SoC01 Maendeleo ya biashara yako yanategemea tabia zako ulizonazo, hali halisi, na ujuzi uliokua nao

Stories of Change - 2021 Competition

Kitumba_

Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
30
Reaction score
21
Mara nyingi tukiwa tunatizamia kufanya biashara fulani ama jambo fulani, huwa tukijikuta tunakwama kwenye situations ambazo ama pengine tunafikiri hatuko vizuri bado, nimekwama sina mtaji, pengine kuna mtu anakuchezea unafikia kusema au siajakaa vizuri bado. Kuna michakato haswa ambayo lazima iwepo ili kukuza biashara yako. Makala hii itakuwezesha kupangilia mawazo na mafikirio uliyonayo kuhusu shughuli haswa unayohitaji kuianzisha. Utaweza kuamua kama kweli unahitaji kukua katika biashara hiyo au la. Kama utaamua kukua hilo litakua wazo jema, utaweza kupata muongozo wa namna ya kuanza na hivyo kukua.

Iko hivi wewe unawajibika moja kwa moja kwa kuiongoza na kuiendeleza biashara husika. Huu wajibu una maana ya presha kubwa, lakini pia uhuru wa kutosha. Kuanzisha shughuli yako binafsi ni hatua kubwa na itabadili maisha yako. Inamaanisha kujituma na kufanya kazi kwa muda mrefu, lakini inaweza kuwa yenye kukuridhisha na kukunufaisha.

Maendeleo ya biashara yako yanategemea tabia zako ulizonazo, hali halisi, na ujuzi uliokua nao. kiasi cha ujasiliamali ulichonacho na ujuzi ulionao, ndipo uwezekano wa shughuli yako kuendelea. Sifa za kijasiliamali na ujuzi unaouhitaji utategemea aina ya biashara unayoamua kuianzisha. Familia yako na hali yako kifedha pia ni vitu muhimu vya kuzingatia kabla hujaianzisha biashara husika. Zaidi na pengine ulivyodhania, Unazo baadhi ya sifa muhimu na ujuzi stahiki.

Kama utakosa ujuzi fulani unaweza kujiendeleza kupitia mafunzo, semina au kwa kujisomea. Kikubwa uweze kutambua ni sifa zipi unazikosa hivyo kuhitaji kujiongeza na kubadili mtizamo wako na tabia husika. Unaweza kufanyia kazi hali yako kifedha na kifamilia kuvifanya vyote viwe murua kwa wewe kuiendesha biashara yako.

Angalia vipimo vifuatavyo, vitasaidia kutambua yote ni wapi haswa unahitaji kuuendeleza na mafunzo yapi au msaada upi utauhitaji. Kuwa wazi kipindi unajipambanua.

Mosi, Ujuzi wa kiufundi. Ule uwezo kiutendaji unaouhitaji kuzalisha bidhaa fulani au kutoa huduma kwa minajili ya biashara yako kwa usahihi mkubwa. Kwa mfano, kukua katika biashara ya gereji utahitaji kujua namna ya kurekebisha gari, pikipiki. Ukihitaji kujishughulisha na ufundi seremala itakuhitaji uwe na uwezo wa kuranda mbao na kutengeneza samani. Kama mtu huna ujuzi husika, iweke hii iwe ni mapungufu na kuifanyia kazi mara moja. Fikilia ni kivipi utapata ujuzi husika, labda kwa kuajiri mfanyakazi mwenye ujuzi huo, kwa kutafuta mtu mwenye ujuzi husika mkaanzisha pamoja kitu hiko (patnership), au kupata mafunzo hayo.

Pili, Ujuzi wa Uongozaji Biashara, kitaalamu business administration.
Huu ni uwezo ulionao wa kuiendesha shughuli yako vyema. Kuyatambua masoko, ni mojawapo muhimu sana ndani ya ujuzi huu lakini maeneo mengine ya uongozaji biashara nayo pia ni muhimu kwa maendeleo ya shughuli yako, kwa mfano gharama na utaunzaji rekodi. Kama hujui kuongoza biashara, unaweza kujifunza kupitia vitabu vinavyoelezea jinsi ya kuoongoza biashara. Mfano ukajifunza maeneo sita muhimu kwenye kuongoza biashara yeyote; Masoko, Ununuzi bidhaa, Udhibiti wa hisa (Stock) ulizonazo, Gharama, Utunzaji kumbukumbu, na mipango.

Tatu, Kutambua Watu wanaofanya kitu kama Chako. Hii ni muhimu na yakuzingatiwa kwa biashara yako kukua. Ujuzi wa kuwasoma watu wanaofanya shughuli kama yako ni muhimu. Kwa kiasi unavyowatambua ni vyema. Kama una huu ujuzi utaweza kuepuka kufanya makosa. Utalitambua vyema soko, washindani na wasambazaji. Kama unaona hujui kucheza na watu wanao fanya shughuli kama yako, unaweza kuangalia namna ya kupata mtu mkashirikiana katika biashara.

Nne, Kujitoa. Kufanikiwa katika biashara unatakiwa kujitoa. Kujitoa kunamaanisha ya kwamba unahitaji kuweka shughuli yako mbele kabla ya kila kitu kingine. Inamaanisha ya kwamba unahitaji kukaa katika shughuli kwa muda mrefu na hivyo unahitaji kughalamia hela yako katika biashara.

Kingine, Kuwa na motisha. Kwa nini umepanga kuanzisha biashara yako binafsi? biashara yako hufanikiwa zaidi ikiwa unashauku ya kujaribu mawazo yako, unatakiwa kuwa bosi wako na unatakiwa kuwa na biashara yako binafsi. Ikiwa umepanga kuanzisha biashara kwasababu tu unahitaji hivyo, kwa mfano ikiwa unahitaji kuanzisha shughuli kwasababu tu unahitaji hivyo, kwa mfano ikiwa haujaajiriwa, nafasi yako ya kufanikiwa kwa ujumla si mazuri.

Tano, Uwezo wa Kuchukua Hatari, wengine wanaita ku-take risks. Hakuna usalama wa moja kwa moja kwenye biashara yeyote. Muda wote unaenda na tahadhari ya kuanguka katika biashara yako. Ingawa mjasiriamali lazima awe radhi kuchukua hatari, lakini lazima ufanye yale yenye sababu zenye mashiko. Kuchukua hatari kubwa ni kamari au kutoweza kuchukua hatari kabisa ni Mapungufu.

Sita, Kufanya maamuzi. Kwenye biashara unayoimiliki, lazima ufanye maamuzi muhimu. Haihitajiki yapite kwa mtu mwengine au kutoyafanyia kazi. Kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu ambayo yanaweza kuwa na matokeo makubwa ni muhimu katika kuiendesha biashara yako.

Saba, Hali Halisi kifamilia. Kuiendesha shughuli yako itachukua muda wako wa kutosha. Ni vyema kuwa na sapoti kifamilia. Familia yako lazima ikubaliane na mipango ya kuanzisha biashara hiyo. Pengine wanaweza hata kuhusishwa na kusaidia. Ukiwa na familia inayokusapoti hapo vyema; kama huna sapoti yeyote kutoka katika familia yako hayo ni Mapungufu.

Wajasiliamali wengi hawana ujuzi wa kutosha, au sifa zote muhimu au hawakua na hali stahiki kipindi ambako wanaanzisha biashara zao. Lakini ujuzi unaweza kujifunza, sifa zingine ukajiendeleza na hali iliyopo ukaiimarisha. Unaweza kufanyia kazi mapungufu yako na kuyageuza kuwa vyema.

Njia Zifuatazo zinaweza kutizamwa: Tafuta Msaada Kutoka kwa Wengine. Ongea kuhusu shughuli yako na rafiki, familia, watu wenye kujishughulisha,…nk, Tizama Mifano ya Waliofanikiwa. Fikiria kuhusu yapi walifanya na kivipi ilisaidia mpaka shughulia zao ziimalike. Hudhuria Mafunzo Mbalimbali. Tafuta mafunzo kwa eneo unaloona lina mapungufu. Kwamfano unaweza kujifunza jinsi ya kutunza rekodi na fedha.

Soma Vitabu. Tafuta vitabu kuhusu maeneo ambayo unahitajika kuyajenga (yenye mapungufu).

Hiyo ni baadhi tu michakato ya msingi katika kuikuza biashara yako.
 
Upvote 2

Mkuu umemaliza chuo mwka gan nimependa aina ya uandish wako
 
2019 mkuu
 
Back
Top Bottom