Princesswaprince
Member
- Sep 9, 2022
- 5
- 3
Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.
Ningependa Tanzania niitakayo kupitia
wizara hii ikajitathmini na kufanya maboresho katika maeneo kadhaa kutoka katika sera zake kwa mfano wazee, hawa wamekuwa hawaangaliwi ipasavyo hii ndio maana wazee wengi hali yao kiuchumi hata kiafya imekuwa changamoto ni muda sasa wa kuwawezesha kiuchumi kundi hili maalum la wazee kwani wao ndio mizizi ya misingi ya familia yoyote ile.
Kundi la wanawake hapa pia kutengenezwe mikakati kweli ya kumuinua mwanamke. Asilimia kubwa ya wanawake ndio wanaonekana barabarani wakipambana kujitafutia kipato,hili pia ni kundi linalohitaji uangalizi na usaidizi kama vile kupunguza baadhi ya masharti ya kupata mikopo kupitia ofisi za serikali ya mtaa husika kwani misingi bora kutoka kwa wazee inasimamiwa na kutekelezwa na kundi hili. Kushindwa kuwawezesha wanawake ndipo ongezeko la neno linalotamba kipindi hiki "vitoto vya 2000" linapozidi kumea.
Hawa watoto wamekosa usimamizi wa misingi bora ya malezi kati ya kwa mama ambaye yuko busy barabarani kutafuta tonge, babu naye ambaye amesharaulika na kutokuwa na thamani tena lakini pia baba ambaye alikimbia mimba. Ikumbukwe tu kuna kizazi kitatokea baada ya hiki swali ni je Tanzania yetu itakuwa na kizazi cha aina gani miaka mitano ijayo? Huyu kizazi cha 2000 naye atakuja kuwa mama je atakuwa mama wa misingi ipi kwa watoto wake?
Tanzania niipendayo ningetamani sana isimamie hiki kizazi kwa kuongeza vituo vya semina kwa mabinti katika ngazi ya kitongoji, kijiji, kata, wilaya, mkoa na kitaifa pia kwa kuanzisha clubs mbalimbali kama vile kutoa elimu na mafunzo ya namna ya kujilinda na kujitambua kama binti, maadili mema, mahusiano, afya na makuzi, kutoa mafunzo ya ujasiriamali kama vile kushona, masuala ya ususi na urembo upishi yenye gharama nafuu kwa kila likizo zao ambapo vituo hivi vinakuwa kama muendelezo wa elimu yao.
Hii itasaidia sana kupunguza muda mwingi wa kuzurura na kuingia kwenye makundi hatarishi. Lakini pia hii itamsaidia hata baada ya kumaliza elimu yake kuweza kujiajiri na kujipatia kipato kwa njia ya uhalali. Wengi wao hingia katika makundi hatarishi kwa dhumuni la kujipatia kipato ama mahitaji fulani ambayo hawawezi kuyapata kutoka kwa familia zao.
Watoto wengi wamekuwa ni watukutu na sio waelewa kwa wazazi wao kutokana na wazazi nao kutomudu gharama za kuwalea watoto wao kwa misingi yenye maadili mema kwa sababu wao wako busy kutafuta kipato sio usiku sio mchanga kutokana na kile wanachopata kutokidhi malengo yao, mwanamke akiinuliwa na kuwezeshwa umeokoa taifa zima. Wizara husika iliangalie hili na kuona italitatua kwa namna ipi ili nchi isonge mbele.

Upvote
4