA siyo hiari na siku ya kupiga kura atakayekosa kupiga kura kuwe na adhabu iliyo wazi yenye kuainisha adhabu ya kuwaadhibu waliokwepa kupiga kura. Serikali na Tume zinatumia mabilioni kuandikisha wapiga kura halafu mtu anajiandikisha na anaingia mitini. Hii haikubaliki. Tunajua pengine kuna Watanzania wamesha kata tamaa kuwa hata ukienda kupiga kura ukachagua chama tofauti na CCM haitaleta mabadiliko kwa vile CCM lazima watachakachua na kuchukua ushindi. Hii ni kutokana na kama nilivoeleza hapo juu kuwa madhali Rais wa CCM ndiye anayeteua Wakuu wa NEC na Wasimamizi wa Chaguzi zote hilo lazima litokee. Lakini kama hili litadhibitiwa kwenye Katiba Mpya kwa kumwondolea Rais madaraka ya kuteua utitiri wa Viongozi hawa ambao wengi ni Makada wa CCM tatizo la Uchakachuaji litakuwa ni historia!
''UKAWA JUU, JUU, JUU ZAIDI,MSHIKAMANO DAIMA KUTENGANA AU KURUDI NYUMA MWIKO!''